Wadau,
Inapendeza sana kuona kumbe humu ndani tupo wengi ingawaje hatujapata nafasi. Hata hivyo, am very sure kwamba hivi sasa opportunities za kufanya publishing zipo sana ila kinachotakiwa ni kuzitafuta. Uwepo wa opportunities za ku-publish kazi unaweza kuonekana na wingi wa machapisho kwenye hadi meza za magazeti. Hivi sasa, hususani Dar, kwenye meza za magazeti kumejaa vitabu vya aina mbalimbali wakati vingine havina kichwa wala miguu....hii inaonesha wazi kwamba, hivi sasa kutoa kazi si kazi sana bali kinachohitajika ni kazi bora yenye mashiko. Hapa chini ni ushauri tu wa nini watu kama mimi tunatakiwa kufanya:
1. Make sure unakuwa na muswada angalau mmoja ambao tayari umeshakamilika na tayari umeaririwa hata kama na washikaji wenye mapenzi na kusoma na wenye uelewa wa lugha. Hawa watu, tunao wengi mitaani.
NB: Kuna faida sana kuwa na muswada ambao tayari umeshakamilika kwani wakati mwingine huwa kunatokea na writing competition! So, kama unakuwa na muswada ulio tayari basi inakuwa rahisi sana kushiriki zinapotokea issue kama hizo.
2. Jaribu kutafuta angalau sh. 60,000/= uwe na Printer yako gheto...siku hizi catridge ambazo ni refilled zinapatikana si zaidi ya sh. 10,000/=. Ukishakuwa na Printer Yako, basi itakuwea rahisi ku-print muswada wako wewe mwenyewe.
NB: Publisher wengi, kama sio wote wanataka muswada uwe kwenye Double Spacing.
3. Ukishakuwa na muswada ambao tayari printed, jaribu kutembelea some of publishers.....kama nilivyosema, hivi sasa wapo....to mention few, especially well known publishers tunao Mkuki na Nyota, Heko Publishers, Big Horns na wengineo. Kuwafahamu hao wengineo, just jifanye umevutiwa na vitabu vilivyorundikana kwenye meza za magazeti....hawa jamaa wa magazeti hawakatzi kuviperuzi....kwahiyo, wakati unajifanya kuperuzi, kariri contacts za Publishers ambazo uandikiwa in the first or second page kisha go and google for more infos! By the way, mpenzi wa uandishi lazima atakuwa na angalau vitabu viwili vitatu home, so check for publishers.
4. Niliwahi kuongea na publisher mmoja, yeye aliniambia wazi kwamba hawana mpango na vitabu ambavyo tunajifanya kutoa new ideas kwa madai kwamba kila Mbongo anajifanya idea yako ndo bora! Hata hivyo, miswada ya riwaya anaipokea.
Let's work together...let's share our experience and am very sure that we'll make it! Na kama yupo member ambae ameshawahi kutoa kazi yake (sio gazetini) basi atupe experience yake!