kuna kuimba kimaadili na kurap, hii ya pili ikiwa nifreestyle kutupiwa dongo ama tusi kawaida sana
Aise mimi hata nafuatiliaga rap, mi najua wanaimba tu, kumbe wanaimba matusi pia.
Haya acha niendelee kusikiliza, nyimbo za Dar jazz, Oss, Juwata , Sikinde urafiki, vijana, Maques, Mk group, Mk beets, Turncut, matimila Ochestra makasy, bicco star, bila kuwasahau Washirika Tanzania stas, kila juma pili pale 92 hotel Shekilango na MCA international 92 shekilango, Bima lee, kila juma pili Ufi Club Ubungo, pale jirani na 92 yaani Legho hetel unakutana band mpya ya Legho, ikiongozwa na Tshimanga Asosa, ukionda sinza juma pili, pale Lion hotel unamkuta mzee, Shem Kalenga, na band yake Mk beets, na mtindo wao wa tukunyema wo,wo,wo.
Ukija pale kijiweni sinza siku za kawaida, pale kwenye kahawa, unamkuta Fredy Mwarasha amekikamata kijiwe ni story tu, Pembeni mwake yupo, Muhina Panduka, Dah samahani nimewakumbusha tu uzamani.