Mtwara: Ilipotoka, ipo wapi sasa na inaelekea wapi?

Mtwara: Ilipotoka, ipo wapi sasa na inaelekea wapi?

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Nilikuwa nasoma kitabu kilichoandikwa na Michael Longfold kiitwacho "The Flag Changed at Midnight: Tanganyika's Progress towards Independence." Katika kitabu hiki, Michael Longfold anaelezea ushuhuda wake wa macho kama mfanyakazi (District Officer) wa utawala wa kikoloni katika miaka 10 ya mwisho kabla ya Tanganyika kupata uhuru.

Michael Longfold alifanya kazi sehemu mbalimbali Tanganyika zikiwemo Iringa na Rungwe kabla ya kuhamimishiwa Mtwara kuwa Staff Officer wa Kamishna wa muda wa Southern Province (Jimbo la kusini lililojumuisha Lindi na Mtwara). Kitabu kina jumla ya kurasa 572. Hata hivyo, ningependa, ku-share Sura ya Nne yenye kichwa "Southern Province" hasa kutokana na yanayoendelea Mtwara hivi sasa.

Wapo ambao hawapendi kujua yaliyopita, lakini kwa hili suala la gesi nadhani siyo vibaya kutakafari Mtwara ilitoka na kujiuliza ilipo sasa na inaelekea wapi. Hii itasaidia kujua kama Mtwara iko kwenye mkondo mzuri. Kitabu kimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza; nitajitahidi kuelezea hiyo ibara ya nne kwa Kiswahili kadri ya uwezo wangu kwa faida ya wengi.

Waliosoma historia watakumbuka kuwa hadi mwaka 1953, makao makuu ya Southern Province (kwa sasa Kanda ya Kusini) yalikuwa Lindi. Makao makuu ya mji wa Mtwara yalikuwa Mikindani. Bandari mpya na yenye kina kirefu ilikuwa imeshajengwa Mtwara na mji mpya ulikuwa unaandaliwa chini ya ramani nzuri kabisa ambayo iliruhusu mji kupanuka siku za usoni.

Mpango wa kujenga mji wa Mtwara kama bandari kubwa kusini mwa Tanganyika ulikuwa sehemu ya mpango mzima wa kilimo cha karanga. Mpango huu ulianzishwa na serikali ya Labour ya Uingereza iliyoingia madarakani mwaka 1945 chini wa Waziri Mkuu, Clement Attlee.

Baada ya kuingia madarakani, serikali ya Clement Attlee ilipitisha sheria mbalimbali (ambazo ni maarufu sana nchini Uingereza hadi leo) ili kukabiliana na matokeo ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mojawapo ni ile sheria (National Health Service Act) iliyoanzisha huduma ya afya kwa taifa (National Health Service, kwa kifupi, NHS). Sheria hii iliwawezesha Waingereza kupata huduma ya afya bure mpaka leo.

Tatizo lingine ambalo serikali ya Clement Attlee ilitaka kulitatua ni utapiamlo uliosababishwa na Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Baada ya vita kulikuwa na ukosefu wa vitu kama mafuta ya kupikia. Mwaka 1946 serikali yake iliamua kupitisha mpango ambao ulihusisha hekari milioni tatu za ardhi ya Tanganyika ambayo ingetumiwa kwa ajili ya kilimo cha karanga ili kupunguza tatizo la ukosefu wa margarine fats, moja ya mafuta ambayo yangesaidia kutatua tatizo la utapia mlo Uningereza.

Mwaka 1948 serikali ya Clement Attlee ilipitisha sheria ambayo siku hizi imesahaulika kabisa kwenye vitabu vya sheria. Sheria hii iliitwa Overseas Resources Development Act 1948. Sheria hii ilianzisha Shirika la Chakula la Nje (Overseas Food Cooperation), kwa kifupi OFD.

OFD ilipewa mtaji wa kuanzia wa Pounds milioni 50 na kuanza rasmi mpango wa kilimo cha karanga mwaka 1948. Kutokana na umuhimu wa mpango huu, haukusimamiwa na ofisi ya makoloni bali wizara ya chakula. Aliyeusimamia mpango huu alikuwa generali wa jeshi.

