mtoto wangu alipata shida wakati wa kuzaliwa

mtoto wangu alipata shida wakati wa kuzaliwa

zaka

Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
30
Reaction score
3
mwanangu alizaliwa kwa kuchelewa kabla ya mama kufanyiwa operetion
na baadae aliishiwa nguvu kiasi cha kulishwa kwa kumkamulia maziwa ya mama.

maendeleo yake kwa sasa, miaka2 inaonekana ni slow sana kimawasiliano, na hana balance
hajatembea bado, ila anapenda sana kucheza kwa kurusha miguu na mikono,

inasemekana alipata mshtuko kiasi kwamba anashindwa kutumia ubongo katika baadhi ya mambo.
kwa mfano uko mnyanyua na kumsimamisha hupenda kukunya miguu hivyo hajisupport...

je, kweli anaweza kutembea vizuri na maendeleo mengine baadae?
kwa sasa nampeleka muhimbili kwa ajili ya mazoezi kila wiki,
msaada tafadhali.....
 
sikumbuki vizuri, ni kama sikosei ni 4kg hivi ulikuwa mzuri tu...
 
Ondoa hofu ndugu akifanya mazoezi atakuwa sawa baada ya muda ila jaribu kumpa mazoezi pia nyumbani na si kusubiri mpaka wiki ipite uende muhimbili.
 
Swali:: je mama_mtoto alikuwa mtu wa mazoezi kipindi cha ujauzito? Au mtu wa hofuhofu sana? Alishawahi kuanguka mara kwa mara? Ana kifafa?

Ni muhimu utafute sababu kwanini mtoto wako amekuwa hivyo. Ili utapopata mwingine hiyo hali isijoykeze tena.

Pole sana
 
Pole sana ndugu, kuna matatizo mengi wakati wa uzazi. Wengine tulipoteza watoto kutoka na huduma isiyoridhisha kutoka kwa watoa huduma, watoto wa kiume kaka mama amekaa kwenye uchunguzi wanapata mfadhaiko haraka kuliko wa kike. Baada ya kuzaliwa anaweza kupata ulemavu au hata kifo.

Nakushauri uendelee kupata huduma za wataalamu. Pole sana na Mungu akusaidie katika kipindi kigumu.
 
Angalia km anasikia vzr coz hearing loss mara nying hupelekea m2 kukosa balance.
 
nenda kawaone wataalam wa neurology watakusaidi au muone Dr BITTA hapa Moi atakusaidia sana. but atapona hana shida
 
Back
Top Bottom