Mtu anajifunza biashara au anazaliwa akiwa anachembechembe za biashara?

Mtu anajifunza biashara au anazaliwa akiwa anachembechembe za biashara?

MY LOVE

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
161
Reaction score
68
An entrepreneur is born or made? Naomba mnisaidie ndugu zangu kwani maisha ya kusubiri ajira yamenishinda sasa. Nafikiria kuwa mfanyabiashara au mkulima lakini sina hata moja ninalolijua juu ya biashara wala kilimo jinsi ya kuanza mpaka kufanikiwa, nasikia kuna makabila Fulani wao niwafanyabiashara kuanzia babu mpaka kitukuu hata kama hajasoma lakini anauwezo wakufanya biashara na ikafanikiwa kuliko msomi mwenye degree kadhaa, ktk hili kuna siri gani? mimi sijazaliwa ktk hiyo jamii na elimu ya Bongo niliyopata haikuniandaa kuwa mjasiriamali wala mkulima tunadanganyana ukimaliza tu unapata ajira. Sasa nitajifunzia wapi kuwa mfanyabiashara mzuri au mkulima mzuri bila kupata hasara kubwa? kwani nimeona baadhi ya watu walioingia kichwa kichwa kwenye biashara au kilimo na wakafilisika hata kile kidogo walichokuwa nacho.
 
waulize wachagga watakujibu vizuri sana maana kwao mtu yyte anaweza fanya biashara na akafanikiwa vizuri,
secret behind me is to respect money unaweza fanya biashara mtu yyte
 
mtu akizaliwa anakuwa kama empty CD... Unarekodi unachokitaka.. Hivyo basi mtu kujuwa biashara, inategemea katika mazingira aliyopitia kabla ya kuanza hiyo biashara. Kama kaishi na wafanya biashara basi naye atakuwa hivyo na itakuwa ni shughuri anayoiweza kuliko nyingine
 
mtu akizaliwa anakuwa kama empty cd... Unarekodi unachokitaka.. Hivyo basi mtu kujuwa biashara, inategemea katika mazingira aliyopitia kabla ya kuanza hiyo biashara. Kama kaishi na wafanya biashara basi naye atakuwa hivyo na itakuwa ni shughuri anayoiweza kuliko nyingine

hilo ndo jibu,hata ma scientist watakujibu hivyo,nje ya hapo hakuna jibu.mtu akizaliwa anakuwa tabula rasa yaani zero brain.anapata mawazo kutokana na na mazingira.mbona kuna wachaga wachovu wanabangaiza?si wote wanajua biashara.
 
Ujue nn mkuu, cos ushajitambua no need to dought, jifunge mkanda na jifikirie kipi kati ya kilimo na biashara ni rahis kutoka ktk mazingira yako, then ukipata jibu anza kuchukua hatua including making different researchs to those who hv succeded. Kikubwa ni kumwomba mungu na kutokata tamaa. B blecd
 
Entrepreners are Born na vilevile wa made, Watu huzaliwa na talent fulani, Wakina Thomas Edson hawakujifunza popote pale, wana Michael Dell, wakina Henery Ford, wawanao zliwa na talent na kujakufanya jambo kubwa sana,

Ila wapo ambao ni Made, hawa hujifunza kutokana na mazingira na hi kundi ndo lin wajasirimali wengi, Born Entrepreners ni wachache sana huku Duniani, wengi ni Made,

Wahindi wko kwenye hii category ya Made, Chukulia watoto waKihindi wanaaza kujua biashara tangu wakiwa wdogo,

HII MAADA NILISHAIZUNGUMZIA SANA SO SITAINGIA KWA UNDANI SANA, TAFUTA THREAD ZANGU
 
Siri ya kupata mali ni rahisi sana. Hakikisha by hook or crook kwamba hela inaingia kwa kasi kuliko inavyotoka. Sasa tafakari biashara zipi zitakuwezesha hili.
 
