Mtumishi wa Mungu, Bagonza kahamasisha maandamano ni dhambi kama dhambi nyingine

Mtumishi wa Mungu, Bagonza kahamasisha maandamano ni dhambi kama dhambi nyingine

Ringo Malisa

Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
25
Reaction score
13
BK.jpg

Baba Askofu Rev. Dr. Benson Bagonza (PhD) Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, katika makala yako umezungumzia namna ambavyo mtu anamfanyia mtu mwingine jambo na kisha kutangaza adharani kuwa amemfanyia kitu fulani. Bila shaka uliilenga serikali ya awamu ya tano kwa kutangaza maendeleo iliyowaletea Watanzania.​

Kama tunavyofahamu kuwa serikali inaundwa na wanasiasa hivyo upatikanaji wa hao wanasiasa ni kupitia Uchaguzi ama Uteuzi. Mwanasiasa anapokwenda kwa wananchi anawaeleza nini atawafanyia ili kujenga ushawishi waweze kumchagua vivyo hivyo kwa wale wanaoteuliwa yule anayewateua ana maelekezo yake kwao ambayo mwisho wa siku wataleta mrejesho. Anayekutuma ndiye mwajiri wako. Hivyo huna budi kumueleza mwajiri wako kuwa ulichonituma nimefanya mpaka hapa.​

Inaonekana dhahiri kuwa sasa Baba Askofu Bagonza umeamua kuonesha chuki yako kwa serikali si tu kwa kuandika makala za kuichafua mitandaoni, bali hata kuhamasisha maandamano kwa kile unachosema ni kudai haki lakini nyuma ya pazia ukweli ni kwamba yale mambo mengi, makubwa na mazuri yaliyotekelezwa na serikali ya awamu ya tano hamyafuarahii wewe na wale wanaokutuma kumchafua Rais Magufuli na serikali yake.​

Mbali na kutambua kuwa unatumika Baba Askofu, naamini kuwa wewe binafsi pamoja na wale wanaokutuma ni mashuhuda wa kile ambacho Mungu kupitia mtumishi wake Dkt John Pombe Magufuli amaeifanyia Tanzania Hata kupelekea Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kuingia kwenye UCHUMI WA KATI.​

Unaposema "Maendeleo bila haki ni ibada ya sanamu" Tambua kuwa "Mtumishi wa Mungu kahamasisha maandamano ni dhambi kama dhambi nyingine" Kweli Nyani haoni kundule.​
 
Shida ni pale unapomlazimisha mtu kuwaza kama wewe, kuhisi kama wewe na kuenenda kama wewe. Siku mkijua hii dhana ya kwamba BINADAMU SIO MAROBOTI hamtaendelea kuwalalamikia wanaopinga serikari.

Jambo la msingi ni kwamba raisi asitishike na walalamikaji bali apambanae kufanya kadri ya uwezo wake. Hata ndani ya ccm kuna wanaompinga. So ni kitu cha kawaida sana kupingwa.
 
Hasira hizi ni effect ya kupungua mapato kanisani, jambo ambalo Mh Rais alilitahadharisha mapema kabisa kanisa kwani anafahamu fika kuwa walafi na mafisadi huchangia kwa kiasi kikubwa mapato ya kanisa.
Swali ni je? Tuendelee kukumbatia mafisadi na walafi ili kuziongezea taasisi za dini mapato au tuwaondoe ili Taifa zima lineemeke?
My take:
Ni hasira tu,
 
Baba Askofu endelea kuwanyoosha hawa madikteta uchwara na vibaraka wao, mpaka watakapo simama kwenye nnia sahihi. Mungu atakusimamia daima.
 
Back
Top Bottom