Mtu asiyetaka kubadilika

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
DALILI ZA MTU ASIYETAKA KUBADILIKA

1. Akielezwa mapungufu yake ya kweli-
(a) ananuna;
(b) Kama ana wajibu wa kutekeleza jambo fulani, Anasusa ili mteseke muone umuhimu wake, muache kumkosoa (kiufupi, hii ni HUJUMA)
(c) Anatafuta sana visingizio vya kuhalalisha madhaifu au uovu wake.
(d) Anaunda timu au genge la kumtetea.
(e) Anakuwa na chuki na anayemueleza ukweli. Kwa ufupi yeye ni Mr au Miss/Mrs Never told, haambiliki. Anaamini ni mkamilifu wakati wote.

2. Mara nyingi si Msikilizaji, hana subra muda wote anahemka kutaka kumjibu anayemwambia.

3. Hana muda wa kukaa chini na kutafakari na kufanya tathmini juu ya kile alichoambiwa, ili abaini ukweli ni upi, na lipi au yepi ni ya uongo amesingiziwa.

4. Kwake yale madhaifu ameshayafanya sehemu ya utamaduni wake. Kwa hiyo haoni tatizo, anakushangaa wewe unayeona hilo ni tatizo. Kwa ufupi, You cannot win the fools in large numbers, yaani huwezi kuwashinda wajinga wakiwa wengi, wewe mwerevu utaonekana ndio mjinga.

5. Daima watu wana namna hii husingizia yale matatizo ya kawaida duniani kote, kama msamaha (excuse) ya matendo yao, kama vile kukosa pesa za kutosha, mshahara duni, kutokuwa na vifaa, nk, bila kujua kuwa kama jambo fulani ni tabia yako hata ungekuwa na hivyo vitu bado utaendelea kufanya tu.

Tafakari

USSR
 
Ahsanteee kwa ushauri

Sent from my Infinix X606D using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…