Baada ya kufanya majaribio ya kilimo cha karanga sehemu mbalimabli Tanganyika kama Kongwa na Urambo, OFD iliona kuwa zao la karanga lingeweza pia kustawi Nachingwea. Pia reli ilijengwa kwa ajili ya kusafirisha karanga kwenda bandarini Mtwara. Uingereza ilitarajia kuvuna tani 400,000 za karanga kwa mwaka na kuzisafirisha nje kwa ajili ya kushughulikia tatizo la utapiamlo.

Lakini mpango mzima wa kilimo cha karanga Nachingwea ulikumbwa na matatizo makubwa ikiwa ni pamoja na taratibu mbaya za mipango, ukaguzi wa hesabu na marejesho. Kwa mfano, walijenga bandari yenye kina kirefu lakini baadae wakaja kugundua kuwa maji yalikuwa na kemikali zenye madhara kwa boilers za meli.

Muhimu zaidi, wakati mpango wa kilimo cha karanga ulipokufa mwanzoni mwa miaka ya 1950, iligundulika kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya fedha na zana za kilimo yaliyosababishwa na usembe na rushwa. Kwa mfano, matrekta yalikuwa yanapotea ovyo Nachingwea, sehemu ambayo haikuwa na watu wengi wala barabara nzuri.

Kwa hiyo, kilimo cha karanga kikafa rasmi mwaka 1950-1951 baada ya wizara ya chakula kuachana na huo mpango na nafasi yake kuchukuliwa na ofisi ya makoloni. OFC nayo ilikufa rasmi mwaka 1954 baada ya kubadilishwa na kuwa Shirika la Kilimo Tanganyika (Tanganyika Agricultural Corporation aka TAC).

Waliopanga mpango mzima ya kilimo cha karanga ni kama vile walikuwa wanaishi maisha ya ndotoni. Of course, wapo wachache ambao walikuwa na matumaini kuwa mpango huo ungefanikiwa. Hata hivyo, mpango wa kilimo cha karanga uliajiri wataalamu wengi kutoka Uingereza ambao walikuwa na nia tuu ya kunyonya mali za wenyeji tena bila ridhaa yao.

Hawakuonyesha kabisa moyo wa kutaka kuiendeleza South Province na watu wake. Wananchi wa maeneo husika hawakushirikiswa kabisa wakati kilimo cha karanga kilipoanzisha kilimo. Hii ilisababisha kuvunjika kwa uhusiano uliokuwepo kati ya watawala wa Kiingereza na Waafrika na Waasia. Mtwara ni mfano wa jinsi kilimo cha karanga kilivyokufa. Zipo pia historia mabaya ya kilimo cha karanga Kongwa na Urambo.

Mwanzoni, mji wa Mtwara ulikuwa umepangwa kusaidia maelfu ya wakazi wake hapo baadae na pia kuvutia wakazi wapya. Waingereza walikuwa na mpango wa kujenga mji maarufu wenye vitu kama maktaba, sehemu za kuombea, shule, hospitali, kumbi za sinema, n.k. Lakini mipango yote hii iliwekwa kapuni baada ya kuanguka kwa kilimo cha karanga.

Inakaridiwa kuwa mwaka 1954 Mtwara mjini ilikuwa na wazungu 100, Waasia 50 na Waafrika 700. Wazungu wengi walikuwa wameajiriwa serikalini na hawakuwa na mpango wa kuishi Mtwara baada ya kustaafu. Walikuwepo pia Waafrika wachache waliokuwa wameajiriwa serikalini lakini wengi wao walikuwa wametokea nje ya Mtwara na walikuwa hawana mpango wa kuishi Mtwara.

Waasia walikuwa wamejikita zaidi kwenye biashara ya maduka baada ya kushawishiwa kuwa wangekuwa matajiri haraka kama wangeanzisha biashara Mtwara. Hata hivyo, wafanyabiashara wengine walikuwa makini zaidi na kuogopa kuomba vibali vya kumiliki ardhi.

