Mtwango secondary school nafasi za masomo kwa mwaka 2013/14

adokila

Member
Joined
Jun 18, 2013
Posts
5
Reaction score
1
NJOMBE DISTRICT DEVELOPMENT TRUST
EDUCATION DEPARTMENT
SHULE YA SEKONDARI MTWANGO
S.L.P 370. NJOMBE
mtwaseco@gmail.com
Simu: +255756962462(mkuu wa shule)
Kumb.Na.MTSS/AD.I/VoIV/75
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 610"]
[TR]
[TD="width: 814"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
YAH: MAAGIZO YA KIJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI MTWANGO
UTANGULIZI
Ninayo furaha kukuarifu kuwa umechanguliwa kujiunga na kidato cha……katika shule hii kuanzia tarehe……..Hii ni bahati kubwa Sana kwako.Nimatumaini yangu kuwa utaitumia vizuri nafasi hii kwa manufaa yako mwenyewe,wazazi wako na taifa kwa ujumla.
Hii ni ya kutwa na ina hosteli.Utaishi nyumbani kwa mzazi au shuleni kwenye hosteli.Jaza fomu ya kukubali nafasi hii wewe na mzazi au mlezi wako.
Nenda Kwa daktari wa hospitali iliyo jirani nawe ili ukapimwe afya yako na kurudisha cheti cha Daktari hapa shuleni siku ya kujisajili
Nunua vifaa vyote muhimu ulivyoagizwa

A:MAHITAJI MUHIMU YA SHULE
(1)Wasichana
(a)Blauzi nyeupe mikono mifupi (2)
(b)Soksi nyeupe jozi mbili (2)
(c)Sketi mbili (2) rangi ya bluu bahari kitambaa kizito kwa ajili ya kuvaa wakati wa vipindi (darasani) mshono marinda nchi tatu (3) sketi ivuke magoti
(d)Sketi mbili rangi ya pinki za heshima Kwa ajili ya kuvaa baada ya vipindi kwa wale wa hosteli
(e)Tisheti mbili (2) rangi ya njano zisizo na maandishi
(f)Sweta mshono V isiyo na maandishi iliyoshonwa kwa uzi wa rangi ya kijani kibichi
(g)Viatu vya jozi moja, rangi nyeusi, visigino vifupi visivyo vya wazi
(h)Raba ya michezo jozi moja
(i)Bukta moja na fulana yake (rangi yoyote) kwa ajili ya michezo
(j)Fyekeo moja
(k)Sketi mbili (2) kitambaa kizito rangi ya kijani kibichi(kwa wanafunzi wa kutwa),mshono marinda nchi tatu(3)ivuke magoti
(l)Track suits rangi ya Bluu yenye “strips”nyeupe mikononi.

(2) Wavulana
(a)Mashati mawili meupe mikono mifupi.
(b)Suruali za heshima mbili (2) rangi nyeusi, mifuko mitatu kwa ajili ya kuvaa wakati wa darasani.
(c)Suruali za kushona mbili (2) rangi ya khaki, za kuvaa baada ya vipindi
(d)Sweta mshono V isiyo na maandishi rangi ya bluu iliyokolea
(e)Viatu vya ngozi jozi moja, rangi nyeusi na visigino vifupi visivyo vya wazi
(f)Raba ya michezo jozi moja
(g)Bukta moja na fulana yake (rangi yoyote) Kwa ajili ya michezo
(h)Jembe moja lenye mpini
(i)Suruali mbili (2) za heshima rangi ya kijani kibichi (kwa wanafunzi wa kutwa) mifuko mitatu kwa ajiri ya kuvaa wakati wa darasani
(j)Tisheti mbili (2) rangi ya njano zisizo na maandishi
(k)Track suits nyeusi yenye “strips”nyeupe mikononi.


WOTE:

B: ADA
Ada ya mwaka ni shilingi milioni moja tu(Tsh.1,000,000/=) kwa hosteli. Wale wa kutwa ni laki sita na nusu tu (650,OOO/=)

C: MICHANGO:
i).MCHANGO WA MAJI, MAJENGO, UMEME NA INTERNET TSH 60,000/=

ii).FEDHA YA TAHADHARI (CAUTION MONEY)
Uje na shilling elf kumi(Tsh 10,000/=) kwa ajili ya tahadhali(caution money)

iii.)KITAMBULISHO CHA SHULE
Uje na shilling elfu tano tu (5,000/=) kwa ajili ya kitambulisho
Picha mbili ndogo(passport size) kwa ajili ya matumizi ya shule.

