Hahahaaaaa nchumu basi kama siku ile.......
Hii whatsap naona iko popular sana dunia ya tatu. Sijui kwa nini tu.
Wengi ni watu wa magumashi,watu ambao hawasomeki,watu ambao ni fekero!!
Kwa nini?
Wala usijifunze... haina maana
Bora na mm niwe mtu huru kama wewe tu, haina haja ya kufichama mtu asikuone wakati hata wewe humuoni
Wengine usipomjibu kwa mda mwafaka na kaona last see lazima pachimbike heri kuficha tu
Naenjoy sana hizi feature ya kuficha Last seen status, profile picture na WhatsApp status, Last Seen sitaki kabisa ionwe na mtu yeyote kwanza na mimi sitaziona za watu wengine, hii inanipunguzia stress za kujibu message maana wengine usipojibu ontime hata kama alichokutumia ni nonsense inakua tatizo, picha na status hivyo nmeweka vionwe na contacts nilizosave, hivyo ukitaka kunispy kwa kuniangalia kwenye whatsapp wakati mi sina contact yako obvious utaona blank tu.
Kama hufanyi lolote baya kwa nini uone tabu kuulizwa maswali na mwenzio? Manake kama kweli hufanyi ambayo hutakiwi kufanya basi hata majibu ya maswali uulizwayo yatakuwa consistent, utayajibu kwa kujiamini, hutakuwa defensive, na hutatafuta lame excuses.
As simple as ABC or 1,2,3.....
Kama hufanyi ambayo hutakiwi kufanya sioni kwa nini uone shida kujibu maswali hata yawe ya mara kwa mara.
Na kama hufanyi lolote ambalo hutakiwi kufanya basi sioni kwa nini ulaumiwe pasi na sababu.
Kuficha ficha mambo ni dalili ya utovu wa uaminifu. Hilo hata mtoto mdogo wa miaka miwili analielewa.
Tatizo watu huwa hawataki tu kukubali kuwa sisi binadamu tuko inherently dishonest.
Unajua nafsi zina tafsiri pana sana. Kuna watu hapa jf wameshajengea id zao "nafsi" fulani... japokuwa najua hakuna mtu anamjua nje ya jf... lakini humu humu ana ka-dunia kake kenye hadi familia...
So anaweza kukosa uhuru...
Labda tuanzie nyumbani, I mean hapa hapa JF.
Kwenye Login & Privacy Settings za JF kuna kitu kinaitwa Invisible Mode ambapo unaweza ku-set Invisible Mode on na Invisible Mode off.
Invisible mode inakuwezesha kubrowse, kuanzisha threads na ku-post bila kuonekana kama uko online.
Baadhi ya members wakiwemo wewe na Husninyo wame-set invisible mode.
Kwa kufanya hivyo ni dalili za kukosa uhuru pamoja na kuwa watu hao wanatumia anonymous ID?
kwahili mkuu naona tutatofautiana tu ,,,,,,, whether nafanya yanayopaswa au sifanyi ........ to me wakati mwingine mood yangu haziniruhusu kujibu maswali ya mara kwa mara ambayo hayajengi chochote zaidi ya kukwazana.........
last seen haina kazi kwangu , kwani hata sitaki kuona last seen ya mtu mwingine kwasababu hainihusu......... na its very ok with me kumuachia mtu hewani msg blindly.
mbona mawasiliano mengine hayana last seen na tunawasiliana vizuri tu?
siyo lazima anayenighasi awe mpenzi wangu........
hata humu jf mara nyingi tumeshaona kuna watu watajifanya wanakufahamu kuanzia nje mpaka ndani ilihali huyo mtu hata pm hamjawahi kutumiana........
kukata mzizi wa fitina hebu niambie ni nini umuhimu au faida ya last seen?
Hii ya invisible mode sidhani kama inahusika na kumficha mwenza wako chochote maana ukianzisha mada au ukichangia kwenye mada mchango wako utaonekana kwa wote.