Mtoto wangu analia sana

Mtoto wangu analia sana

shangwe shangwe

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
108
Reaction score
24
Nisaidieni wadau, mtoto wangu analia sana hasa wakati au baada ya kunyonya. Anamwezi mmoja na wk 2. Nilishampa dawa nyingi kama daktari alivyo elekeza lakini bado anateseka. Naomba msaada wenu.
 
Gesi tumboni mkuu!jitahidi anyonye titi moja mpaka ashibe halafu mlaze begani mpige pige mgongoni mpaka acheue!hakikisha mtoto anacheua kila baada ya kula.ikishindikana mpe grip water
 
Kama alivyosema BONGOLALA,mumeo kwa kuwa ana kifua flat afanye hivyo.Pia mpe scott's mafuta ya samaki duka la dawa muhmu
 
Kama alivyosema BONGOLALA,mumeo kwa kuwa ana kifua flat afanye hivyo.Pia mpe scott's mafuta ya samaki duka la dawa muhmu
you mean cod liver oil? Asubiri kidogo, hiyo inaanza kutumiwa from 8 to 9 month hivi. At 1,5 mtoto bado mchanga, asimpe chochote zaidi ya maziwa yake.
Ahakikishe pia kua yeye mwenyewe anakula vizuri na anakunywa maji. avoid cabbage.
 
Wengine huwa wanasema mpeleke kwa bibi yake! Kulialia kutaisha.....
 
Hizo ni chango hakikisha mama anakula vyakula vya mzazi,then mtoto mpe mafuta ya samaki na jaribu kumkanda tumbo na maji ya moto.
 
Hiyo scott's kwa umri wake anapewa milimita 5.Mafuta hayo ni muhimu asikuambie mtu
 
Duh!navyojua miezi mitatu ya mwanzo ni kawaida ya watoto wadogo kulia.cha muhimu uhakikishe ameshiba, na kila unapomnyonyesha unatakiwa umuweke kifuani kwako huku umekaa ili gesi itoke, na uhakikishe kwmba nguo zake hazina mikojo.Huyo daktari aliyekushauri kumpa dawa nina wasiwasi na taaluma yake.Hizo dawa ulizompa umemuumiza bure.
Halafu hutakiwi kumpa chakula chochote mbali na maziwa ya mama(exclusive breastfeeding). huu utamaduni wa akina mama kusingizia kwamba mtoto hashibi halafu unampa kitu kingine, unamsababishia maumivu ya tumbo.
Kingine, kama una uwezo kidogo financially, seek advice from a paediatrician.kama uko dar, mwanza, arusha hao madaktari bingwa wanapatikana.Usipeleke mtoto mchanga kwa bora daktari, hasa kwenye vi-dispensary vya uswahilini.wengine sio madaktari, wamevaa makoti tu, watakuumizia mtoto.
 
Jiandae kulazwa hospitali kama utampa mafuta ya samaki.
 
Back
Top Bottom