BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mahakama ya Wilaya ya Mtwara imemhukumu kwenda jela miaka 30, Salum Shamte (35), Mkazi wa Libobe wilayani hapa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.
Hukumu hiyo imetolewa siku ya Alhamisi Machi 23, 2023 (jioni) na Hakimu wa Mahakama hiyo, Lucas Jang'andu baada ya kuridhishwa na maelezo ya mashahidi watano waliotoa ushuhuda wao mbele ya mahakama.
Kesi hiyo namba 21 ya mwaka 2021 ilifikishwa mbele ya Hakimu Jang'andu kwa mara ya kwanza Februari 18, 2022 na Mwendesha Mashtaka wa kesi hiyo alikuwa Wakili wa Serikali Gedion Magesa.
Awali ilielezwa mahakamani hapo kuwa Shamte alikamatwa baada ya polisi waliokuwa doria eneo la Libobe kufika na kufanya upekuzi nyumbani kwa mshtakiwa huyo kufuatia taarifa za kiintelijensia walizozipata na kukuta kiroba cha kilo 12 za dawa hizo aina ya bangi.
MWANANCHI