Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Maarifa ni kitu cha msingi sana katika maisha ya binadamu, ili tuendeshe maisha yetu ya kila siku tunahitaji maarifa. Na kama maarifa yakituongoza katika kila kitu tunachofanya na kutenda, tutaishi maisha mazuri sana. Kwahiyo natumaini mambo mema kwenu, ya kwamba mtakuwa chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu. Na kwamba tutatafuta maarifa kadiri ya uwezo wetu ili yatuongoze katika maisha yetu ya kila siku. Kwahiyo hatutaishi maisha ya kama vipofu; bali kama ya watu wanaoona sahihi. Na ya kwamba mwanga utajaza maisha yetu badala ya giza.
Leo ningependa kuongelea kuhusu familia. Familia ni sehemu ndogo katika taifa lakini ni muhimu sana. Mtu ambaye anaharibu familia yake kwa njia yeyote ile ni mtu ambaye anaharibu nafsi yake mwenyewe na pengine ana haribu jamii.
Familia ni institution kama institution yeyote nyingine ambayo iko katika taifa. Kuendelea kwa familia yeyote ile kunategemea sana akili za watu wawili ambao wameungana kutengeneza au kuunda familia. Watu wawili wanapoungana idea ni kutengeneza familia kama institution. Kwahiyo ubora wa familia inategemea sana ubora wa watu wawili walioungana na kuunda familia.
Tunapooa lengo la kwanza na kubwa ni kutengeneza familia ambayo ni institution. Hatuoi mwanamke kama chombo cha starehe. Tunaoa ili tuzae, tutengeneze familia na kuiangalia katika ubora wa hali ya juu. Tunaoa ili tutengeneze instution na ku create order ndani ya jamii yetu. Kama tusingeoana kungekuwa hakuna order katika jamii yetu na hakuna serikali ambayo inaweza kuendeshwa pasipo familia, yaani watu wazaane tu bila ya uwepo wa familia. Kwahiyo familia ni muhimu sana kwa taifa na katika utawala wa binadamu. Ndio inayotufanya tuwe binadamu na kujitofautisha na wanyama. Mtu anayechepuka anafanya kosa kubwa sana kwa taifa kwa kujua au kutokujua kwasababu familia ikiyumba jamii na taifa halitoweza kuwa salama, kwahiyo kuvumilia watu wasio heshimu familia ni madhara kwa taifa. Maadili ya familia yakiyumba taifa haliwezi kupona. Mtu ambaye anaharibu familia anaharibu order katika jamii na katika nchi. Kuna uhusiano mkubwa kati ya familia imara na jamii imara. Tunapodharau familia hatutaweza kuunda taifa imara. Inaanza kwenye familia inafuata kwenye ujirani mwema inaendelea hadi kufika katika utaifa.
Natumaini kwamba tutapata akili na kuwa tayari kuunda taifa letu kuanzia chini. If you are devoted to your family ni rahisi kuwa devoted kwa taifa lako. Kwasababu utafikiria future ya watoto wako ambao wanaishi katika kitu kikubwa kinachoitwa taifa. Kama Taifa lisipokuwa na amani unajua familia yako itaathirika kwasababu hauishi katika kisiwa unaishi na watu wengine.
Uhusiano wa mtu na familia yake, uhusiano wa mtu na jamii pamoja na taifa lake ni muhimu sana. Ili kwanza tujenge taifa ni lazima tujenge mahusiano yetu. Hakuna raia bora kama yule anayeangali familia yake vyema kwa kuwatiisha na kuwaongoza watoto wake katika njia iliyo sahihi.
Hakuna kiongozi mzuri atakayetokea ambaye hayuko devoted kwa familia yake. Siongelei habari ya kuiba na kuwapelekea mali hii sio sahihi. Bali kuielekeza familia katika njia ambayo inapaswa kupita. Njia sahihi.
Mtu yeyote anaweza kuzaa lakini sio kila mtu ana uwezo wa kuwa baba. Unazaa ndio lakini tabia na matendo hayaonyeshi kama unapaswa kuwa baba ambaye ni mwangalizi wa familia. Mtu ambaye anapaswa kuwafundisha watoto njia ambayo wanapaswa kupita. Na kwa kuwafundisha watoto njia wanayopaswa kupita utakuwa umeisaidia serikali na jamii yako kwa ujumla kwa kuwafanya watoto wetu kuwa na tabia njema.
Tunahangaika kila siku kuhusu ufisadi lakini mambo haya lazima yaanzie chini na katika jamii yetu. Hatutakuwa na matumaini kama hatutajenga tabia za watu wetu wakawa ni wenye kuzalisha na wenye tabia njema. Kwahiyo heshima kwa familia ni kitu cha kwanza katika taifa lazima tukisisitize. Hatuwezi kuchezea familia tukasema tutaendelea na kujenga taifa imara.
Kiongozi ambaye familia yake imesambaratika hawezi kufanya chochote. Uongozi unaanza katika familia. Kwahiyo baba na mama wanaoana wanazaa watoto na kutengeneza unit. Hii small unit ndani ya kitu kikubwa kinachoitwa taifa lazima ifanye kazi vizuri. Haiwezekani mtu kutaka vitu vikubwa wakati vidogo vinamshinda. Kwanza ni lazima aonyeshe uongozi katika familia yake. Tutashangaza sana kama kwa mfano tukimpa uongozi wa serikali za mtaa mtu ambaye familia yake haiko stable. Inawezekana tu kama sisi wote familia zetu ziko katika hali mbaya. Au pengine tunachukulia ki rahisi nafasi hizi za uongozi na watu tunaowapa.
Kwahiyo kiongozi mzuri hato furahia kuona watu wake wakipeana talaka na kuachana. Kwasababu anajua fika madhara yake kama hali hiyo itaendelea katika jamii kwa kipindi kirefu. Tunapenda kuona watoto wetu wakikua katika afya njema ya kiakili na kimwili wakipata mapenzi ya pande zote mbili na muongozo kutoka kwa wazazi.
Tunapoona watoto wa mitaani kuna mambo mawili ni kielelezo kwamba kuna familia iliyosambaratika ama isiyo fanya kazi vizuri, tukitambua kwamba familia ni institution na wazazi wana wajibu wa kuwaangalia watoto, kuwalisha na kuwavisha, jambo jingine huenda kuna jamii isiyofanya kazi vyema kama kungekuwa na jamii inayofanya kazi vyema watu wangeulizwa kwanini hawawajibiki ipasavyo kwa familia. Tunapozungumza serikali inashindwa kutawala, lazima tuangalie familia zetu tunazitawala vipi na kuziongoza. Kwasababu serikali inatoka huku kwenye familia zetu. Ukweli ni kwamba tumeamua kujenga taifa la watu wabinafsi tusioangalia jamii. Mwelekeo tunaoenda nao sio sahihi. Tukiwa na viongozi wabinafsi hatutaweza kujenga jamii iliyobora.