Mtoza ushuru kanipiga elfu 5 Daraja la Kigamboni

Mtoza ushuru kanipiga elfu 5 Daraja la Kigamboni

Habari,

Tunamshukuru Mungu kwa kutuamsha salama, na anatuwezesha kuendelea na harakati za maisha ya kila siku. Utukufu ni wake.

Asubuhi hii huku mvua kubwa ikinyesha nikafika pale darajani, na kutoa elfu 10 ili nilipie gharama za kuvuka.

Mtoza ushuru huyu, kijana tu akafanya haraka kunirudishia change pamoja na risiti, kwa sababu ya haraka nikaipokea na kuweka kwenye kiti nikaondoa gari.

Nafika kazini, kuangalia kwenye siti nikaona kuna elfu 3.5 na elfu 5 sikuiona. Nikaitafuta kweli labda imeanguka mle ndani lakini wapi, baadae nikajisemea sio rahisi ianguke noti moja pekee na zingine zibaki intact.

Ndipo, nikagundua yule dogo kanipiga, huenda aligundua kwa sababu ya mvua ile watu watakuwa na haraka na kushindwa ku concentrate sana.

Nimemsamehe, Ila Vijana hasa kwenye ofisi za umma tuache tamaa na kujihusisha na TABIA ZA UDOKOZI. Sio sawa, ni laana. Muda mwingine nitajitahidi kuwa nahesabu.

Uzi tayari. Nawatakia majukumu mema
Pole sana amekuvurugia bajeti ya supu itabidi upige chai chapati tu na maji madogo
 
Jisajili kwenye CASHLESS SYSTEM utaepuka mambo ya chenji na mengineyo.
 
Kwa asilimia kubwa ni uzembe wako mwenyewe ndio uliochangia kupoteza hio 5,000.
Kutokuhesabu pesa unayokabidhia ni makosa yako.
NADHARIA
1)Inawezekana alikupa change kamili wewe ndio umeidondosha.
2)Inawezekana ulimpa 5,000/- ila ukahisi umempa 10,000/-
3)Inawezekana ulimpa 10,000/- ila mtoza ushuru akahisi alipewa 5,000

Ungekua makini wakati wa kurudishiwa change hizi nadharia zisinge kuwepo.
Kwa hii situation binafsi siwezi kumtuhumu mtoza Ushuru.
 
Mkuu hapo huna uhakika kama kweli kakuibia pengine ulirudishiwa umeangusha au umei misplace tu.
Any way siku nyingine hesabu hela yako kabla hujaondoka.
 
Kwa asilimia kubwa ni uzembe wako mwenyewe ndio uliochangia kupoteza hio 5,000.
Kutokuhesabu pesa unayokabidhia ni makosa yako.
NADHARIA
1)Inawezekana alikupa change kamili wewe ndio umeidondosha.
2)Inawezekana ulimpa 5,000/- ila ukahisi umempa 10,000/-
3)Inawezekana ulimpa 10,000/- ila mtoza ushuru akahisi alipewa 5,000

Ungekua makini wakati wa kurudishiwa change hizi nadharia zisinge kuwepo.
Kwa hii situation binafsi siwezi kumtuhumu mtoza Ushuru.
Sawa,
 
Back
Top Bottom