SoC02 Mtoto/ Watoto wako wenye vipaji/talent unawasaidiaje wakati huu?

Stories of Change - 2022 Competition

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Ni ukweli Usiopingika kwamba Mifumo yetu ya elimu ni mibovu sana, inaangalia Div 1 ya 7 au Div 1 ya 3 basi na ni mifumo ya enzi za Uhuru na wakati huo huo kuna changes nyingi sana Duniani tangia 1960 hadi leo hii.

Utafiti uliowahi kufanywa na Chuo kikuu cha Harvad Marekani ulikuja na matokeo yafuatayo;

Watoto 1200 waliwahi kufanyiwa utafiti na matokeo yakawa kama ifuatavyo;

1. Kabla hawajaanza shule kabisa asilimia 90 ya hao watoto walikuwa na ubunifu wa kuzaliwa nao na kulikuwa na kila dalili ya wao kuja kufika mbali sana kiubunifu.

2. Baada ya miaka 9 hapo walishaanza shule sasa mfano kama ni Tanzania wapo Chekechea au kindagateni huko wanapigishwa Home work maswali 70 na wakagundua idadi imeshuka iko asilimia 30 tu maana yake hao wengine tiyari wameisha inject yale mambo walimu wanawafundisha.

3. Wakiwa Secondary sasa ile asilimia 30 ikaja fanyiwa utafiti na wakagundua imebakia asilimia 12 tu, wengine wote walisha poteza ile talent na wameingiza vitu kama types of Rock, River, Types of Dictatorship na kadhalika mfano.

4. Baada ya miaka kibao tangu wamalize shule zao wakaja fanyiwa tena hio asilimia 12 ikawa imebakia 2 tu, maana yake hapa wengine walisha ajairiwa na Mishahara isha wapumbaza, zile Posho na kadhalika.

Maana yake hapa, Ile talent ya asili, inapotea kadri mtoto anavyo endelea kupokea formal education, Sema wazazi wanao gundua hili mapema huwa wanawasaidia sana watoto wao na pia wengine hukumbana na bahati ya Kuto endelea na shule au kuto kusoma kabisa kwa sababu za umasikini, na hapo ndio huwa advantage kwao.

Nakubaliana na huo utafiti kabisa na sisi humu ni ukweli kwamba watoto wetu wana natural talents za kuzaliwa nazo ila kwa sababu mifumo inataka tunawapeleka shule sasa kuna kila dalili zile talents zitapotea kumbuka mifumo yetu ya elimu haina mazingira ya kulea vipaji na vipaji wanavyo vijua Serikali ni vya Div 1 ya 7 au ya 3.

Shuleni wanaenda kuinjectiwa kuchomwa sindano ya vitu vipya kabisa vya watu wengine, wanapaswa sasa wajue kuna mito mingapi Tanzania, wajue kuchora ramani ya Africa na kadhalika.

Swali ni je tunawasaidia vipi kwa hali ya sasa? Make huenda hicho kipaji chake ndo kikaja kumtoa na wala sio hio shule anayo komaaa nayo sasa.

Vitu tunavyo weza kufanya Wazazi pamoja na hali zetu za vipato kuwa Duni ila wengine vipato vinaruhusu.

1. Mtoto wako ana Kipaji my be Cha Kuchora- Hakikisha facility zote za kuchorea anazipata, kwa namna yoyote ile na hakikisha baada ya masomo ya shuleni yeye ni kuingia kupractise kipaji chake, ondo vitu vinaitwa sijui tuiotion kwa mtoto wako, na kama kuna taasisi au Centre ya vipaji ya Kuchora mpeleke huko faster muda ambao sio wa shule awe kule.

Pia Ongea na Walimu wake shuleni kwamba mtoto ana kipaji ha kuchora hivyo wawe wanamtumia.

2. Mtoto wako ana sauti nyororo ya kuimba kama ya Whitney Huston, hakikisha anaelekea huko huko na daily awe ana practise na akitoka shule hizo ndo home work zake, na awe ana present ila pia kama kuna centre za watoto kujifunza kuimba mpeleke pia na ukiwezi kumtambulisha kwa waimbaji hata kama sio wale wakubwa sana itapendeza sana pia anapata confidence na Exposure.Kama uwezo unaruhusu tafutia yeye mwalimu wa mziki.