iv).MITIHANI
Uje na bunda moja ya karatasi kwa ajili ya majaribio na mitihani ya ndani(photocopy A4 size)

v).CHAKULA (Kwa wale wa hosteli tu)
uje na sahani,kikombe na kijiko kwa ajili ya chakula

vi).MALAZI (Kwa wale hosteli tu)
Uje na:
a)Godoro la upana wa futi mbili na nusu na mto mmoja
b) Blanketi zito Mtwango ni eneo la baridi. Pia mashuka mawili: Wasichana rangi PINKI na wavulana rangi ya BLUU.
c).Taulo
d).Ndoo

vii).WANAFUNZI WA KUTWA NI WAZAWA MTWANGO TU.


viii).KURIPOTI SHULENI:
Unatakiwa kuripoti shuleni tarehe..............................…, saa nne(4.00)asubuhi.
Ili upokelewe unatakiwa uje na vifaa/mahitaji yote yaliyo orodheshwa hapo juu pamoja na stakabadhi ya benki(banki pay –in slip) isiyopunguwa shillingi:

  • LAKI TANO NA ELFU SABINI NA TANO(575,000/=)KWA WANAFUNZI WA HOSTELI,
Kwa muhula wa kwanza, 500,000/=muhula wa pili

  • LAKI NNE(400,000/=) kwa muhula wa kwanza,325,000/=kwa muhula wa pili kwa WANAFUNZI WA KUTWA.
Malipo yote yafanywe benki kwenye akauti zifuatazo
1. NBC
MTWANGO SECONDARY SCHOOL
ACCOUNT NO.039103001206
2. NMB
MTWANGO SECONDARY SCHOOL
ACCOUNT NO.6063500087
3. CRDB
MTWANGO SECONDARY SCHOOL
ACCOUNT NO.0150349760200
Pembeni kwenye “pay in slip”andika ada ya………………..(jina la mwanafunzi).Unaporipoti uje na hiyo”pay in slip”.
………….MKUU WA SHULE………………Tarehe




















REQUEST FOR MEDICAL EXAMINATION

PART A:
TO THE MEDICALOFFICER
…………………………………………..
…………………………………………..
…………………………………………..
…………………………………………..
FROM THE HEADMASTER
MTWANGO SECONDARY SCHOOL
PO BOX 370
NJOMBE.
RE: Mr/Miss………………………………………………………………………………..
Please examine the above named as to her or his fitness for admission as a student at mtwango secondary school
Date……../……../…….

Signature………………..

Stamp……………………
PART B:
MEDICAL CERTIFICATE
(To be completed by the medical officer)
I have examined the above mentioned and consider that he/she is physical fit /unfit for admission as a student to the said school.

Date…….../……/….. Signature………………………

Station…………….. Designation…………………….

Stamp………………………….










WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
SHULE YA SECONDARY MTWANGO


SHERIA ZA SHULE
Kila mwanafunzi lazima asome shelia hizi kwa uangalifu azielewe,azifuate na kuzitii.
Uvunjaji wa sheria yoyote ya shule hata kama ni ndogo kiasi gani hauta vumiliwa katika shule hihi na shirika la NDDT kwa ujumla.

MAKOSA YANAYO WEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULE
Makosa yafuatay yana weza kusababisha mwanafunzi kufukuzwa shule mara moja.
1. Wizi wa aina yoyote
2. Uasherati
3. Ulevi wa aina yoyote
4. Uvutaji bangi
5. Makosa ya jinai
6.Kupigana
7. Kuharibu Kwa makusudi Mali ya umma
8. Utolo shuleni
9. Kudharau bendera ya Taifa
10. Kutofanya mtihani wowote unaoandaliwa na shule
11. Kutotii ratiba ya shule
12. Kusababisha au kushiriki katika migomo
13. Kumiliki simu ya mkononi ukiwa shuleni

MENGINEYO
1. Unatakiwa kuvaa mavazi rasmi ya shule wakati wote
2. Hutakiwi kukaa na madawa bwenini bila idhini.
3. HURUHUSIWI KUWA NA SIMU SHULENI.NI MARUFUKU
4Unatakiwa kula chakula kilicho andaliwa na shule.
 

Attachments

umetuwekea joining instruction? mi nilitegemea kuliona Tangazo. Anyway, nilisoma hapo 'O' Level. it was a good school.
 

Adonaye Kila..... Sasa hii kitu gani tena jamaa yangu? Its adv or what?
 
Anakutaarifu kuwa umechaguliwa kujiunga fomu wani..

Hahahahahahahahaaa. Huyu jamaa namfahamu kwa sura hadi mavazi sasa hiki kitu alicho kipost hapa hafanani nacho kabisa...... He is above 32..... sasa imenibidi nicheke tu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…