Mtumishi wa Halmashauri wilaya ya Hanang atupwa Jela miaka ishirini kwa ubadhirifu

Mtumishi wa Halmashauri wilaya ya Hanang atupwa Jela miaka ishirini kwa ubadhirifu

John Walter

Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
68
Reaction score
63
Mahakama ya Wilaya ya Hanang imemhukumu aliyekuwa Mkusanya Mapato kwa kutumia mashine ya POS wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Bw. PETRO MICHAEL MURAY.

Mshitakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la ubadhirifu kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya Bw. Petro Michael Muray katika shauri la Uhujumu Uchumi Na.03/2023, imetolewa na Mhe. Anorld Kileo - Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hanang - Aprili 19, 2024.

Mshtakiwa ameamriwa kwenda jela miaka 20 na ametakiwa kurejesha kiasi cha shilingi 3,532,000/= .

Mshitakiwa alifanya ubadhirifu wa fedha hizo kupitia makusanyo ya fedha kwa njia ya POS ambapo alikua akikusanya fedha zilizotokana na vyanzo vya misitu Wilaya ya Hanang.

Mshitakiwa amepelekwa magereza kutumikia kifungo chake.
 
3mil. 20yrs? Yale yale ya mama na nyama ya porini.

Na kuna watu walichukulia hela kwenye magunia ila bado tupo nao mitaani.

Hapo ndo mahakama zetu zinatia shaka utendaji wake.

Hata umuhimu wa CAG siuoni
 
Huyo hakula na wenzake ndio maana
Eti 3.5
Sasa kama kuna haki hao wanaoiba billions si watauwawa kabisa
 
Miaka ishirini kwa kuiba 3.5M halafu kuna watu wanaiba trillions of money wanalindwa kwa kodi zetu.
Funzo: ukitaka kuiba iba nyingi.

Hapo huwa nashindwa kuelewa hzo hukumu zao huwa zipoje
 
Dunia ni utapeli yaani miaka 20 ni parefu ,kuna wana wanachimbia mabillion ila wanadunda tu...


Bora wamuachie huyu jamaa.
 
Wanaonea wanyonge wakubwa wanadunda tu 3.5 aiseee, what about trillions
 
Back
Top Bottom