3. Mtoto kipaji chake ni cha kucheza na computer komaaa naye huko huko mnunukie computer na vifaa vingine na mpatie home work za kufanya na pia kama uwezo una ruhusu leta mtu wa kumsaidia.

4. Mtoto anapenda pet animal sana kama Mbwa na Paka basi ndo uelekeo wake uliko, kuna matajiri wa mbwa tu na Paka.

5. Anapenda Mpira na ukiona kabisa dogo ana kipaji kama cha Ronardo De Lima komalia hapo hapo, na hakikisha una mling na taasisi au vituo ya watoto vya mpira na hakikisha sehemu kama uwanjani hakosekani kutazama wenzake, mkutanishe na wachezaji wakubwa na wadogo kama inawezekana, Hakikisha muda wote wa ziada baada ya masomo ni mpira tu mwanzo mwisho.

Na vipaji vingine vingi kama Sarakasi, Kukimbia, kupenda kuogelea, mtoto kupenda maigizo maigizo na kadhalika.

Shida kubwa mifumo yetu ya elimu inaua vioaji ya asili kwa sababu shuleni pale ni mwendo wa kusoma na mitihani na mtoti I nabidi akariri sana afaulu make kuna kushindana wa kwanza na wa mwisho.

Unakuta mtoto baada ya shule ni either tuition, au homework, mtoto anapoteza kujiamini na kile kipaji chake make wazazi nyumbani wanataka tu waone karatasi kawa wa ngapi au kapata max ngapi, hivyo mtoto anapoteza confidence kabisa na kipaji kinaisha anabakia sasa asome akatafute kazi tu.

Fikilia mtu kama Dimond kama angesoma hadi Chuo kikuu, huenda angekuwa ni mfanya kazi wa Halmashauri fulani, lakini kumbe ile kuto endelea sana na shule kulimsaidia.

Ila pia unaona mtoto ana kipaji real na shule ni kama hapendi basi acha aendelee na kile kipaji chake, au mwambie wewe hata Darasani ukiwa wa mwisho usijali niko na wewe, endelea kuzuga zuga tu shuleni.

Tumepoteza sana vipaji kwa sababu ya mifumo mibo ya elimu, ila pia kutokana na Wazazi kuju kwamba kusoma ndo kila kitu.

Sisi tuna Exposure, tunajua Dunia inavyo enda hebu tuwasaidie watoto wetu wenye vipaji, Ndoto zao zisiishie njiani.

Wasaniii wengi na awavumbuzi wengi kilicho waokoa ni Mazingira ya maisha yalio fanya wasiendelee na Formal Education na pia kuna walio gundua mapema na waka drop out.

Formal Education ni nzuri ila kama mtoto wako ana kipaji cha asili cha kuzaliwa nacho basi Formal education inaweza futa hicho Kipaji chake cha asili.
 
Upvote 5
Kwa nchi za kiafrika watu wengi wana Amin maisha mazuri/mafanikio yapo kwenye elimu ya darasani pekee na sio kipaji.
 
Inawezekana lakini tunapaswa kuanza mapema Sana kuvijua vipaji vya watoto wetu kabla ya kujiunga na elimu rasmi
 
Baada ya kuusoma uzi wako huu nimebaini kwamba mimi na wewe tuna maono yanayolandana!. Binafsi nimeshaanza kulitafutia ufumbuzi wa kudumu janga hili na Mungu yupo karibu sana nami katika hili.
 
Wazazi wengi wako bize kutafuta hawana muda wa kukaa na watoto ili kujua vipaji vyao.

Waalim wa shule za awali wana nafasi kubwa ya kujua vipaji vya watoto, ila na wenyewe hawajawekwa kimfumo wa kutambua hayo.

Pia wazazi tunaamini tuwaache wasome ili wapanue uelewa, kumbe ndo elimu hiyo hiyo inafuta kipaji cha kuzaliwa na kupanda kitu kingine.
 
