Mtoto wangu hapati choo vizuri naombeni ushauri

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Mtoto wangu tangu azaliwe sijui ana janga gani alikuwa anapata choo mara moja kwa week nilimuuliza Dokta akasema haina shida sasa hivi ameanza kula misosi bado hapati choo fresh ukizingatia anakula chakula vizuri tu.

Halikadhalika ananyonya,nakablendia vyakula laini,nakapa juice papai likiwepo ,maji kanakunywa,mafuta ya samaki,grape water nayo nampa hana shida yoyote ila natamani mtoto wangu apupu kila siku
Naombeni ushauri
 
Umri wake,
Inachukua muda gani hadi kupupu,
Anakula mara ngapi kwa siku,??
Hiyo hali haswa umeanza kuiona lini baada ya kuanza kula misosi ya nguvu??
 
Ana umri gani mtoto wetu?
 
Kama hana tatizo according to doctor usijali ila kupupu nako vinakera wangu alikuwa anapupu tuu nikimweka kwenye beseni kumwogesha natamani umpatee
 
Kwa mtoto mdogo kupitisha siku 2-3 bila kupata choo si kawaida, kutakuwa kuna shida kidogo.

A) Kwa mtoto anayenyonya.
Unatakiwa ujue kama mtoto ananyonya vizuri, vile vile uzingatie hali ya lishe ya mama kwasababu hiyo ndo huchangia kwenye kutengeneza maziwa ya mama.

Kwa kawaida kiafya mtoto anatakiwa anyonyeshwe dakika 20 ziwa moja. Kwasababu unyonyaji wa mtoto dakika 10 za mwanzo kinachotoka ni maji kwa wingi pasipo kuwa na nutrients za kutosha kwenda kwa mtoto, dakika 10 zinazofuata ndo kunakuwa na nutrients za kutosha.

Akina mama walio wengi hawafuati/hawajui utaratibu huu hivyo kupelekea mtoto kuhamishwa hamishwa manyonyo hata kabla ya dk 10. Hivyo kupelekea mtoto kupata maji ziwa hili na kumalizia kupata maji ziwa lingine, anakosa virutubisho vya kutosha, hivyo kupelekea shida katika upatikanaji wa choo.

Endapo mtoto ananyonya vizuri na tatizo likaendelea kuwepo kuna uwezekano mkubwa kukawa na shida katika mfumo wa chakula (Mara nyingi tumbo linakuwa kubwa na anaweza kupata maumivu makali ya tumbo.

B) Mtoto anatakiwa apewe chakula chenye nyuzinyuzi (fibres) kwa wingi, ambavyo ni pamoja na:-
-Matunda
-Mboga za majani
-Maji ya kunywa ya kutosha.
Inashauriwa mtoto mwenye mwaka 1-2 anywe lita 1.3 kwa siku.
-Vyakula vyenye maji maji.

Hivyo basi jaribu kuangalia wapi haupo sahihi katika lishe ya mtoto ili urekebishe. Endapo tatizo litaendelea jaribu kufika hosp. kwa uchunguzi zaidi.
 
Oooh shukrani sana Mkuu umenipa mwanga sana hapo kwenye kunyonyesha namuamisha ziwa fasta fasta tu me nachoka bana kumbe inatakiwa dakika kumi?
 
Oooh shukrani sana Mkuu umenipa mwanga sana hapo kwenye kunyonyesha namuamisha ziwa fasta fasta tu me nachoka bna.kumbe inatakiwa dkk kumi???
Sio wewe tu, wamama wengi kwa kutokuwa na elimu juu ya unyonyeshaji wa watoto wamekuwa wakihamisha hamisha watoto toka ziwa moja kwenda ziwa lingine wakifikiri ziwa moja limepungukiwa maziwa hivyo kumbadilishia mtoto ziwa ndani ya muda mfupi sana.
 
Pendelea Kulisha Lisha Mapapayi Au Juice Yake....!!!

Ila Tangu Uolewe Umekuwa Busy Na Ur Family
 
Sio wewe tu, wamama wengi kwa kutokuwa na elimu juu ya unyonyeshaji wa watoto wamekuwa wakihamisha hamisha watoto toka ziwa moja kwenda ziwa lingine wakifikiri ziwa moja limepingukiwa maziwa hivyo kumbadilishia mtoto ziwa ndani ya muda mfupi sana.
Ila unaona limeisha maziwa kabisa.dkk kumi nyingi sana Mkuu hata mtoto mwenyewe hatonyonya sasa
 
Huyo Mtoto Namuhurumiaa...

Na ww Mama?!!???!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…