Mawazo tafadhali: Mimi ni mtumishi wa Halmashauri X, nasumbuliwa na mguu (lymphedema-right leg) kwa kipindi kirefu, hivyo cellulitis imekuwa ikinirudia mara kwa mara.
Nikatoka mkoani nikaingia DSM ili kujichanganya, lakini cha kushangaza hali ya mguu ilikuwa shwari kidogo, sioni kama ilivyokuwa mkoani. Baada ya kufika mjini, nilikuwa natimiza mpaka miezi 6 bila kwenda hospitali. Miaka ikazidi kusonga nikiwa Dar, nikabahatika kupata ajira mkoa wa Mtwara. Baada ya miezi kadhaa, mguu ukaanza kusumbua.
Nimeenda kutibiwa sehemu mbalimbali mkoani Mtwara, lakini nafuu ilikuwa inadumu kwa muda. Ndipo nikawa nafunga safari kwenda kutibiwa Muhimbili. Nimefanya hivyo mara kadhaa, ndio madaktari waliponiandalia medical report na confirmation letter, ikinitaka nisogee karibu na mazingira ya DSM kwa ufuatiliaji zaidi ili kutafuta favourable environment.
Nikaandika barua kupitia kwa Mkuu wangu wa Idara kwenda kwa DED, nikiambatanisha zile report na document nyingine nikampelekea ili anisaidie kuniombea uhamisho wa dharura kutokana na tatizo la kiafya.
Majibu kutoka kwa Mkurugenzi yalirudi kwamba niombe kupitia mfumo. Na kwenye mfumo nilikuwa sijatimiza vigezo vya miaka 3, hivyo nikamfuata Mkurugenzi anisaidie kibinadamu. Ndipo akanambia niandike barua kwenda kwa Katibu Mkuu TAMISEMI kupitia kwake.
Kwa hiyo, baada ya kuandika hiyo barua, DED akapitisha na ikatumwa na Halmashauri kupitia posta kwa njia ya EMS.
Toka tarehe 1 mwezi wa 6 mpaka mwezi wa 9 tarehe 1, nikaona kimya bila majibu. Nikaona niende TAMISEMI kufuatilia.
Nilifika TAMISEMI mapokezi nikaambiwa niingie Room namba 48. Niliwakuta wanawake wawili na mwanaume mmoja. Mapokezi yao baada ya kujieleza yalianza vibaya sana na kunikatisha tamaa.
Baada ya kuanza kujieleza kwa mmoja wa wale wadada wawili, yule mwanaume akaingilia ile case kwa asilimia yote iliyobakia. Kwa kifupi, inaonesha kama ndio alikuwa senior kwao.
Alidai kama barua imetoka Halmashauri ikatumwa moja kwa moja TAMISEMI, hiyo haiwezi kushughulikiwa, ndio maana naona kimya mpaka sasa. Kwa hiyo, Mkurugenzi alitakiwa akupitishie barua yako kwa RAS, ndipo ije TAMISEMI.
Pia akasema hata kama Mkurugenzi ataipitisha kwa RAS, pia wao kama TAMISEMI wataniangalia tena mimi kama nina muda gani kazini ili niombe moja kwa moja kwenye mfumo. Wakiona nimebakisha miezi michache kutimiza miaka 3, hawawezi kuhangaika na ombi langu, badala yake watasubiri hiyo miezi ya kutimiza miaka 3 ikamilike, kisha wataniambia niombe kwenye mfumo.
Na baada ya kunieleza hayo, mmoja wa wale wanawake akaniambia niende Masijala kutazama barua yangu iliyotumwa kama imefika.
Nilipoenda Masijala, wakatazama kwenye mfumo wakaikuta na wakanipa kimemo niende kwa HRO1. Na huyo HRO1 ndio yule aliyenipokea mwanzo na kuniambia masuala ya barua kupita kwa RAS.
Kwa hiyo nilipompa kile kimemo, akachukua majina yangu na Halmashauri ninakotokea pamoja na viambata nilivyovibeba. Kisha akaniambia anashughulikia.
But now ni mwezi umekata, ila naona kimya.
Kinachonishangaza, yule HRO1 alinipokea vibaya sana na kunikatisha tamaa. Hakutaka hata kuniangalia shida yangu palepale physically, licha ya kuona picha ya mguu kwenye viambata.