Habari,
Tunamshukuru Mungu kwa kutuamsha salama, na anatuwezesha kuendelea na harakati za maisha ya kila siku. Utukufu ni wake.
Asubuhi hii huku mvua kubwa ikinyesha nikafika pale darajani, na kutoa elfu 10 ili nilipie gharama za kuvuka.
Mtoza ushuru huyu, kijana tu akafanya haraka kunirudishia change pamoja na risiti, kwa sababu ya haraka nikaipokea na kuweka kwenye kiti nikaondoa gari.
Nafika kazini, kuangalia kwenye siti nikaona kuna elfu 3.5 na elfu 5 sikuiona. Nikaitafuta kweli labda imeanguka mle ndani lakini wapi, baadae nikajisemea sio rahisi ianguke noti moja pekee na zingine zibaki intact.
Ndipo, nikagundua yule dogo kanipiga, huenda aligundua kwa sababu ya mvua ile watu watakuwa na haraka na kushindwa ku concentrate sana.
Nimemsamehe, Ila Vijana hasa kwenye ofisi za umma tuache tamaa na kujihusisha na TABIA ZA UDOKOZI. Sio sawa, ni laana. Muda mwingine nitajitahidi kuwa nahesabu.
Uzi tayari. Nawatakia majukumu mema