An entrepreneur is born or made? Naomba mnisaidie ndugu zangu kwani maisha ya kusubiri ajira yamenishinda sasa. Nafikiria kuwa mfanyabiashara au mkulima lakini sina hata moja ninalolijua juu ya biashara wala kilimo jinsi ya kuanza mpaka kufanikiwa, nasikia kuna makabila Fulani wao niwafanyabiashara kuanzia babu mpaka kitukuu hata kama hajasoma lakini anauwezo wakufanya biashara na ikafanikiwa kuliko msomi mwenye degree kadhaa, ktk hili kuna siri gani? mimi sijazaliwa ktk hiyo jamii na elimu ya Bongo niliyopata haikuniandaa kuwa mjasiriamali wala mkulima tunadanganyana ukimaliza tu unapata ajira. Sasa nitajifunzia wapi kuwa mfanyabiashara mzuri au mkulima mzuri bila kupata hasara kubwa? kwani nimeona baadhi ya watu walioingia kichwa kichwa kwenye biashara au kilimo na wakafilisika hata kile kidogo walichokuwa nacho.

Mkubwa kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara iwapo hana woga na iwapo ana nidhamu ya pesa.
Hapo pekundu mkuu panaonesha tayari wewe una woga,una roho ya kusita,hiyo roho ya kujiuliza itakuaje iwapo nitafanya halafu biashara isiwe kama ninavyotarajia ndio itakayokufanya usiwe mjasiriamali.

Umeuliza unawezaje kufanya biashara bila kupata hasara kubwa,ukweli ktk ulimwengu wa utafutaji hakuna guarantee ya kutopata hasara,kinachotakiwa ni kutumia akili kupunguza uwezekano wa kupata hasara.Hata wafanyabiashara wakubwa,wamepata hasara mara nyingi tu lkn kwa njia moja au nyingine waliweza kusimama na kufika hapo walipofika.

Kuna topic moja ya mkuu Chasha inayozungumzia wagiriki kuchoma meli zao,ukiisoma ile topic utajua kuwa ili kuwa mjasiriamali unatakiwa uwe na roho ngumu kama ya mwanajeshi ambaye anajua kuwa ni lazima ashinde maana asiposhinda basi atapoteza uhai wake.Kupata hasara kupo na kutaendelea kuwepo,ila unapopata hasara unachotakiwa kufanya ni kujua kwanini umepata hasara ili usirudie kilichofanya hasara.

Vile vile ujasiriamali unataka mtu uwe na nidhamu ya pesa,sio mtu biashara inakuingizia faida ya 3M kwa mwezi halafu wewe unaspend 2.5M halafu unasave 0.5M,hapo utachemsha,maana iwapo itatokea umepata hasara kubwa ikakata nusu ya mtaji,ina maana faida uliyosave haitatosha kuisimamisha tena biashara.Vile vile ukisave kiasi kikubwa ina maana una nafasi ya kupanua biashara yako baada ya muda fulani,la sivyo biashara yako itakua kwenye level ile ile miaka nenda miaka rudi.
 
Last edited by a moderator:
Mie my great grandfather yaani babu yake baba yangu mzazi nimeambiwa alikua mfanyabiashara,akaja babu yangu nae mfanyabiashara,akaja baba yangu pia mfanyabiashara so familia yangu imeanza biashara toka vizazi nyuma lakini nilivyotaka kuanza mie ilibidi kuanza kujifunza toka hatua ya mwanzo kabisa so kwa uzoefu wangu hivi vitu unajifunza tu acha uoga,maana kama kuzaliwa nacho kipaji mie ningekua nacho bro u should learn ziko njia nyingi za kujifunza ila cha muhimu uwe na passion na ujasiriamali wenyewe sio tu kwakua bosi wako leo kakufokea unakurupuka mie sitak tena kuajiriwa tehtehteh natania!
 
You can do absolutely anything as long as you put yourself up to it. It aint easy but you can make it. GO!
 
Mkubwa kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara iwapo hana woga na iwapo ana nidhamu ya pesa.
Hapo pekundu mkuu panaonesha tayari wewe una woga,una roho ya kusita,hiyo roho ya kujiuliza itakuaje iwapo nitafanya halafu biashara isiwe kama ninavyotarajia ndio itakayokufanya usiwe mjasiriamali.

Umeuliza unawezaje kufanya biashara bila kupata hasara kubwa,ukweli ktk ulimwengu wa utafutaji hakuna guarantee ya kutopata hasara,kinachotakiwa ni kutumia akili kupunguza uwezekano wa kupata hasara.Hata wafanyabiashara wakubwa,wamepata hasara mara nyingi tu lkn kwa njia moja au nyingine waliweza kusimama na kufika hapo walipofika.

