Mtu anayeongoza kunuka kwa kutooga kwa muda mrefu

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,219
Reaction score
4,608
Kailash Sing ambaye hivi sasa ana umri wa
miaka 65 hajawahi kuoga wala kukata
ndevu zake tangu alipooga kwa mara
mwisho kabla ya sherehe ya harusi ya
kumuoa mkewe, mwaka 1974.
Sing anaelezea sababu ya msimamo wake
huo kuwa ni sharti la utabiri aliopewa na
mmoja wa kiongozi wa dini ya Hindu kuwa
atakapopata mtoto wa kiume, basi mtoto
huyo atakuwa mwenye mafanikio makubwa
sana kwenye maisha yake na atakuwa tajiri
sana.
Ni miaka 37 imepita lakini Sing anaendelea
na msimamo wake wa kutooga mpaka pale
atakapofanikiwa kupata mtoto wa kiume.
Sing ana jumla ya watoto saba wa kike lakini
juhudi zake zote za kupata mtoto wa kiume
bado hazijazaa matunda.
Mkewe ambaye sasa ana umri wa miaka 60,
alishawahi kujaribu kuweka mgomo wa
kutoa unyumba mpaka Sing atakapooga
lakini mgomo huo uligonga mwamba kwani
Sing hakujali chochote na matokeo yake
mgomo huo uliisha.
Majirani na watoto wamekuwa wakimtania
na kumtupia maneno ya kejeli mzee Sing
ambaye amekuwa akipuuza kila
anachoambiwa mpaka pale ndoto yake ya
kuwa na mtoto wa kiume itakapotimia.
Familia yake nayo imewahi kujaribu kutumia
maguvu kumuogesha kinguvu Sing kwenye
mto lakini Sing alifanikiwa kuwazidi nguvu
na kukimbia akisema kuwa ni heri afariki
kuliko kuvunja sharti litakalomwezesha
kupata mtoto wa kiume.
Kinachomfanya Sing awe anatoa harufu kali
ni kazi yake ya ufugaji ambayo huifanya
akizunguka kuwalisha majani ng'ombe
wake kwenye kijiji chake cha Chatav
ambapo hali ya hewa yake ni ya joto kali
wakati mwingine kufikia joto la nyuzi 47C.
Mbali ya kutooga, Sing hajazikata ndevu
zake na wala kuzinyoa nywele zake ambazo
hivi sasa zimefikia urefu wa mita 1.9.
Ili kuusafisha mwili wake, Sing huota moto
kila siku jioni huku akisali kumuomba
mungu wake wa Kihindu, Shiva.
'Wakati ninapoendesha baiskeli kwenda
kwenye shughuli zangu, watoto wamekuwa
wakitania na kunipiga kelele kuwa
siogi,hawaelewi kwanini nafanya hivi
sitabadili uamuzi wangu mpaka
nitakapopata mtoto wa kiume", alisema
Sing.
Source: News Agencies
 
Aendelee na imani yake pengine mungu wake kuna siku atamsikia.
 
mhhh kazi kwelikweli...ila sie waafrika ndio tunaoga sana wenzetu hawa usiwapimie!
 
Atapataje mtoto wa kiume wakati mkewe ana umri wa miaka 60?? Au itabidi aoe mke mwingine mdogo
 
Hata mimi nampango wa kuanza kuyakwepa maji hadi nitakapokuwa tajiri mwenye mali nyingi.
 
Nilikuwa Mfindi ndani kule, kuna baridi kali, sikugusa maji siku nne mfululizo, siku narudi Dar ilikuwa kasheshe. Tulipofika maeneo ya Ruaha, nikashanga jamaa niliyekaa naye anahama seat. Sasa huyu Mhindi kwa miaka yote hiyo,si anafaa kuwa expell ya kijiji chao !!!!. Imani sio mchezo.
 
Umewahi kuwanusa ama kukaa karibu na vijana wa UVCCM? nakuambia utatapika ulichokula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…