The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa viongozi kuhakikisha wanawasaidia vikundi mbalimbali ili wajue namna bora ya kutimiza vigezo vya kupata mkopo wa aslimia 10 unaotolewa na halmshauri.
Sawala ametoa rai hiyo wakati wa kikao maalum cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kuhusu mapitio ya bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2024/2025 na makadirio ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo Serikali ya mkoa huo imekisia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 290.2.
Ameongeza kuwa vipo baadhi ya vikundi vinashindwa kupata mkopo kutokana na kushindwa kutimiza vigezo licha ya kuwa fedha imetengwa kwaajili yao hivyo amewataka wahusika kushirikiana na wabunge na Madiwani kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kupata mikopo.
Nae Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mtwara Agnes Okololo amempongeza Rais samia kwa kufungua tena dirisha la mkopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambapo kwa awamu hii fedha wanazokopeshwa zinasaidia kuchechemua maendeleo kwa walengwa na amewaomba wahusika kuweka nguvu kubwa kwenye utoaji wa elimu ukizingatia mfumo wa uombaji ni wa kidijitali.
Akiwasilisha taarifa ya mpango huo wa bajeti ya Mkoa huo wa Mtwara kwa mwaka huo 2025/2026, Katibu Tawala msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Mtwara Abdillah Mfinanga, amesema katika fedha zilizokadiriwa kukusanywa kwa mwaka huo 2025,2026 shilingi bilioni 2.9 zitatumika kwaajili ya mikopo hiyo ya asilimia 10, ambapo wakawake shilingi bilioni 1.2, vijana 1.2 na watu wenye ulemavu ni milioni 592.
Hata hivyo katika mwaka huo wa fedha Mkoa wa Mtwara unakadiria kupokea na kutumia fedha za ruzuku jumla ya shilingi bilioni 62.3 ambapo fedha za ndani ni bilioni 29. 02 sawa na asilimia 46.54 na fedha za njeu shilingi bilioni 33.3 sawa na asilimia 53.45.
Kati ya fedha hizo, ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo inakadiria kupokea na kutumia shilingi bilioni 4.5 zikiwemo fedha za ndani bilioni 2.3 sawa na asilimia 51.11 na fedha za nje bilioni 2.1 sawa na asilimia 48.88.