Musoma Yetu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2016
- 2,633
- 2,297
Ukiachia udhaifu mwingine wa watendaji wetu, watumishi pia tunachangia ktk matatizo tunayoyapata. Hivi unawezaje kwenda masomoni bila barua/document ya kukuruhusu? Ikiwa mtu unafahamu udhaifu wa baadhi ya watendaji wetu, iweje usipate muda wa kufuatilia mpaka upate barua? Hata shetani wakati mwingine huwa anatushangaa.
Tatizo ni kwamba rushwa ya ngono imetawala sana mtu yupo masomani miaka yote hamalizi lakini mshahara anapata hii manispaa ya kinondoni io sana hasa hawa maafisa utumishi ninoma sana inakera wengine wanafanya kazi wengine wapo masomoni hawamalizi miaka inaenda tuMkuu umenena Si ajabu hata barua hizo kafoji, utaendaje masomoni bila mkataba kusainiwa? Unashindwaje Kufuatilia ili uondoke kialali? Atakuwa Na matatizo au alionga mkuu wake wa shule ili aende kimya kimya sasa kimenuka
kwakuwa salary slips bado zinakuja maana yake ni kwamba mshahara haujasimamishwa na kwamba wewe bado ni mtumishi halali. dai mishahara yako yote ! kama mkurugenzi ni mzembe shauri yake.Ni kwamba, barua ya kuniambia jaza mkataba ilitolewa na ofisi ya mkurugenzi, afisa utumishi akaisaini kwa niaba..!!! Yeye hataki tena kufanya kazi serikalini, ila anataka kujua hatma ya hiyo mishahara yake. In turn, ukumbuke hajafukuzwa kazi..
Ajira ni suala la kisheria hivyo kila kinachofanywa huwa kinakuwa na utaratibu ambao unaweza kuhojiwa kisheria. Kusoma ni haki ya mtumishi kama ana sifa zinazomruhusu kutumia haki yake hiyo lakini kama nilivyosema awali lazima taratibu zifuatwe. Cha msingi ni kuwa na nyaraka zote zihusianazo na suala hilo, mfano barua ya kuomba ruhusa na majibu yake kama yapo, mkataba uliojazwa na huyo mtu kama ana nakala yake...Pili kumbukeni hakuna mtu mpuuz wa kuamua kwenda masomoni pasipo barua ya ruhusa. Ina maana kafatilia akachoka, kila hatua vigingi na sababu Kibao? Kila boss analeta mbwembwe kuhusu kuruhusiwa. Mwingine utasikia anasema, kwenye vikao vya Shule huwa una maswali mengi ya kuhoji hoji, sasa hapa utatujua si nani? Halafu mtu unasema ufuatilie ruhusa, kwa model gani sasa? Mtueleze
Barua hata ikisainiwa na ofisa elimu kama mkurugenzi haja ipitisha ni kazi bure kwa sababu mkurugenzi mdio mwajiri wako na ndio bosi wako namba moja. Hivyo kama ulienda ni dhahiri ulikiuka taratibuMtumishi ameomba ruhusa, na mkuu wa idara kapitisha, ila mkurugenzi hakupitisha. Nikaamua kwenda kupiga kitabu. Ghafla nikaandikiwa barua ya utoro kazini na nikajieleza. Ni kapewa ovyo, na ofisi ya mkurugenzi ikanipa barua ya kwamba jaza mkataba wa ruhusa ya kwenda masomoni rasmi. Nikajaza, ghafla mkurugenzi tena hakusaini mkataba wakati mwanasheria na boss wangu tayari wamesaini. Mara nikakatiwa mshahara, miaka miwili ila salary slip zinakuja kila mwezi. Sina barua ya kufukuzwa kazi, je?? Nina haki ya kulipwa pesa yangu yote ya mshahara tangu nilipokuwa nasoma hadi sasa? Au sistahili.