Mtu mrefu zaidi duniani aliishi Handeni, Tanga

Mtu mrefu zaidi duniani aliishi Handeni, Tanga

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
KWA Mujibu wa Wikipedia, Robert Pershing Wadlow, aliyeishi kati ya Februari 22, 1918 na Julai 15, 1940, pia alijulikana kama Jitu la Alton na jitu kubwa la Illinois, alikuwa ndiye mtu mrefu aliyewahi kuingizwa katika kumbukumbu za kitabu cha Guiness, Duniani.
Urefu wa Wadlow ulifika futi nane na inchi 11.1 au sentimita 2.72 na alikuwa na uzito wa pauni 439 au kilo199 wakati wa kifo chake akiwa na umri wa miaka 22.
c861439c5f97889839ff0ff79ac99bf2.jpg

Kisayansi umbile lake kubwa liliendelea na ukuaji usio wa wa kawaida hadi wakati wa utu uzima kutokana na kuongezeka kwa seli katika kiungo kiitwacho pituitary gland, kinachosababisha kuwepo kiasi kikubwa cha homoni za ukuaji. Aliendelea kukua hadi wakati wa kifo chake
Mtu huyo alikuwa na urefu wa futi tatu alipokuwa mtoto mdogo tu. Na aliweza kumbeba baba yake alipokuwa na umri wa miaka tisa. Mikono ya Wadlow iliweza kufikia urefu wa futi tisa na inchi tano ikipanuliwa na viganja vyake vilivyokuwa na ukubwa wa futi moja.
Wadlow's alipofariki, jeneza lake lilikuwa na uzito wa pauni 1,000 na lilihitaji wabebaji 18 walilibeba na kulifikisha katika a mapumziko yake ya mwisho Alton, Illinois.
Familia ya Wadlow iliamua kuharibu vitu vyake kwa hofu kuwa vinaweza kukusanywa na kuonyeshwa kwenye maonyesho ya vitu vya ajabu vya kumbukumbu
Wakati kumbukumbu hizo zimetunzwa rasmi, taarifa hizo zinaweza kuwavutia watalaamu wa kumbukumbu za kihistoria za matukio ya kipekee yanayowatokea watu na kuvunja rekodi kuwa sio ya kawaida.
Inasemwa kuwa, utafiti uliofanyika kwa miaka 16 huko Handeni mkoani Tanga, unaonyesha kuwa, Tanzania inaweza kuwa na historia ya kuwa na mtu anayedhaniwa kuwa mrefu zaidi duniani.
Tafiti isiyo rasmi inadai kuwa mtu huyo alikuwa na urefu wa futi 35 na kubainisha yaweza kuwa ni maajabu yanayohitaji kuvutia watafiti mbalimbali ili kujiridhisha na matokeo ya utafiti huo wa awali usio rasmi
Ni katika kijiji cha Ngwujini, wilayani Handeni mtafiti mmoja wa mambo ya kale na ya asili aitwaye, Ramadhani Ayubu amegundua kitu cha ajabu kwamba katika eneo hilo aliwahi kuishi mtu ambaye ana urefu usio wa kawaida .
Mtafiti huyo amegundua kaburi la mtu mmoja wa ajabu aliyejulikana kwa jina la Mbulushi Malilo.
Katika utafiti huo, lilipimwa kaburi la mtu huyo lililofikia futi 35 ambaye inaashiria kwamba hakuwa mtu wa kawaida aliyeishi katika karne ya 16 inayesemekana kwamba alikuwa na nguvu za ajabu.
Kwa mujibu wa matokeo ya Mtafiti Ayubu ni kwamba katika uhai wake, mtu huyo inasemekana aliwahi kuchimba bwawa ambalo hadi sasa linatumiwa na wenyeji wa eneo hilo.
Taarifa nyingine zinabaninisha kuwa mtu huyo, alikuwa na sauti kubwa ambayo hata akiita mtu aliweza kuisikia hata akiwa umbali wa kilomita moja.
Mtafiti Ayubu, anayemiliki kampuni iitwayo Regulate Body Temperature Cilini yenye makao yake Amana, jijini Dar es Salaam, mtu huyo inadaiwa kwamba alikuwa mtaalamu wa masuala ya kivita na alitumika hata katika vita ambavyo watu mashuhuri enzi zile za ukoloni OleTiptip na Bushiri walipigana dhidi ya watawala wa enzi hizo.
Ayubu, anayedai kwamba alisoma masomo ya sayansi nchini Ethiopia na akalazimika kuacha kutokana na mgogoro wa mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea alidai kuwa, kabla hajafa aliacha wosia kuwa akifa lazima azikwe Ngugwini.
