Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Shooter Again

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
5,603
Reaction score
9,263
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
 
Hesabu we huoni hapo million 10 na 20k Kwa siku ni mbingu na ardhi halafu biashara yenyewe bajaji
Kwani utakuwa unategemea hiyo bajaji kwa kila kitu?? Hiyo biashara ni ya kuzungusha hela hata kama faida ni sio kihvyoo.
Kuna watu wanalisha familia mbili kwa bajaji mzee, nenda kitaa ujionee!
 
Wanakuwa wamepiga mahesabu haya
Screenshot_20241209-201940.png


Kwa siku 500 wanakuwa wamerudisha hela yao. Siku 500 ni sawa na mwaka mmoja na miezi mitano hivi.

Kwa hiyo baada ya kipindi hicho kupita ndio anaanza kuhesabu faida.
 
Ni biashara ya kifala kweli, ila biashara nyingi faida yake ni ndogo pia cha msingi ni mzunguko wa fedha usiende mbali na wewe.
unaijua biashara ya hardware hii ni manyoko usipouza stock kubwa kwa mwezi mmoja tu
 
Hizo ni biashara za watu wavivu wasiotaka kuwajibika, ukiwakuta huko makazini wanavyojisifu utaskia

" Nina bajaj yangu nimempa kijana kwa week napata 140k yangu nna wasiwasi gani "

😀😀😀
 
Bora anaetoa pesa yake cash, akikomaa mwenyewe pesa yake ataiona.

Nawaona wajinga wale wa kuchukua bajaj za mkopo halafu kila siku upeleke 20,000 ya marejesho kwa miezi 36. Unakuta unainunua hiyo Bajaj hata mara 3.

Unamaliza kulipa deni na Bajaj imekufa.
 
Back
Top Bottom