Mtu mwenye cheti cha Medical labaratory science anaweza kufungua Health laboratory center

Mtu mwenye cheti cha Medical labaratory science anaweza kufungua Health laboratory center

Tommy 911

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2019
Posts
600
Reaction score
510
Habarini wakuu.

Hivi mtu mwenye basic technician certificate in medical laboratory science anaweza kufungua maabara na akaoperate? Je taratibu zake zipoje

Msaada wa maoni na experience yenu..
 
Ili ufungue maambara unatakiwa uwe na
1. Angalau diploma ya maabara.
Au
2. Kama huna diploma uajiri mwenye diploma ya maabara
Au
3. Kama utashindwa kuajiri utumie cheti cha mwenye diploma kama msimamizi na mmiliki wa maabara hiyo.
4. Pia unatakiwa uajiri ambaye atafanya kazi kila siku, huyu anatakiwa awe na usajili kutoka baraza la maabara kwa ngazi ya cheti.
5. Maabara inatakiwa iwe na vyumba v3, mapokezi, sehemu ya kuchukulia vipimo/sample(philobotomy) na sehemu ya kufanyia vipimo(lab)
6. Nenda wilayani ili waje wakague
7. Uwe na vifaa muhimu vyote kama darubini,friji, nk nk

ONYO.
hutakiwi kutibu kwenye maabara, maabara kazi yake ni kuchukua vipimo tu, hata dawa hutakiwi kuandika
 
Back
Top Bottom