Nchi yenye watu takribani milioni 70. inategemea maamuzi ya mtu mmoja. Ambaye kakalia kiti Cha utawala. pamoja na kuwa na jopo la washauri lililosheheni wasomi wenye shahada kubwa. Lakini Saini yake kwenye makaratasi ya mikataba ya wawekezaji kutoka nchi kubwa zenye nguvu Duniani ndio inayoweza kuamua muelekeo wa nchi na maisha ya wananchi wake kwa sasa nakwa Karne zijazo. Nchi iliyojaliwa rasilimali za kutosha ikiwemo madini mfano; (dhahabu, Almasi, Tanzanite, rubi, grafiti,chuma,Nikieli, bokside,urani, kokoa n.k) Vivutio vya asili (milima, misitu, maziwa, mito n.k), Mbuga za wanyama(Ngorongoro, Serengeti,manyara n.k), Ardhi kubwa yenye rutuba inayofaa kwa kilimo Cha biashara na chakula. Nchi pamoja na rasilimali zote zilizomo ndani. Zipo kwenye mamlaka ya mtu mmoja ambaye maamuzi yake asipofikiria kwa kina yanaweza kubadilisha mchana ukawa usiku. Hakuna mtu anayeweza kumzuia kufanya chochote kwenye Nchi anayoitawala kutokana na mamlaka aliyepewa kikatiba. Na Saini yake ndo silaha kubwa anayoitumia kufanya maamuzi. akiamua alete maendeleo anasaini, akiamua auze Nchi na rasilimali zake anasaini, akiamua aue anasaini, akitaka kuwaachia huru wa fungwa anasaini kiufupi Nchi na kilakitu kilichopo kipo kwenye Saini yake. Mtu huyu ni rais.
Fikiria hii nchi inakuwa chini ya utawala wa rais mwenye tamaa, Uchu wa Mali, asiyetosheka, Asiyejali kuhusu wananchi wake, mwenye kujifikiria yeye nasio maendeleo ya nchi. Anauwezo wa kupitisha na kutia Saini mikataba ambayo Haina manufa kwenye nchi endapo ataahidiwa donge Nono na wahusika. Hata wale ambao wataonekana ni wakereketwa na wapenda maendeleo ya nchi akiona wanamletea chokochoko kwenye utawala wake yupo Radhi hata kuwanyamazisha kwa kuwapa ahadi ya malimbikizo ya Mali au kuwapa nafasi za juu kwenye serikali iliwasiingilie utawala na maamuzi yake. Au kuwanyamazisha kwa kuwaondo uhai wao ilimradi mipango yake na malengo yake yafanikiwe. kwani wewe hujawahi kusikia juu ya mtawala mmoja aliyejilimbikizia Mali, alijaza fedha kwenye benki kubwa zote za Dunia, alinunua kisiwa chake, alitengeneza mbingu yake ilihali yupo Duniani, alijenga nyumba za kifahara kila Kona ya Dunia,magari ya kifahari alibadilisha kama viatu Tena kwa kutumia jasho la wananchi masikini wanaopambana usiku na mchana kupata walau Chochote kitu. lakini mwisho wa siku alipinduliwa, Mali zikachukuliwa na akabaki mkavu.
Kuwa kiongozi au mtawala sio kwaajili yako ni kwaajili ya watu wengine ambao wanataka ufanye kwa niaba yao. Na utawala Bora niule unaoleta maendeleo chanya kwenye eneo au nchi husika. kuwa kiongozi haimaanishi uwaonee wengine au uwatumikishe wengine Bila kujali ubinadamu wao. kuwa kiongozi au mtawala inamaanisha kubeba jukumu lakusimamia maono na malengo ambayo yanatarajiwa kufikiwa kwa muda flani na jamii au nchi husika. Na utawala au uongozi Bora ndo nguzo ya kuwezesha mafanikio chanya kwenye jamii. uongozi unaanza na mtu mmoja mmoja. Ukiweza kujisimamia na kutimiza majukumu yako Bila kusimamiwa na mtu basi wewe ni kiongozi. kila mmoja wetu akiwa kiongozi na mtawala mzuri wa maisha yake basi kunauwezekano Mkubwa wakupata viongozi Bora wanatakaoweza kuongoza familia, ukoo, Kijiji, kataa,tarafa,wilaya, mkoa nahata kufikia ngazi ya juu kabisa kuongoza nchi. uongozi na utawala bora unaanza na Mimi.

Upvote
3