Mtumishi huyu afanyeje ili asidhulumiwe haki yake?

Mtumishi huyu afanyeje ili asidhulumiwe haki yake?

vamda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
895
Reaction score
571
Ndugu wana JF. Endapo mtumishi wa umma (mwalimu) amepata barua ya kuhama kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine na alikuwa na madai ya mapunjo ya mishahara ya miaka kadhaa. Alishaprocess madai yake kwa kujaza fomu za ngao lakini wakati anafunga taarifa zake za kiutumishi (DATA SHEET) kwenye faili lake ikagundulika barua yake ya madai ya mapunjo ya mishahara pamoja na nakala za fomu za ngao havionekani afanyeje ili asipoteze haki zake za malipo kabla hajahamia kwa mwajiri mwingine? Kwa nini barua ya madai na nakala za fomu za ngao vimenyofolewa? Je hapo hakuna dalili ya kudhulumiwa? Unahitajika msaada wa mawazo kutoka kwenu wataalamu wa sheria. Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom