DOKEZO Mtumishi huyu idara ya Ardhi Halmashauri ya Jiji Ilala anapaswa kuwajibishwa kwa vitendo anavyofanya

DOKEZO Mtumishi huyu idara ya Ardhi Halmashauri ya Jiji Ilala anapaswa kuwajibishwa kwa vitendo anavyofanya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na kero Halimashauri ya jiji la Ilala kitengo cha Ardhi kinachosababiswa na huyu mtumishi mmoja

Huyu mtu amekuwa akitumika kwa maksudi kuminya haki za Wananchi kupata Hatimiliki.

Amekuwa akishirikiana na maeneo ya upimaji ambayo baadhi yake yanamilikiwa na walimu wake waliomfundisha huko Chuoni.

Baadhi ya kampuni anazokingia kifua ni KMM. Ambalo lilikusanya ukusanyaji wa pesa za wananchi nakutokomea nazo bila kazi kufanywa.

Wananchi wanapohoji kampuni husika linasema kazi ipo kwa huyo mtumishi. Ukimfuata atakuambia sababu zisizo za msingi.

Ni miaka sasa kila wananchi hawajapata stahiki zao.
Ukifika Halimashauri watakuambia muone huyo mtumishi.
Ukiongea naye atakuambia kazi imeenda wizarani.

Ukifika Wizarani utapewa jibu la kuwa vibali bado havijaruhusiwa na huyo mpima wa Halimashauri ambaye alikwambia kazi ipo wizarani.

Kama wananchi tumechoswa sana na huyu mtu ambaye ukifika kwake hakuna msaada wowote.

Wizara ya Ardhi tunaomba muangalie hili, ni miaka mitano sasa wananchi wanateseka.
 
Sekta ya Ardhi ni jibu kubwa sana, kuna miungu watu huko.
 
Fanyeni kitu,mshikisheni adabu

Ova
 
Back
Top Bottom