Kimsingi, kuanguka kwa mpango mzima wa kilimo cha karanga Mtwara, ambao uligharibu fedha nyingi, kuliharibu sana heshima ya Uingereza kimataifa kama nchi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Mataifa kuindaa Tanganyika kupata uhuru.

Pia utawala ya kikoloni ulikuja na mpango wa kuhamisha makao makuu ya Mtwara kutoka Mikindani kwenda Mtwara mjini ya sasa bila ridhaa ya wananchi. Wananchi wa Mtwara waliupinga sana mpango huo kwa madai kuwa hawakushirikishwa kabisa. Maamuzi ya kulifunga boma la Mikindani yalitoka Dar Es Salaam, na siyo Mtwara.

Mwandishi anasema alibahatika kulipitia faili ambalo lilikuwa na nakala ya barua ya uamusi wa kuhamisha makao makuu ya mji na kukuta malalamiko mengi ya kimaandishi kutoka kwa wakazi wa Mikindani lakini hakuna aliyehangaika kuwasikiliza.
 
Nilikuwa siijui mtwara kihistoria pamoja na kuwa mdau wa mtwara,makala ya jana na ya leo zimenitoa tongotongo sana,natamani killa maktaba ya mkoa yenye kitabu chenye historia ya mkoa husika!!!
 
Wanahaki yakulalamika na mbaya zaidi kutendewa na watanganyika wenzao. Tuweke utawala wa majimbo na federal government.
 
mabango.jpg

What it only need now is its own KEN SEROWIWA figure then thats it.

This is what happens when a Government gives half baked answers to the People of Mtwara.
 
George Ngolwe ndiyo iliishia hapo. Baada ya hapo Tanganyika ilipata uhuru na mwandishi kurejea zake Uingereza.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu EMT,

Kuna sababu nyingi ikiwa ni pamoja na miundo mbinu duni. Kwa wale waliokuwa na ufahamu, miaka ya 70 ma 80 hadi 90 mwanzoni usafiri wa kwenda kusini ulikuwa seasonal.

Majira ya mvua bara bara na madaraja hayakupitika kabisa. Ilibidi kusubiri meli zizlizokuwa zinasafiri kwa baadhi ya siku kama si mwezi.

Hili lilifanya watu wa sehemu nyingine kutokuwa tayari kuhamia Kusini kuchelea adha ya usafiri. Maendeleo ya sehemu yanatokana na mwingiliano wa watu na mwamko wa wakazi wake. Hilo la kukosekana kwa mawasiliano limeathiri sana kusini katika namna nyingi sana.

Tangia kumalizika kwa daraja hali inaonekana kubadilika kwani uhamiaji kwenda kusini unaongezeka. Changamoto iliyobaki ni kwa wakazi wa kusini kubadili utamaduni. Nimeshawahi kulijadili na akina Jokakuu ya kuwa maendeleo yanaanza na wenyeji kwanza. Sasa utamaduni wa watu wa kusini kuhama makwao unawaathiri sana.

Mathalani, gesi ya songo songo ipo kuanzia miaka ya 80. Kutokana na wakazi wa huko kuhama basi ile ''elite'' group iliyotakiwa kuhoji matumizi na umhimu wa gesi hiyo haikuwepo. Wakabaki raia wa kawaida tu.

Nafaham wapo watakaouliza, je, kwasasa wananchi wanapigania rasilimali hiyo ina maana wakazi wameanza kurudi! Jibu ni rahisi kuwa ujenzi wa miundo mbinu umesaidia sana watu wa kusini kusafiri na kujifunza kutoka kwingine lakini pia watu wanaohamia kule wanakuwa sehemu ya chachu ya maendeleo kwa kutoa mawazo mbadala.

Kwa maneno mengine ile kazi iliyokuwa ifanywe na akina Kawawa,Majogo, Mkapa n.k. sasa inafanywa na wahamiaji kwa kuhamasisha wakazi wa huko kujitambua na kuamka.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu EMT

Mada nzuri kweli kweli unanikumbusha JF ya wakati uleeeeeeeeeeeeee.
 
