marandu2010
JF-Expert Member
- Aug 7, 2010
- 1,201
- 446
Kwanza mwamini huyo mfanyakazi wako. Ni muhimu kuifanya hiyo biashara wewe mwenyewe kukuwezesha kujua trend ya mauzo mkiwa pamoja na huyo mfanyakazi, tufanye mwezi mmoja. Fanya projection ya mauzo unayotegemea kuyafanya kila mwezi kwa miezi 6. Mpatie hayo matarajio ya mauzo huyo mfanyakazi. Kama kutakua na tatizo ya mauzo kwenye kila mwezi baada ya miezi sita unaweza tafuta muda tena wa kukaa pamoja na mfanyakazi wako uone biashara inaendaje... Ni muhimu sana kumoonyesha mfanyakazi wako kwamba unamuamini na yeye aamini hivyo hivyo. Kama anapata cha juu nje ya projection zako hayo ni maruppurupu yake na yatamfanya apende zaidi kazi yake. Kila la kheri mkuu!habari wakuu,
naomba mnisaidie mawazo ya jinsi ya kuifanya biashara ya duka la vitu mbalimbali kwa kumwajiri mtu mwingine bila yeye kukuibia,,ni swali ambalo mimi linaniumiza kichwa,,maana wengine huweka vitu vyao na kuviuza wakikwambia biashara ngumu.
naomba mtu mwenye uzoefu wa kuanya biashara hii kwa kumwajiri mtu mwingine anisaidie jinsi anavyofanya,,ikumbukwe mimi niko mbali na nimebanwa na shughuri nyingine na siwezi kuwa natembelea kule mara kwa mara.pia nimeamua kuifanya biashara hii kutokana na vile ujazo wa mfuko wangu kuwa ni mdogo.
natanguliza shukrani zangu kwa wakuu watakaonisaidia katika hili.