Kuna topic moja ya mkuu Chasha inayozungumzia wagiriki kuchoma meli zao,ukiisoma ile topic utajua kuwa ili kuwa mjasiriamali unatakiwa uwe na roho ngumu kama ya mwanajeshi ambaye anajua kuwa ni lazima ashinde maana asiposhinda basi atapoteza uhai wake.Kupata hasara kupo na kutaendelea kuwepo,ila unapopata hasara unachotakiwa kufanya ni kujua kwanini umepata hasara ili usirudie kilichofanya hasara.

Vile vile ujasiriamali unataka mtu uwe na nidhamu ya pesa,sio mtu biashara inakuingizia faida ya 3M kwa mwezi halafu wewe unaspend 2.5M halafu unasave 0.5M,hapo utachemsha,maana iwapo itatokea umepata hasara kubwa ikakata nusu ya mtaji,ina maana faida uliyosave haitatosha kuisimamisha tena biashara.Vile vile ukisave kiasi kikubwa ina maana una nafasi ya kupanua biashara yako baada ya muda fulani,la sivyo biashara yako itakua kwenye level ile ile miaka nenda miaka rudi.
Asante Queen, nimekupata
 
waulize wachagga watakujibu vizuri sana maana kwao mtu yyte anaweza fanya biashara na akafanikiwa vizuri,
secret behind me is to respect money unaweza fanya biashara mtu yyte
kuhusu wachaga si wote wafanyabiashara wengine wameajiriwa na wamesomea uhasibu
 
Topic yako ni nzuri sana na swala kubwa hapa ni kusubutu ndipo utaweza kufanikiwa kila wakati mwanzo ni mgumu sana kwa kila jambo unatakiwa ujilipue then utaona faida kubwa lakini ukisema sioni njia na kweli hautoiona kabisa kiufupi unatakiwa kujitoa muhanga kwa swala hili na utaona mafanikio makubwa sana. Jambo la msingi unatakiwa kuwa na mtaji na eneo la kufanyia biashara hilo ndiyo jambo la msingi sana kwa upande wangu.
 
Biashara is all about your confidence. Na confidence unajengewa kutokana na malezi ya familia yako na jamii nzima inayokuzunguka. Confidence nnayoongelea hapa ni ile hali ya mtu kutokuogopa kujielezea. Hii inamfanya mtu kuwa na urahisi katika kuielezea product yake so inakuwa rahisi kuuza. Angalia watu wote waliofanikiwa ibiashara ambao hawajaenda shule ya biashara, wote ni watu wanaojichanganya na jamii na sio watu wanaoogopa kujielezea mbele ya wenzao. Sasa kwa wale wengine ambao hawajiamini, wao wana-rely zaidi kwenye elimu ya biashara. Mtu wa namna hii akishapata elimu ile, inamsaidia kupandisha leves yake ya confidence, maana anakuwa ashahakiukishiwa kwamba akiitumia ile elimu aliyopewa atapata mafanikio. Sasa hiyo idea ya kufanikiwa kutokana na elimu yake, ndo inamfanya awe na confidence.

Sasa ni kwanini wengine wana confidence wengine hawana? Ni jinsi tunavyolelewa. Wazungu wengi wana confidence maana wanawapa watoto wao uhuru wa kujieleza na kufanya maamuzi tokea wakiwa wadogo na hawatishitishwi na kuchapwa kama watoto wa kiafrika. Mfano mmama wa kitanzania anamwita mtoto wae 'ng'ombe wewe' tokea akiwa mdogo, sasa unategemea mtoto kama huyo atakuwa na confidence gani akiwa mkubwa? Atakuwa ana doubt ideas zake maana anajiona hana thamani maana hata mzazi wake hamuoni kama ana thamani. Watu kama hawa huwa wanabakigi na ideas zao mioyoni mwao bila kuzisema, na wakati wote huwa ni ideas nzuri.

So biashara is all about confidence. Na ukibahatika kuwa na confidence na kupata elimu ya biashara, unakuwa poa kishenzi kibiashara.
 
Back
Top Bottom