Mtumishi wa Umma kuingizwa kwenye bajeti ya 2020/2021 ili kurekebishiwa cheo lakini kupata barua mwaka 2022

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
4,730
Reaction score
6,736
Wajuzi wa mambo naomba tuelemishane hapa. Kuna ndugu yangu ambaye kwa sasa ni Afisa Biashara daraja la kwanza katika moja ya Halmashauri za manispaa nchini.

Katika kufuatilia kwake ili arekebishiwe cheo chake ili awe Afisa Biashara Mwandamizi ameambiwa ataingizwa katika bajeti ya mwaka 2020/2021 kitu ambacho kitafanyika miezi hii hii.

Kilichomshtua ni baada ya kuambiwa kuwa hata baada ya kuingizwa kwenye bajeti hiyo ya 2020/2021 lakini itabidi asubiri hadi mwaka 2022 (yaani miaka miwili baada ya kuwa ameingizwa kwenye bajeti) ndipo atarekebishiwa na kupewa barua ya mabadiliko ya cheo hicho kipya.

Je, wadau ndivyo utaratibu ulivyo?
 
Mkuu hiyo naona ndoo utaratibu wao kwa sasa,mm nimetoka masomoni 2019 lakini baada ya kupeleka vyeti ili wanibadilishie muundo wakasema ninawekwa kwenye bajeti ya 2020 ,kupata mshahara mpya mpaka 2021.Kwahiyo mwaka mzima kwenye bajeti na mwaka unaofuata ndoo unabadilishiwa mshahara ila inaumiza sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini mkuu baada ya kuwekwa jina lake kwenye bajeti ndiyo mtumishi asubirie miaka miwili kupata barua tu kwamba amepandishwa cheo?
 
Mkuu hiyo naona ndoo utaratibu wao kwa sasa,mm nimetoka masomoni 2019 lakini baada ya kupeleka vyeti ili wanibadilishie muundo wakasema ninawekwa kwenye bajeti ya 2020 ,kupata mshahara mpya mpaka 2021.Kwahiyo mwaka mzima kwenye bajeti na mwaka unaofuata ndoo unabadilishiwa mshahara ila inaumiza sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

watumishi ni wapumbavu tu... enddeleen kupmbn
 
Unwezakupata mjibu sahihi kutoka Wizara ya Utumishi ambao ndiyo wanapitisha majina ya wale waliopandishwa madaraja aidha kwa OPRAS au kuongeza elimu/ujuzi. Watakumabia taratibu na hata kwa wanaofanyiwa recategorization (kubadilishiwa majukumu ya kikazi) au wanaohama kwenda katika Taasisi/ Wizara/ Shirika ambalo mshahara ni mdogo au mkubwa. EMAIL ni ps@utumushi.go.tz
 
Hao wafalme ukiwaandikia email ukibahatika kupata majibu ya ulichoouliza utayapata baada ya miezi sita na kuendelea. Ndiyo maana wanyonge sie tunachanga changa majibu hapa hapa kwenye mada hii.
 
Exactly...

Wewe uliona wapi eti mtu unauliza swali (una shida) lakini utatuzi wake au jibu lake mpaka lipitie kwa na huko napo lazima lipitie kwa kisha lazima lihakikiwe na halafu lithibitishwe na mwishoni lihaririwe na kisha mwishoni kabisa ndipo likufikie wewe..!?

Stick around, majibu mumu humu.
 
Nina mfano wa jamaa mmoja, yeye alisumbuliwa sana na HR wake juu ya kurekebishiwa mshahara akalazimika kwenda yeye mwenyewe UTUMISHI suala lake lilishughulikuwa kule kule utumishi. Kwa hiyo, mara nyingine unakuta unaye HR lakini naye ni kama wewe hajui mambo mengi ya kiutumishi. Mfano suala la kurekebisha mishahara linagusa watumishi wengi kwa vile chanzo cha matatizo ni hao HR; hivyo, huwa wanakwepa kujikaanga kwa mafuta yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom