Mtu mwenye ulemavu (Albino) akutwa amefariki ndani, mlango ukiwa umefungwa kwa kufuli

Mtu mwenye ulemavu (Albino) akutwa amefariki ndani, mlango ukiwa umefungwa kwa kufuli

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wande Mbiti (38), mkazi wa Kitongoji cha Busalala, Kijiji cha Nhelegani, Kata ya Kizumbi, mkoani Shinyanga, mwenye ulemavu wa ngozi (albino), amekutwa amefariki dunia ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi huku mlango wa nyumba hiyo ukiwa umefungwa kwa kufuli kwa nje.

Tukio hilo limebainika jana, Jumapili, Machi 2, 2025, saa saba mchana baada ya wakazi wa eneo hilo kusikia harufu kutoka katika nyumba hiyo na kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji, Kulwa Sheka.

Sheka amesema alipigiwa simu na kuambiwa kuwa kuna kitu kinatoa harufu katika nyumba hiyo. Alipofika, alitoa taarifa kwa polisi wa kata, ambao walibomoa dirisha na ndipo walipouona mwili wa marehemu.

Amesema baadaye walibomoa mlango.

Kwa upande wake, Mbiti Kulwa, baba mzazi wa marehemu Wande, amesema aliondoka hapo nyumbani kipindi cha utawala wa Mkapa (marehemu Rais Benjamin Mkapa) baada ya kutengana na mama wa marehemu na kueleza namna alivyopokea taarifa hizo.

Aidha mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, amefika eneo la tukio kutoa pole kwa wafiwa huku akisema kuwa serikali, kwa kushirikiana na Kanisa Katoliki, itahakikisha mtoto wa marehemu, anayefahamika kwa jina la Evelyn na ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Montessori, anaendelea kupata elimu bila changamoto.

 

Attachments

  • 1741004598509.png
    1741004598509.png
    280.2 KB · Views: 1
Pole sana
Sasa police waingie kazini wapeleleze kesi
Haiwezekani mtu afu ndani na mlango Kwa nje uwe na kufuli
Ni uhakika kuwa aliuliwa
 
Back
Top Bottom