Mkuu Nguruvi3

Kweli kutokuwepo kwa mawasiliano kuliwatenganisha watu wa kusini na sehemu nyingine za nchi. Hata baada ya uhuru hawakupata nafasi ya kujifunza kutoka sehemu nyingine. Kanda ya kusini ina utajiri mwingi tuu kuanzia madini ya chumvi, korosho, gesi, n.k. Hata hivyo, suala limekuwa ni jinsi gani wananchi wa Kusini wamenufaika na utajiri huo.

Pamoja na utajiri huo bado wananchi wa kusini wana hali ngumu ya maisha. Hii ilifanya serikali kupunguza bei ya kuunganishiwa umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kutoka Sh 455,000 kwenda Sh 99,000 kwa nyumba zilizo ndani ya meta 30 kutoka nguzo ilipo.

Lengo la serikali lilikuwa kuwanufaisha wananchi wa kusini hasa na gesi inayozalishwa huko. Punguzo hilo lilitarajiwa kumalizika mwezi Disemba mwaka jana. Hata hivyo, wakazi wengi wameshindwa kunufaika na punguzo hilo kutokana na aina makazi ya makazi yao.

Serikali haikuwapa wakazi wa kusini muda wa kutosha kuyaboresha majengo yao. Nimesikia kuna punguzo lingine la kuunganishiwa umeme ambalo lilitarajiwa kuanza mwezi huu lakini siyo tuu kwa wakazi wa Mtwara na Lindi bali pia kwa Watanzania wote.

Hata hivyo, punguzo la Januari si la chini kama lile la Disemba. Kama wananchi wengi wa Mtwara na Lindi walishindwa kufaidika na punguzo la Disemba mwaka jana watawezaje kunufaika na punguzo jipya la Januari mwaka huu? Serikali inaweza kujikuta inafanya yale yale yaliyofanywa na wakoloni bila kuwa na planning na kuwahusisha kwa karibu zaidi stakeholders wa kusini.

Kuna umuhimu wa kutafuta njia mbadala wa kuwasaidia wakazi wengi wa mikoa ya kusini ili wanufaike na umeme wa gesi unaozalishwa katika maeneo yao kwa kuwatafutia namna ya kuezeka nyumba zao. Nilisoma mahali kuwa Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa na mikakati wa kusomesha vijana wa kusini kwenye vyuo vya VETA kuhusiana na masuala ya gesi na mafuta.

Kama vijana wa kusini watanufaika na mpango huu sijui, lakini hivi karibuni kulikuwa na tangazo kutoka Ikulu kuwa Tanzania inatafuta wataalamu wa Kitanzania kwenye mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi asilia na mafuta.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu EMT,
Kwakweli nina bahati ya kusafiri Tanzania kwa kiasi kikubwa sana. Katika safari zangu za maisha nimewahi kuishi mikoa ya kusini Mtwara na Lindi tena vijijini. Hali ni mbaya sana. Tunasema Tanzania hali ni mbaya, lakini kuna sehemu ni zaidi.

Ni kupitia uzoefu huo ambao pia upo kule Tanga nimekuwa nasema maendeleo ya sehemu husika kwanza yanaanza na wenyeji. Nitatoa mfano, katika mkoa ambao viongozi wao wanaishi kule baada ya utumishi hali ni tofauti sana.
C.D.Msuya ni mjumbe katika wilaya ya Mwanga, mweka hazina wa chama wa Wilaya na mjumbe wa taasisi nyingi.

Moja ya mafanikio makubwa ya mji wa mfano barani Afrika(namba 5) ni Moshi. Angalia timu inayounda madiwani na hata viongozi wa vitongoji. Wengine nafasi zao za zamani ni katika ukataibu mkuu, ukurugenzi n.k.

Ni kwa utaratibu huo tumeona wakazi wa maeneo kama Mbeya, Iringa, Bukoba, Musoma na kwingineko wakirejea makwao japo baada ya muda fulani. Heshima ya mtu wa kabila la Wahaya ni kuwa na Nyumba nzuri kijijini kabla ya mjini.

