mtu ambaye amekuwa akiwazuia nyie msipate mafanikio amekufa

mtu ambaye amekuwa akiwazuia nyie msipate mafanikio amekufa

BOB OS

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
3,440
Reaction score
6,881

Siku moja wafanyakazi wa kampuni walifika ofisini ,na walioona tangazo kubwa kwenye mlango limebandikwa
“jana mtu ambaye amekuwa akiwazuia nyie msipate mafanikio amekufa.tunawakaribisha katika chumba cha mazishi ambacho kimeshaandaliwa kwenye gym”.Mwanzoni walikuwa na huzuni kutokana na kifo cha mfanyakazi mwezao,lakini baada ya muda kidogo wakawa na shauku ya kujua ni nani amekuwa akiwazuia wasipate mafanikio pamoja na kampuni.


Msisimko kwenye gym ulikuwa kwa askari wa usalama walikuwa na amri ya kuzuia umati wa watu ndani ya chumba.jinsi watu walivyokuwa wanakaribia jeneza ndivyo msisimko ulikuwa unaongezeka.kila mtu alikuwa anawaza “Ni mtu gani huyu alikuwa anafanya sipati maendeleo”, afadhali ameshakufa!” mmoja baada ya mmoja wale wafanyakazi walipofika karibu na lile jeneza, na walipokuwa wanaangali ndani ya jeneza ghafla wakawa kimya.walisimama karibu na jeneza kama watu waliotishwa huku wakiwa kimya kama mtu ambaye ameguswa nafsi yake.Kulikuwa na kioo ndani ya jeneza,kilamtu ambaye alikuwa akiangalia kwenye jeneza alijioona yeye mwenyewe.

Kulikuwa na alama kwenye kioo ikisema kwamba “ Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza kuweka mipaka ya ukuaji wako ambaye ni wewe” . wewe ni mtu pekee ambaye unaweza kubadilisha maisha yako .wewe ni mtu pekee ambaye unaweza kushawishi furaha yako.utambuzi wako ndio mafanikio yako.wewe ndio mtu pekee ambaye unaweza kusaidia maisha yako.maisha yako hayana mabadiliko wakati ,rafiki zako wamebadiliko,jirani zako wamebadilika,ndugu zako wamebadilika.maisha yako yanabadilika pale unapobadilika,unapokwenda zaidi ya mawazo yako unayoamini,ndipo utagundua wewe ni mhusika mkuu wa maisha yako. “Uhusiano muhimu zaidi ambao unaweza kuwa nao katika maisha yako ni huo ulionao mwenyewe”




Ujumbe:dunia ni kama kioo:kinatoa taswira ya mawazo ya mtu anayeyaamini.dunia na ukweli wako ni kama kioo kilicholazwa katika jeneza,ambacho huonyesha kifo cha mtu aliyeshindwa kutumia mawazo yake ya kufikiri pamoja na uweza aliopewa na Mungu wa kujenga furaha yake na mafanikio yake.
 
Back
Top Bottom