mtumwa hauawi jamani......

BabuDC umelala? Njoo ujibu hoja hapa.
 
Last edited by a moderator:

Ni vigumu kusema moja kwa moja kwa sababu binadamu tunatofautiana. Kuna watu wanapenda mwanamke au mwanamume ambaye hajichanganyi kabisa. Hata hivyo kuna watu wanachukia tabia ya kutojichanganya.

Binafsi napenda mtu ambaye yuko katikati..siyo chakaramu sana wala mother house wa kukaa jikoni 24/7!

Babu DC!!!
 
jamaa alishindwa nini kuwa wazi kwamba asingeweza kuendelea na uhusiano na huyo dada kutokana na situation aliyomkuta nayo... kusepa kimyakimya ni kuonyesha kwamba huna balls za ku-face reality head-on


Watu wanatofautiana,na si kila mtu anaweza kuwa na guts za kusema kila kitu kilichoko moyoni mwake. Ndiyo maana kuna watu wanajua sana kupepesa mdomo wakati wengine wanongea kwa vitendo. Kila njia ina madhara yake!

Babu DC!!
 
Watu wanatofautiana,na si kila mtu anaweza kuwa na guts za kusema kila kitu kilichoko moyoni mwake. Ndiyo maana kuna watu wanajua sana kupepesa mdomo wakati wengine wanongea kwa vitendo. Kila njia ina madhara yake!

Babu DC!!

kama aligonga mzigo halafu akaingia mitini kwa style hii atakuwa amemuumiza sana huyo dada.... why leave her guessing nini chaweza kuwa cause ya kukimbia kwake?
 
Dark City,

nimegundua mambo ni magumu kuliko nilivyofikiri.

Ila huyo nampongeza mwanamme huyo kuondoka mapema kabla madhara makubwa hayajafanyika.

Huyu Cindy naye pole zake naona alijipa matumaini makubwa mapema mno.

Ila sikujua kama kuwa mtalikiwa ni hasara.

Vipi tena wewe? Au wewe ndiye Candy?

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Ila sikujua kama kuwa mtalikiwa ni hasara.

jamaa alipima uwezo akaona maji marefu... btw mara nyingi mwanamke akishapata masahibu kama haya na asipokuwa makini anaweza kupata symphasisers wa uwongo ambao wanaweza kumharibia zaidi
 

Sisi tunawakimbia ninyi mnawanyanyasa, ngoma droo
 
huyo mwanamme sie kabisa,yani kusikia ana watoto unatoka mbio loh mungu asinikutanishe na kiumbe kama hiko..

Samahani sana kwa wale ambao hawatapenda comment hii,....hata hivyo huwa nalisema hili mara nyingi!

Mwanamke mwenye watoto anatakiwa kutafuta mwanamume ambaye ana watoto kama yeye. Ni kosa kubwa kwa mwanamume kujidanganya na kumwoa mwanamke mwenye mtoto/watoto.

Nayasema haya kutokana na uzoefu na wala siyo kwa nia mbaya ya kuwanyanyapaa dada zetu. Ndiyo maana huwa nawashauri wajukuu zangu kwamba, kama inawezekana, mtu asizae kabla ya ndoa!

Samahani tena kwa post hii,

Babu DC!!
 


Naomba kutofautiana na wewe ndugu yangu Kongosho,

Cindy anaonekana amekomaa kiasi cha kutosha (she is mature enough) na ndiyo maana yuko tayari kuweka CV yake mezani ili mtu ambaye yuko tayari kumbeba yeye na mzigo yake afanye informed decision. Alikuwa na uwezo wa kuficha kila kitu na kumwacha jamaa aamue huko mbele ya safari. Nadhani alishaonja machungu ya kufanya uamuzi kama huo na sasa hataki kufanya makosa tena!!

Naomba nikufahamishe kuwa kitendo cha kuwa mtalaka ni kizito...afadhali hata kuwa mjane....Kila mtu unayekutana naye lazima ajiulize kwanza; kwa nini alishindwa kudumu katika mahusiano yake ya awali....?

Na kwa mtu ambaye anaongozwa na akili zake zote (siyo tamaa ya ngono), hataweza kuamini kwamba mhusika hana kosa au mchango wowote katika kuvunjika kwa mahusiano yake ya awali! Na mhusika mara nyingi atakuwa na hisia kwamba labda anaonekana mkorofi/mkosefu, kiasi cha kusababisha mahusiano yake ya awali kuvunjika. Hili linafanya mchakato wa kujenga uhusiano mpya uwe mgumu sana kwa pande zote mbili, labda kama wahusika wamekaa kimaslahi zaidi!

Babu DC!!
 
Huyo mwanaume ****, vipi utamwingia mtu bila kufanya fact findings?


Kweli ila MadameX umesahau kuwa mtu anapoanzia kwenye tamaa zaidi basi uwezo wake wa kufikiria au kutumia busara unakuwa compromised!

Babu DC!!
 

Ok,nashukuru sana kwa jibu lako Babu DC
 
Hoja ipi tena kamanda,

Tumeshakueleza kuwa huyo dogo (mwanamume) kichwani ni mzima sana...

Lingine ni jipi?

Babu DC!!

Bishanga alimaanisha hoja yangu niliyokuuliza
 
kama aligonga mzigo halafu akaingia mitini kwa style hii atakuwa amemuumiza sana huyo dada.... why leave her guessing nini chaweza kuwa cause ya kukimbia kwake?

Kwa nilivyoelewa mm hao watu walikutana kwa mara ya kwanza wakaongea na baada ya hapo jamaa akingia mitini kwahiyo hayo mengine tunayofikiria hayakutokea. Binafsi naona angemuacha baada ya kula tunda majibu yangekua mengi.
 

Dark City duuuh nimeshtuka kidogo,mm nna watoto na sitafuti wanaume ila wao wananitafuta sasa inakuaje hapo???na wengi wao hawana watoto. Kwahiyo Babu ushauri wako nisikubali mwanaume yeyote ambae hana mtoto hata kama ameonyesha ana mapenzi na wanangu na mambo mengine mengi tuuuu...kweli nimkatae,kisa hana mtoto????!!!!
 
Last edited by a moderator:

Kama ndio mambo yenyewe haya MIMI BADO NIPO NIPO sanaaaa aiseee loooh
Ila mbona kwa wanaume inakua rahisi sana kuoa na kuacha,kuoa na kuacha kama mzee wetu Bishanga.....ina maana hili tatizo ni wanawake tu ndio wanakua na kasoro au?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…