Mtoto wangu anavimba kitovu wakati wa baridi

YohanaE

Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
5
Reaction score
2
Habari....
Mtoto wangu wa kiume ana miezi 2 toka azaliwe....anasumbuliwa sana na tumbo....wengine wanasema ngiri, wengine wanasena chango....kitovu chake ni kikubwa kiasi (kama golori) lakini ikitokea chango likambana ndo inakuwa kama kinavyoonekana katika picha...na analia sana kwa maumivu makali......naomba msaada/ushauri

 
Please mpeleke muhimbili haraka,ukaonane na daktari wa watoto,kuna wakongwe pale,fanya nae appointment,mtoto afanyiwe vipimo.
 

pole sana , hiyo ni Hernia..........

ikibana mpeleke hospitalini haraka sana , kwani inaweza kufanya pingamizi kwenye utumbo ambao ni hatari sana..
 
asante sana Asakuta....nilikuwa niko njia panda kwa sababu kinavimba, na baada ya muda mfupi kinapotea
sasa maneno ya watu ndo balaa....mama anasema na mimi nilikuwa hivyo hivyo ikaisha yenyewe tu, na dawa za kienyeji kidogo, shemeji anasema na mtoto wake ilikuwa hivyo hivyo....ni tumbo la chango tu....ila hernia hakuna aliyeniambia , THANX
 
Pole kwa maswahibu. Kila la heri mtoto apone aje kuwa sukari ya warembo. Mwanao kajaliwa dushelele. Hapo ana miezi miwili Madame B anamtamani. By the way kuna vile vifunga kitovu ambavyo vingi ni fake inaweza kuwa ni chanzo. Inashauriwa wamama wajawazito wawe na angalau vitatu kabla siku ya kwenda kujifungua. Pia pampasi sio nzuri hata kidogo kwa watoto wachanga. Namtakia mtoto afya njema, apone haraka.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ni umbilical hernia.

Tatizo hilo linasababishwa na ukuta wa tumbo kuwa haujafunga vizuri na hivyo sehemu ya utumbo unapenya na kuja mpaka chini ya ngozi. Hatari yake ni kwamba utumbo unaweza kuziba na kusababisha maumivu makali au hata mtoto kupoteza maisha iwapo hali ya namna hiyo haitatatuliwa mapema.

Kwa kawaida hizi hernia za watoto huwa zinapotea zenyewe kadri mtoto anavyokua, hata hivyo ushauri wangu kwako ni kuwa kwa vile huduma za afya za dharura nchini sio za uhakika. Hakikisha mtoto anafanyiwa operation mapema bila kungoja dharura. Huu ni ushauri wa kiujumlajumla, lakini iwapo mazingira yako yana uhakika wa kupata huduma ya dhararu iwapo itatokea hernia kuwa incarcerated basi unaweza kumuacha tu mtoto bila operation mpaka kuwe na emergency kwa matumaini kwamba itajifunga yenyewe kadri mtoto anavyokua.
 
asante sana Kwamtoro...
inawezekana ni vifungo fake... nitampeleka hospitali mapema
ila dushelele !!! ....hahahaha
 


asante sana ZeMarcopolo
ushauri wako ni mzuri sana....sikuwaza hata kidogo juu ya hernia, nilijua ni chango / ngiri
THANX
 

Pole ndugu,mm pia binti yangu alipata tatizo hilo alipokua na miezi miwili.Mpeleke Furaha Clinic ipo Morocco kwa Dr. Masawe atakusaidia.Namshukuru Mungu binti yangu aliponea hapo baada ya kuhangaika sana.Sasa ana miezi mitano na anaendelea vyema kabisa.
 
Kwa kawaida hernia kubwa kama hiyo sio hatari sana uwezo wa kubana ni mdogo sana kwa hiyo usiwe na wasiwasi sana. Kusema itaziba yenyewe akikua sina uhakika sana lakini inaweza tokea. Cha msingi ni observation tu kama ikitokea kikabanwa ndio akimbizwe hosp kwa ajili ya operation kama madaktari wataona inafaaa. Kumuwahisha hosp kwa ajili ya op kama alivyoshauri marcopolo mimi nisingeshauri mpaka walau akue kue kidogo.
 

Siku zote, ukiona mtoto ana tatizo la kimaumbile au kiafya kumpeleka hospitali akaonwe na wataalam ni jambo la hekima.

Picha inaonyesha kitovu lakini ukimshika mtoto na kumpima unaweza kugundua mengi zaidi!

Kufanya au kutokufanya operation ni uamuzi wa daktari atakayempima. Mimi nimeshauri hivyo kuwa sababu najua kuwa sio kila mtanzania ana access ya emergency surgical care. Unaweza kumshauri mtu angoje dharura wakati dharura ikitokea hana msaada!

Ukisoma kwenye vitabu wanashauri kama wewe ulivyoandika lakini vitabu hivyo havijaandikwa na watanzania wala havijaandikwa kukidhi mazingira yetu ambayo kuna wilaya nyingine zina daktari watano tu! Wenzetu eneo linalofanana na wilaya yetu kuna madaktari zaidi ya 200.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…