Ninaposema wananchi wa Kusini wabadili tabia, I real mean it! Wengi wao wana nafasi nzuri sana sehemu nyingine na wakifika huko nyumbani ndio basi tena.
Wanajamvi si wasumangi watu atakayekwazi namuomba radhi tunatafuta mawazo.

Mkapa ameamua kwenda kuishi Lushoto na si Mahuta, Masasi au Nakapanya. Nitty gritt!
Ndivyo ilivyo kwa mlololongo wa viongozi na wananchi wengine tunaowafahamu.

Hizo nyumba ulizoona ni za wazazi wao, wenyewe wapo Dar na kwingineko. Kwavile hakuna anayerudi nyumbani masikini wazazi hao wamebaki katika maisha duni na vijana waliobaki uwezo wao unafikia ukomo.

Nadhani wanahitaji msaada kama uliyosema.Na msaada huo uanze kwanza kwa kuwaambia ukweli! Warudi kuendeleza nyumbani walikoacha wazazi wao. Huko kwingine ni ugenini tu.

Pili, suala la gesi wana hoja ya msingi kabisa. Hoja yao ni kuwa hatua za awali za kusafisha gesi hiyo na mambo mengine zifanyike huo ili zilete tija.
Hapa napo tunaona athari za kutokuwa na watu wa kuwasemea.Leo hoja yao imegeuzwa na kuonekana kama vile hawataki kutumia rasilimali kwa nchi nzima.

Nadhani akina vita Kawawa na Mkapa walikuwa katika uwezo mzuri kabisa wa kuiambia serikali isipotoshe madai yao ya msingi kwa kuchomeka hoja zisizo akisi madai yao. Nguvu ya hoja haipo kwasababu wanaoweza kujenga hoja wamehama liwalo na liwe.

Ningependa kuona gesi inainua kiwango cha maisha ya kusini na nakubaliana na EMT kuwa something must be done.

Kitu kimoja ambacho ningewaasa (nayo ni athari ya kutokuwa na weledi) ni hatari inayowakabili kwa kugawanyika.
Madai yao ni ya msingi na yana sababu za msingi,vinginevyo CCM na JK wasinge haha kubadili hoja.
Sioni kwanini waanze kugawanyika katika misingi ya udini.

Mimi sikupendezwa na makundi ya dini kuanza kutoa kauli. Ninafahamu haki ya mtu au watu kutoa maoni, lakini kimkakati hilo ni jambo baya. Leo kila aliyewaunga mkono anabaki kujiuliza kama madai yale ni kama yalivyo au yanajingine nyuma

Wao wanatakiwa wawe kitu kimoja na kusimami kwa nguvu kabisa hoja yao bila kuondolewa katika maudhui na hoja dhaifu za serikali.

Na mwisho, lazima wajiulize kama miaka 50 ni michache na wanahitaji 50 mingine kuondoka walipo.

Kitu nisichoafiki ni wao kupewa kipaumbele.
Positive affirmative action haijawahi kumsaidia mtu au taifa.

Ni lazima kwanza waanze na kubadili utamaduni.
Kuhusu kusaidiwa nyumba, hilo siafiki kwasababu yupo mtu wa mkoa mwingine aliyejikusuru hadi akapata kibanda kinachoweza kuhimi nyaya za umeme.

Kwamba gesi itumike kubadili hali zao hilo naliunga mkono kabisa. Vyovyote iwavyo kwa sababu za kisiasa au kiuchumi, bado wanahitaji kufaidika na gesi ili kuinua maisha ya wazee waliobaki Lindi na Mtwara.
 
I wonder if our leaders adopted this "wameshindikana" attitude.

I dont even see a case being made to justify the governments bully pulpit.

A fellow like myself, deeply steeped in economic utilitarianism, expected the government to lay down a comprehensive case contrasting the merits and demerits of processing in Mtwara, including the numbers, considerations to decentralization initiatives, demachinganization, or even stating that it is interested in the merit of the plain numbers.

If there is such a case somewhere, I haven't seen it.

I am not one to encourage whining, regionalism or sectarianism, but I have to wonder what is the government's M.O.
 
