Mtoto wangu hacheki kwa sauti

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Mtoto wangu ana miezi Tisa now alhamdulilah yupo vema
Ila kuna kitu kinanipa hofu,hajui kuongea ila anapenda kuita baba,tata eeh tena kwa sauti kubwa kabisa.
Shida ipo kwenye kucheka akicheka hatoi sauti kabisa inatoka kidoogo hata umtekenye vipi.
Nifanyeje mwanangu acheke kwa sauti hadi majirani wasikie jamani?
 
Haaaaa hadi majirani wapate kicheko
 
...kwa sauti hadi majirani wasikie...

Ni mtoto wako wa kwanza?
 
Sasa wewe unataka acheke kwa sauti ili nini? Au unataka awe mmbea? Ila kama unataka kulazimisha mwekee subwoofer
 
Hakuna shida hapo......ni hzo reflex tu bado zijatengamaa kwake......usijari...kwan kwnye kulia VP? Napo hatoi sauti
 
Nenda kwenye Setting kisha Restore Factory au Kwenye Audio Profile bonyeza General ataanza kucheka kwa sauti.
Duh! hiyo setting ipo wapi mkuu, au ipo sehemu gani kwenye mwili? Hata mimi kuna vitu nataka nijifanyie setting
 
Mpeleke hospital asije akawa bubu........... Usipuuze
 
Vipi akiachia ushuzi sauti inatoka?
Ahahaa kipindi nimejifungua maziwa yalikuwa hayatoki so nikawa nampa ya kopo .alikuwa anajamba mtaa mzima ahaa acha tu.siku hizi anapupu pupu tu sana maana anakula kula kama mi maza ake
 
Ahahaa kipindi nimejifungua maziwa yalikuwa hayatoki so nikawa nampa ya kopo .alikuwa anajamba mtaa mzima ahaa acha tu.siku hizi anapupu pupu tu sana maana anakula kula kama mi maza ake
Basi punguza hofu mwanao atacheka kwa sauti mpk watu wahisi unafuga fisi .

BTW ni mtoto wa kike au wa kiume?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…