doriani
Member
- Nov 24, 2019
- 42
- 38
Tukianzia kwenye miaka ya kiza mwenye nguvu ndie atawale. Vita inapotokea baina ya nchi na nchi au kabila hili na kabila lile, wale watakao shindwa vita, hao huchukuliwa kama mateka. Hivyo alieshinda vita hiyo ni hiari yao kuwauwa hao mateka au kuwatumia kwa shughuli yao kama Watsona inafaa kufanya hivyo. Ikiwa watawatumikisha basi hao huitwa watumwa.
Zanzibar imetawaliwa na Wareno, Waarabu, Waingereza na sasa inatawaliwa na Watanganyika. Maana ya kutawaliwa ni nchi kukosa maamuzi yake. Mfano mzuri ni pale tunapodhani kwamba mfalme ndio mtawala, lakini utawala gani huo kuanzia 1890,kila jambo kubwa na dogo ilikuwa lazima liamuliwe kutoka Uingereza.
Mfalme wa nchi alifanywa kua ni alama tu ya dola, hakuwa na uwezo katika kukata shauri juu ya uwendeshaji wa nchi.
Je! ipo tafauti gani hivi sasa ukilinganisha alivyokuwa mfalme zamani chini ya Serikali ya Uingereza na hivi sasa Rais wa Zanzibar chini ya Serikali ya Tanzania Bara?.
Kawaida ya Wakoloni popote Ulimwenguni wanapo tawala lazima watumie mbinu ya kuwagawa watu kwa kutumia asili za makabila yao. Angalia hivi sasa wananchi wa Zanzibar wanagawiwa kutokana na Unguja na Upemba, hapana tofauti, zote ni njia za kuwagawa watu. Kaburu ni Kaburu yeyote yule atakaefanya matendo, ya makaburu basi na yeye atakua Kaburu.
Ikiwa mzungu au Muafrika. Narudia tena. Muuza watu na muuza nchi ni nani mbaya zaidi?.
Huyu anaeuza watu ni mkoloni mkongwe na huyu anaeuza nchi kwa kuwatumia wale aliowateka vitani ni mkoloni mpya.
Vipi ukijiuliza kwani sisi Wazanzibari tulishindwa vitani? Ndio tulipovamiwa 1964 tulishindwa kujitetea kwa hiyo sote tumefanywa kuwa watumwa. Wako miongoni mwetu wamekubali kumtumikia mkoloni mpya na wengine wengi waliuwawa na wengine waasi wameendelea kuasi na kukataa kuwatumikia wakoloni wapya ndio hao wanaoitwa "wapinga Muungano" hawaitaki minyororo ya utumwa kwa kutumika kuimaliza Zanzibar.
Tanganyika ilifanya uvamizi sio Mapinduzi maana Mapinduzi lazima yapangwe, yaongozwe na yatekelezwe na wananchi wenyewe kwa faida ya nchi na wananchi wake. Tukiangalia yaliotokea Zanzibar yalipangwa, yaliongozwa na yalitekelezwa na wageni kutoka nchi za nje za jirani zetu. Ukweli huu unathibitishwa zaidi na yule alieongoza mavamizi haya Jemedari John Okello na wasaidizi wake akina Injini na Mfaranyaki.
Nani kati ya hao kitovu chake kimezikwa Zanzibar?. John Okello amezaliwa na kukulia kwao Uganda, Injini amezaliwa na kukulia kwao Kenya na Mfaranyaki amezaliwa na kukulia kwao Tanganyika wote hao walikuja Zanzibar wakiwa watu wazima na shughuli zao. Wamekuja kutafuta kibaruwa na kaukimbia kodi ya kichwa katika nchi zao.
Hata hivyo waliloliita Baraza la Mapinduzi utaona wengi wao hawakuwa Wazanzibari, si kwa kuzaliwa wala kwa kuchukuwa tajnisi (kuandikisha uraia).
Nyerere alikwksha wapenyeza wamakonde kutoka msumbiji kwa kuivamia Zanzibar na kisha akatuma askari 300 kuongeza nguvu juu ya uvamizi huo na kututeka na kutushinda na kuanzia hapo Wazanzibari tukubali tukatae ndio tulipokuwa watumwa.
Na miongoni mwa watumwa hao yaani Wazanzibari wakatokezea kuwa watumwa wa aina mbili, kuna yule mtumwa wa nyumbani yaani wale wanaotii na wale wanazurura yaani waasi wanapinga.
Mtumwa wa nyumbani anavaa vizuri maana huyu anaishi ndani ya nyumba ya bwana wake na anakula vizuri ingawa makombo ya bwana wake na hata kulala analala humo humo ndani ya nyumba ya bwana a wake ingawa yeye hulala sakafuni lakini ameridhika kwavile yuko ndani ya nyumba ya bwana (Muungano) wenzetu hao wakaridhika kwasababu yupo karibu na Bwana wake nduguzetu hao waliwapenda wamiliki wao kuliko hata hao mabwana kujipenda wenyewe.