Akizungumzia kuhusu namna alivyofahamu simulizi za mtu huyo, mtafiti huyo alisema kuwa alipata taarifa za mtu huyo kutoka kwa watu wa familia ya Mbulushi aliokutana nao Same, mkoani Kilimanjaro. Alifahamishwa kuwa katika kaburi lake alizikwa akiwa na mkuki wake.
“Simulizi hizo zilinivutia kwenda huko Ngwujini. Hata hivyo nilipata taabu sana kupata ushirikiano wa karibu na wenyeji. Wenyeji walikuwa wanaona ajabu sana mimi kufuatilia kaburi ambalo wao walikuwa wanaliona kama kaburi la kawaida sana,” alisema Ayubu kwamba imemchukua miaka 16 kuwashawishi wanakijiji hao hadi kukubali kuwa ni kaburi ni la mtu wa ajabu sana.
Alisema kuwa, vijana, wazee na wanawake baada ya ugunduzi huo walikuwa hawaamini kile walichokisikia na hivyo wanauliza “kwa nini kaburi hilo, kama ni la mtu wa ajabu halijulikani?”
Kama hiyo haitoshi, watu hao wanadai kuwa hawaoni kuwa kuna faida yoyote kuwepo kwa kaburi hilo.
Eneo lenye kaburi hilo, wenyeji wanalichukulia kuwa kama eneo la mizimu na matambiko. Kuna mti mkubwa aina ya mkuyu ambao inaaminika kuwa hata ukikatwa utaendelea kusimama kama ulivyo.
Kutokana na hali hiyo, eneo hilo wanakijiji wameamua kulihifadhi licha ya kwamba linakabiliwa na tishio la kukatwa kwa miti inayozunguka eneo hilo.
Kwa mujibu wa mtu mmoja aitwaye Omari Athumani, almaarufu kwa jina la Mganga ambaye ni wa kizazi cha Mbulushi wanaotunza kaburi hilo, hapo mwanzoni kulikuwa na msitu mkubwa.“Miti ilikuwa inavuma sana lakini sasa hakuna miti.
Msitu umekatwa.Mtu huyo alikuwa na uwezo wa kutembea zaidi ya kilometa 500 kwa muda mfupi tu na alikuwa na nguvu za ajabu.
Aliendelea kusema kuwa, historia na utamaduni sasa hivi vimepotea na kubainisha kwamba alikuwepo nyani ambaye akipita tu mvua inanyesha, lakini sasa amepotea kutokana na msitu kukatwa na mazingira kuharibika.
Mganga pia alieleza kuwa, kwenye bwawa linalodaiwa kuchimbwa na Mbulushi peke yake kuna mamba ambaye hatoki hadi aitwe kwa jina.
Naye Sudi Mohamed Mgweno akifafanua zaidi kuhusu mti unaoaminika kuwa ukikatwa unaendelea kusimama, alisema mwaka mmoja watu kutoka Kenya walikwenda kukata miti kwa ajili ya mbao na kuukata mti huo.
Amesema kilichowasukuma kuukata mti huo ni kwamba ulikuwa unavutia kutokana na ukubwa wake. “Mti huo ulikatwa na kusimama tena,”alisema.
Nao vijana mmoja Swedi Ramadhani na Juma Said walisema wanaamini kuwepo kaburi hilo, kunaweza kusababisha fursa za maendeleo ambazo hazikuwepo hapo awali pamoja na kuwepo kwa raslimali hiyo ya watu wa kale.
 
Duh hata kama ni kupenda vya kwetu lakini huu utafiti hapana aiseeh..

Kama ndugu mtafiti alifanikiwa kulipata kaburi lililodumu kwa centuries takriban 4 kwanini asichukue mifupa akaipima urefu na tatizo likaisha..

Halafu ni ngumu kumeza eti kaburi la toka karne ya 16 kuendelea kuwepo mpaka leo..
 
Utafiti wa mtafiti wa kitanzania aliyetumia miaka 16 kuwashawishi watanzania wenzake kukubali kuwa ni kaburi la karne ya 16 maajabu haya. Yaani hii tafiti angefanyia nje ya TZ angetumia miaka 50. Halafu karne ya 16 ni mika 1500+ sasa Tiptip ni wa mwaka gani wale wanahistoria mko wapi msaidie hii mambo?
 
hahaha nacheka kama mazuri hilo lilikuwa jitu sio mtu. sipati picha angekuepo mpaka sasa.

enzi za Nuhu watu walikuwa wakubwa sana toothpick ilikuwa ni nguzo ya umeme kwa sasa
Yaani umenifanya niache Kazi yangu nianze kucheka. Hiyo Toothpick!!!
 
Back
Top Bottom