Mtu anae dhaniwa kuwa ni jambazi ni nani hasa?

Mtu anae dhaniwa kuwa ni jambazi ni nani hasa?

DZUDZUKU

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2012
Posts
3,909
Reaction score
2,115
Habari wandugu,
Mie nnaswali moja, hivi mtu anaedhaniwa kuwa ni jambazi ni mtu wa aina gani hasa?
Mtu amekutwa eneo la tukio akifanya wizi, anauawa na wananchi baadae vyombo vya habari vinaripoti "mtu alie dhaniwa kuwa ni jambazi ameuawa" Inakuwaje huyu mtu aliekutwa kwenye wizi akawa anadhaniwa kwa wizi?

Nawasilisha.
 
jambazi ni mtu anayejihusisha na wizi kwa kutumia silaha(hasa silaha za moto) hawa wengine wanaingia ktk makundi ya vidokozi,vibaka.ni makosa kusema kuwa kila anayekutwa eneo la wizi ni jambazi
 
"Anadhaniwa..." Kwa Kuwa Kisheria haijathibitika, ... MTU hubakia Kuwa mtuhumiwa hadi Mahakama itakapo mtia hatiani kwa ushahidi usio na shaka.
 
kudhaniwa ina maana kwamba haijathibitishwa!

hivyo basi mpaka polisi ama wananchi watoe ushahidi vyenye vielelezo ndipo ataitwa jambazi.
 
Back
Top Bottom