Walimu hawana huo Muda, na nyakati formal Education ni ya kutoa ujinga tu, na pia tusidhanie hili swala la ukosefu wa ajira litapungua no
 
Baada ya kuusoma uzi wako huu nimebaini kwamba mimi na wewe tuna maono yanayolandana!. Binafsi nimeshaanza kulitafutia ufumbuzi wa kudumu janga hili na Mungu yupo karibu sana nami katika hili.
Karibu sana mkuu, hii ni muhimu sana, watoto wana zika vipaji vyao kwa juwa force kuingiza vitu ambayo hata hivyo hawatavifanyia kazi.
 
Namimi ninaungana na wewe mtoa mada kwahili na ni janga la kitaifa na endapo hatua muhimu zikiweza kuchukuliwa, tunaweza kuleta kitu muhimu sana ambacho kinaweza kuwa na tija kwa jamii..

Ninazungumza hili nikiwa ni miongoni mwa wahanga wa tatizo hili sababu, katika familia ukiwa unakipaji cha asili ni wazazi asilimia sio zaidi ya 10 wanaotambua umuhimu wa vipaji vya asili kwa jamii zetu.
Kama vijana na wadau wa jukwaa hili, ni maoni yangu kuwa tungeweza kuleta michanganuo yenye tija kwa mustakabari wa taifa letu na vizazi vyetu ilikuhakikisha kila sehemu ya Tanzania! Angalau kunakuwepo na vituo maalumu kwaajili ya kuendeleza vipaji vya asili kwa vijana wetu.

Nadhani tungeweza kuwa na uwanja mpana wa kujadiri hoja na mwisho wa siku tukaleta kitu kimoja ambacho kinaweza kuwa na mjumuiko wa mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kumtoa kijana katika ombwe ya kujiona anaweza kufanya vitu vingi zaidi pasipo kutegemea ajira.

Jamii zetu za sasa tumekuwa tukilaumu sana na kuwadharau hasa wasomi wa sasa kwakushinda kutwa kutafuta ajira pasipo kuilaumu mifumo ambayo inamfanya kijana huyu wa sasa asiwaze maisha mengine tofauti na ya ajira.

Katika jukwaa hili nadhani ni vyema tuainishe labda mawazo mbadara ambayo tukiweza kuyaunganisha nadhani tunaweza kuleta kitu very special kwaajili ya ustawi wa taifa letu.

Binafsi ninamawazo machache ambayo kwa upande wangu naona yanaweza kuwa na msaada kwa taifa letu kama tukiyachanganua na kuongeza mawazo zaidi huenda tukapata kitu kipya.

1). ELIMU YA KUJITEGEMEA

Miaka ya nyuma kulikuwa na mafunzo ya stadi za maisha ambazo ndizo zilikuwa zinaongeza kitu katika ujuzi wa kijana, miaka ya sasa elimu hizi hazitolewi tena sijui ni sababu ya nini! Lakini niimanj yangu kuwa, kama elimu hizi zikianzishwa tena pamoja na ujasiliamali na zikawazinatolewa sio tu kwa ngazi ya elimu ya primary bali ziende hata katika elimu za juu kwa kuzingatia swala la mnyororo wa thamani nadhani inaweza leta kitu katika safari ya kijana wa sasa.

Mfano; ukizungumza katika elimu ya Sanaa basi Sanaa iwe inafundishwa kwa kuipambanua kwa mitindo tofauti tofauti sababu ukiuchukulia Muziki unakuta ni kitu kimoja lakini ndani yake kunakuwa na fursa nyingi sana ambazo zikiunganishwa kwa pamoja ndipo tunaupata muziki ukiona vionjo na ladha ya kuvutia.
Vivyo hivyo pia hata katika kilimo, ujenzi, mpira nk.
Vijana pia waeleweshwe jinsi ya kupata mitaji, jinsi ya kuwekeza na namna mbalimbali.

2). UANZISHWAJI WA VIKUNDI MBALIMBALI KWAAJILI YA SHUGHURI FULANI.

3). MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII

4). MOTISHA KATIKA UVUMBUZI WA MASWALA MBALIMBALI YENYE MASLAI MAPANA KWA TAIFA nk.

Mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…