Ndugu zetu hawa wanadiriki hata kujitolea maisha yao ili kuilinda nyumba ya mmiliki wake (Muungano) hata hata bwana mwenyewe. Kama tajiri wake akisema kwamba tuna nyumba nzuri hapa (Yaani Muungano) basi yule ndugu yetu mtumwa atarukia a tasema 'kweli Bossi tuna nyumba nzuri' kila wakati Bossi akitumia neno 'sisi' basi na hawa ndugu zetu watumwa watalitumia na wao neno hilo hawatasita.
Mfano kama nyumba ya bosi ikishika moto yule mtumwa atakimbia zaidi kuzima moto ule hata koliko mwenye nyumba mwenyewe, kama bwana akiumwa, utamkuta mtumwa wake akiuliza, vipi bossi hata sisi tunaumwa (kwa hali ya kumsikitikia na kumliwaza bossi wake) Alijitahidi kumtambuwa bossi wake zaidi ya bwana wake kujitambuwa mwenyewe.
Mtumwa wa sasa hana tofauti na mtumwa wa zamani. Anasema wapi nitakaa katika nyumba nzuri kama hii? Wapi nitavaa nguo nzuri kama hizi? Wapi nitakula chakula kizuri kuliko hiki?. Huyo ndio mtumwa wa nyumbani. Kwa kipindi hiki bado tunao humu nchini wanazunguka zunguka kuturudisha nyuma mitaani. Huyu mtumwa wa kisasa anampenda bossi wake sana. Anataka aishi karibu nae.
Ataridhika kulipa mara tatu ya thamani ya nyumba ili apate nafasi ya kuishi karibu na mabisi wake (viongozi wa juu) na kutamba kwa wenzake, "mimi ndie ninae stahiki pekee hapa" Ndio pekee katika kazi hii ndio pekee katika Chama hiki.
Tunawaambia wao si chochote zaidi ya mtumwa wa nyumbani kama wale watumwa wa zamani. Na kama mwenzake akimshauri kuondoka pale alipo basi atamwambia yale yale waliokuwa wakiyasema watumwa wa zamani katika mashamba, atamwambia mwenzake "unamaanisha nini ukisema tuondoke?" Tutoke kwenye Muungano? Muungano huu ni mzuri wa Waafrika.
Bwana wa watumwa wa zama hizo alimtumia nokowa kulinda wenzake, ndio hicho hicho kinachofanyika sasa kwani hawa vibaraka na makuwadi wa Muungano si lolote zaidi ya kuwa ni wajomba wa kisiasa tu. Kina mjomba wa karne ya 21 wanatumika kutulinda sisi na wanaturudisha nyuma. Wanatufanya tupende amani ambayo ni ya uongo ili tusiwe na vurugu.
Huyo ni bwana yule yule anaekufanya uwe hivyo ili uendelee kutawaliwa. Ni sawasawa umeenda kwa daktari wa meno ambae atakutowa jino lako, utampiga tu atapoanza kukutowa jino. Sasa itambidi aweke dawa ( sindano ya ganzi) kwenye taya zako ili usikie ganzi na hapo utakuwa unaumiya kwa amani kabisa. Damu itakuwa inamwagika katika taya zako na wewe utakua huwezi kuuhisi chochote Kikiendele. Eti kwa sababu kuna mtu anaekufanya uumie kimya kimya.
Wenzetu Wanatufanya jambo hilo hilo nchini mwetu. Wanapotaka kututumia watakavyo na wasiwe na hofu ya wewe kupigana nao huwa wanawatumia hawa ndugu zetu, wakituelekeza tusiache kuumia ila tuumiye kimya kimya! Wanatufundisha damu za raiya zimwagike mitaani. Wenzetu hawa wameuwachukua ndugu zetu, wakawavalisha vizuri wakawapa elimu kidogo ili sisi sote tuwatazame wao. Kwa njia hiyo iwe rahisi kuwa tawala wale waliobakia kupitia kwa hawa ndugu zetu.
Wengi miongoni tumetumika kuuza nchi badala ya kuuza watu. Lipi baya zaidi katika ya haya mawili?.
Malumbano ya kisiasa ya karne hii si ya biashara ya Utumwa au Wakoloni, huo sio ukombozi tunaoutafuta hivi sasa, maneno hayo hayana ushawishi hivi sasa. Katika hoja za kisiasa haya ndio maneno yenye ushawishi kwa kila mwenye kura:
Yalio muhimu hivi sasa ni uhuru wa mawazo katika kudhibiti uchumi wa Nchi yetu iliuwafikie wananchi na kukoma kudhalilishwa kwa wananchi kwa kukosekana kwa huduma muhimu yaani elimu nzuri, matibabu muwafaka na kuweza kujikimu kwa kila familia katika upatikanaji wa mahitaji muhimu ya siku hadi siku.
Haya ndio maneno yenye ushawishi kwa kila mwananchi, sio Uwarabu, Utumwa wala Usultani mategemeo ya wananchi ni:
Uhuru baada ya Ukolini
Neema badala ya Umaskini
Usawa badala ya Ubaguzi
Haki badala ya Uonevu na ukandamizaji
Piganieni haya mpokee nishani kwa wananchi sio watawala.