Mtu anayejihami akimuua mtesaji wake sheria inahukumuje?

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,315
Kwa mfano polisi wanakupa visago na kwa kujitetea kumbe una kisu. Ukamchoma akafa huku Ukiwa katika jitihada za kujitetea. Je kisheria utahesabika kama muuaji au mtu aliyejihami?Au sheria itakuita shujaa? Au ni ruksa upigwe bila kujitetea?
 
Kisheria utakuwa umeua bila kukusudia. Hukumu yake ni miaka kadhaa jela(sio kifungo cha maisha na wala sio kunyongwa). Kesi yake mara nyingi inachukua muda kidogo lakini unaweza kupata dhamana.
 
hiyo itaitwa "self defence" itakuwa umeua bila kukusudia...lakin lazima kuwe na
reasonable force used...yaani nguvu
utakayo tumia kujihami isiwe kubwa kuliko ya mtu anae kudhuru.
mfano polisi akiwa anakupiga na virungu...usijihami kwa bunduki.
 
Kwa mfano polisi wanakupa visago na kwa kujitetea kumbe una kisu. Ukamchoma akafa huku Ukiwa katika jitihada za kujitetea. Je kisheria utahesabika kama muuaji au mtu aliyejihami?Au sheria itakuita shujaa? Au ni ruksa upigwe bila kujitetea?

Polisi? Aisee...labda kama kuna ushahidi kwamba hicho kosago kilikuwa cha uonevu....ila kama walikuwa wanatekeleza jukumu lao kisheria........................
 
Mathalani nimekutana na PANYA ROAD 20 wana visu bisibisi pangaz na mimi nina bastola. Wskanizingira na kuanza kunishambulia. Nikiua baadhi hapo nitahukumiwa kuua?
 
Una uwezo wa kuwatandika miguuni tu....ila ukiwapa za vichwa wakati wewe hauna hata alama moja ya kuchanwa na panga utaaminika vipi kwamba hukukusudia??
 
Kisheria utakuwa umeua bila kukusudia. Hukumu yake ni miaka kadhaa jela(sio kifungo cha maisha na wala sio kunyongwa). Kesi yake mara nyingi inachukua muda kidogo lakini unaweza kupata dhamana.

section 198 penal code
"mtu yeyote anayepatikana na kosa la kuua bila kukusudia adhabu yake ni kifungo cha maisha gerezani"
 
Na unapokuwa ndani na silaha nje kukawa na wavamizi ndani ya uzio wako sheria inasimama vipi

1. Wakiwa na silaha za jadi
2. Silaha za moto
3. Huna uhakika kama wana silaha au hawana
 
muuliza swali yafaa kujua kwamba, sheria za makosa ya jinai katika mazingira ya kujitetea, mambo yafuatayo yazingatiwe
1. nguvu unayotumia iwe sawa na nguvu inayotumika kukushambulia
2. sira aliyotumia kumshambulia adui yako iwe ni siraha ambyo hukufuata mbali bali ni silaha ambaya ulikuwa nayo mokoni
mwako
3. eneo utakalo mdhuru liwe nikuanzi kiunoni kwenda miguuni , pia muwe ni watu mnaonesha mlitazamana nasiyo umpige risasi kisogoni au eneo lolote la nyuma
4. kama ni siraha, basi siraha hiyo iwe imesajiliwa kisheria naumeilipia leseni
5.kuna kitu kinaitwa "necessity and proportionalty use of force" hii ni kanuni ambayo unapaswa kuizingatia sana.
 
Shukran
 
Hiyo ya kumpiga mtu mguuni ni ndoto na muvi zinawadanganya, law enforcement daima wanafundishwa kulenga eneo kubwa la mwili kwa hiyo kuanzia mabega hadi kiunoni, hii ni kutokana na ukweli kuwa kumpata mtu na bastola sio kazi rahisi kama kwenye movie.
 
Back
Top Bottom