Mtuhumiwa wa nchi moja anaweza kuhukumiwa na nchi nyingine

Mtuhumiwa wa nchi moja anaweza kuhukumiwa na nchi nyingine

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
0001-15444239893_20210112_175512_0000.png


Sheria za Kimataifa zinaruhusu mtuhumiwa na Raia wa Nchi moja kwenda kuhukumiwa Nchi nyingine tofauti na Nchi yake.

Ili Mtuhumiwa aweze kuhamishwa kwenda kuhukumiwa Nchi nyingine ni Lazima kuwepo na Vitu vifuatavyo:-

1. Mkataba wa Kimataifa wa uhamishaji wa Watuhumiwa(Extradiction Treaty)

2. Ombi Maalum la kuhamisha mtuhumiwa. Nchi inayotaka kumchukua mtuhumiwa wa Nchi nyingine kwenda kumhukumu kwake inatakiwa itume ombi maalum kwa Nchi inayomshikilia mtuhumiwa huyo.

3. Kosa la mtuhumiwa lazima liwe Kosa pia kwenye nchi inayotaka kumuhukumu(Double criminality)

4. Nchi inayotaka kumuhukumu mtuhumiwa lazima ithibitishe kwenye mahakama za Nchi ambayo Mtuhumiwa yupo kwamba mtuhumiwa ana kesi ya kujibu.

5. Kosa la mtuhumiwa halitakiwi kuwa Kosa la Kisiasa.
 
Upvote 1
El Chapo alifanya uhalifu Mexico akaja kuhukumiwa Marekani!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom