Mtu adaiwa kufufuka nchini Msumbiji

Mtu adaiwa kufufuka nchini Msumbiji

DreezyD98

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2020
Posts
1,610
Reaction score
2,874
Kijana mmoja kaskazini mwa Msumbiji ambaye alidhaniwa kuwa amefariki dunia na ambaye mazishi yake yalifanyika mwezi Novemba ametokea kijijini kwao Lindi.

Jumuiya inamtaja Eurélia Manuel Benjamim kama mtu aliyefufuka kutoka kwa wafu, lakini anasema alikuwa ameenda tu kufanya kazi katika shamba la mjomba wake kwa miezi michache.

Msimamizi wa eneo katika wilaya ya Montepuez aliambia mtangazaji wa serikali: “Walifanya sherehe zote za mazishi - mazishi, sherehe ya siku ya tatu na kutembelea kaburi - na kaburi halijavunjwa.”

Kikosi cha wataalamu kinatumwa Lindi kufanya uchunguzi ili kuona ni nani au nini kilizikwa kaburini.

Source: BBC SWAHILI
 
Nilijua haya mambo yapo Tz tu kumbe hata Msumbiji kuna vibweka🏃‍♂️

Afrika na baadhi ya maeneo ambayo Waafrika walifika kama watumwa na wakashikilia mila zao, hizi mambo zipo sana
 
amezikwa kabisa Ndugu wame hakikisha

Sasa si wamezika kitu kinachofanana na mtu wao...

Kuna mchawi mmoja alikuwa anatoa ushuhuda baada ya kuachana na hizo mambo, kuwa mwanadamu ana uwezo kujigawanya na kuwa hata mara tatu au zaidi...

Yaani mfano wewe afisa manispaa ujigawanye na muwe watatu kama kirusi kinavyojigawa vile...
 
Back
Top Bottom