Mkuu EMT,

Kuna sababu nyingi ikiwa ni pamoja na miundo mbinu duni. Kwa wale waliokuwa na ufahamu, miaka ya 70 ma 80 hadi 90 mwanzoni usafiri wa kwenda kusini ulikuwa seasonal.

Majira ya mvua bara bara na madaraja hayakupitika kabisa. Ilibidi kusubiri meli zizlizokuwa zinasafiri kwa baadhi ya siku kama si mwezi.

Hili lilifanya watu wa sehemu nyingine kutokuwa tayari kuhamia Kusini kuchelea adha ya usafiri. Maendeleo ya sehemu yanatokana na mwingiliano wa watu na mwamko wa wakazi wake. Hilo la kukosekana kwa mawasiliano limeathiri sana kusini katika namna nyingi sana.

Tangia kumalizika kwa daraja hali inaonekana kubadilika kwani uhamiaji kwenda kusini unaongezeka. Changamoto iliyobaki ni kwa wakazi wa kusini kubadili utamaduni. Nimeshawahi kulijadili na akina Jokakuu ya kuwa maendeleo yanaanza na wenyeji kwanza. Sasa utamaduni wa watu wa kusini kuhama makwao unawaathiri sana.

Mathalani, gesi ya songo songo ipo kuanzia miaka ya 80. Kutokana na wakazi wa huko kuhama basi ile ''elite'' group iliyotakiwa kuhoji matumizi na umhimu wa gesi hiyo haikuwepo. Wakabaki raia wa kawaida tu.

Nafaham wapo watakaouliza, je, kwasasa wananchi wanapigania rasilimali hiyo ina maana wakazi wameanza kurudi! Jibu ni rahisi kuwa ujenzi wa miundo mbinu umesaidia sana watu wa kusini kusafiri na kujifunza kutoka kwingine lakini pia watu wanaohamia kule wanakuwa sehemu ya chachu ya maendeleo kwa kutoa mawazo mbadala.

Kwa maneno mengine ile kazi iliyokuwa ifanywe na akina Kawawa,Majogo, Mkapa n.k. sasa inafanywa na wahamiaji kwa kuhamasisha wakazi wa huko kujitambua na kuamka.

Kwa upande mmoja ni lazima kukubvaliana na wewe, hasa tukijikita kwenye aina ya uchumi ulioanza kujengwa na serikali zetu kwa maana kwamba baada ya uhuru, hizo kweli zilikuwa ni changamoto!

Ila tukirudi kwenye hicho kipindi cha serikali ya ukoloni naamini suala la miondombinu ilikuwa ni changamoto ya sehemu kubwa tu ya eneo zima, hivyo toka mkoloni alipokuwa anaweka mipango yake alilijua hilo ndio maana akawa ana mipango ya kuimarisha miundombinu mbadala kama reli na hiyo andari ya kina kirefu....

Ladba kitu ambacho ninachoona kimeendelea kuwa changamoto nzito zaidi kwa ndugu zetu wale ni "Utamaduni wao" na namna wanavyojiweka wao wenyewe, hii imepelekea kuwa rahisi sana kutokuwachukulia kama ni watu wa maana hadi kuwashirikisha kwenye mipango mikubwa inayowaathiri wao wenyewe.... Hapa ndio tatizo kubwa linapoanzia!

Wakoloni waliwapuuza wenyeji wenye mji ambao wao siku zote ndio wameelewa tabia za mazingira yao na ndio wenye uwezo wa kucheza na hizo tabia za mazingira yao.
Kwa kupitia hali hii ya kuwapuuza wanamtwara hata sasa bado tumekwama kwenye mtego huo huo hata serikali za CCM mara zote zimeendelea kuwa dharau watu wale hadi kwenye hili la gesi hivyo ni baya sana kuwa hata hizi hadithi za gesi kuna sehemu zitakwamia tu kwa dhambi ile ile ya kudharau wazawa na wenye mali ambao nguvu za asili ziliwapa dhamana.

Hilo ndio tatizo na changamoto kubwa sana kuliko miondombinu!!!
 
Back
Top Bottom