Mtumishi Serikalini kushiriki mashindano ya ku-rap ni sawa?

Mtumishi Serikalini kushiriki mashindano ya ku-rap ni sawa?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
1666895236234.png

Nina rafiki ambae ni mtumishi wa umma katika shirika mojawapo kubwa tu, hivi sasa kuna mashindano ya freestyle ya kurap yanaendelea na yeye ni mshiriki.

Kuhusu kipaji anacho cha kuchana mistari na anavutia hadhara pale anaposhika kipaza akianza kurap , ubaya ni kwamba kwenye hizi freestyle kuna muda unamshambulia mpinzani wako kwa lugha za maudhi na kebehi.

Je, hii haiwezi kumpa taabu muajiri wake akijua ?
 
Hapana tena a-rap kuhusu Tozo,Ukosefu wa maji,Umeme na Mfumuko wa bei za vyakula na Bando pia asimsifie Mama aseme huku mtaani tunamlaani.
 
Ni sawa kabisa
Wapo wengi sana na yeye hato kuwa wa mwisho

Wapo walianza na wana endelea
Bonta
Niki
Fa
Ay

Wengine mtaongezea...
 
Kwani sheria inasemaje, mbona kwenye michezo wapo, marehemu Komba alikua anaimba.
Hata hivyo, Nakumbuka zamani kulikua na Band za mziki zilikua chini ya Taasisi za serikali, na waimbaji wake pia walikua watumishi wa serikali.
 
Ni sawa kabisa
Wapo wengi sana na yeye hato kuwa wa mwisho

Wapo walianza na wana endelea
Bonta
Niki
Fa
Ay

Wengine mtaongezea...
Hao wengi waliacha walipolamba vyeo, Pia kuna utofauti mkubwa sana wa hizi freestyle battle, hizi battle ni kushambuliana sana kwahio kuna muda inabidi umdhihaki mpinzani wako kwamba yeye si lolote kwa kumshambulia na mistari ya kumshusha hadhi
 
Kwani sheria inasemaje, mbona kwenye michezo wapo, marehemu Komba alikua anaimba.
Hata hivyo, Nakumbuka zamani kulikua na Band za mziki zilikua chini ya Taasisi za serikali, na waimbaji wake pia walikua watumishi wa serikali.
kuna kuimba kimaadili na kurap, hii ya pili ikiwa nifreestyle kutupiwa dongo ama tusi kawaida sana
 
Marejesho kikoba utamrejeshea? Kaz za ziada hizo ndo mpango
 
kuna kuimba kimaadili na kurap, hii ya pili ikiwa nifreestyle kutupiwa dongo ama tusi kawaida sana
Aise mimi hata nafuatiliaga rap, mi najua wanaimba tu, kumbe wanaimba matusi pia.
Haya acha niendelee kusikiliza, nyimbo za Dar jazz, Oss, Juwata , Sikinde urafiki, vijana, Maques, Mk group, Mk beets, Turncut, matimila Ochestra makasy, bicco star, bila kuwasahau Washirika Tanzania stas, kila juma pili pale 92 hotel Shekilango na MCA international 92 shekilango, Bima lee, kila juma pili Ufi Club Ubungo, pale jirani na 92 yaani Legho hetel unakutana band mpya ya Legho, ikiongozwa na Tshimanga Asosa, ukionda sinza juma pili, pale Lion hotel unamkuta mzee, Shem Kalenga, na band yake Mk beets, na mtindo wao wa tukunyema wo,wo,wo.

Ukija pale kijiweni sinza siku za kawaida, pale kwenye kahawa, unamkuta Fredy Mwarasha amekikamata kijiwe ni story tu, Pembeni mwake yupo, Muhina Panduka, Dah samahani nimewakumbusha tu uzamani.
 
kuna kuimba kimaadili na kurap, hii ya pili ikiwa nifreestyle kutupiwa dongo ama tusi kawaida sana

Kama unazungumzia mziki wa kutukanana au kudhalilishana ni kosa la jinai, sio mtumishi wa umma tu, hata ambaye si mtumishi haruhusiwi, na akifanya atachukuliwa hatua kali.

Mkuu, huko kwenye mashindano nashauri uandae mistari sio lazima yenye ujumbe sana maana watu hawana muda na ujumbe sana, ila andaa Vitu vya utani, kufikirisha au kuchekesha dhidi ya mpinzani wako, na sio kujipanga kwa matusi na udhalilishaji.
 
Hakuna tatizo as long as huna mawazo mgando, nidhamu ya uwoga, kutojitambua na kuwa mlamba miguu !!
 
Back
Top Bottom