Mtwara: Mkuu wa Mkoa atoa saa 48 za kukamilisha Madarasa 452

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza Halmashauri zote mkoani humo kukamilisha majengo 452 ya madarasa ndani ya saa 48. Madarasa hayo 452 yamejenga na fedha za Uviko-19 na yapo katika hatua ya umaliziaji.

Akizungumza Desemba 7, 2021 wakati wa kupokea vyumba vya madarsa 22 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya, Gaguti amesema kuwa Halmashauri zote zinatakiwa kufanyakazi usiku na mchana ili kukamilisha madarasa hayo ndani ya saa 48.

Amesema kuwa madarasa hayo yanajengwa kwa fedha za Uviko-19 ambapo kwa Manispaa ya Mtwara Mikindani ampokea madarasa 22 yenye thamani ya Sh440 milioni.

"Nataka hadi kufikia Desemba 10 mwaka huu madarasa 452 yenye thamani ya Sh11.67 bilioni yawe tayari nimekabidhiwa fanyani kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo" ameagiza Gaguti

"Tuendelee kujenga majengo yetu kwa kasi hii hii ni dhambi kwa watumishi kupewa fedha za ujenzi wa miradi na kushindwa kukamilisha kwa wakati tunakuwa hatutendi haki kwa wananchi na Serikali pia"

"Tunazo zaidi ya Sh11 bilioni kwenye miradi ya afya na elimu nataka ikamilike kwa wakati ili shughuli zingine za maendeleo ziweze kufanyika ingawa kwa leo nakagua madarasa" amesema

Chanzo: Mwananchi
 
IMG_3804.jpg

Jinsi zege inavyosoma hizi taarifa.
 
Waache ufanyaji kazi wa hivi. Tayari makosa yalishafanyika kwenye usimamizi, kuwapa saa48 ni chanzo cha kuzima moto na kuharibu.

Kama fungu lipo, yeye mkuu wa mkoa na team yake waingia front aka nyapara style kwa mwezi mmoja kuhakikisha madarasa yamekamilika.

Ndani ya mwezi wahusishe wanasiasa wote kutoka vyama vyote, wamobilize manpower kutoka kwa wananchi wakujitolea hata sikunza weekend madarasa yajengwe.
 
Hii Haiwezekani baadhi y halmashauri kama Masasi, Mkurugenzi wao anapiga hela tu. Kila kitu ananunua yeye, hii inapelekea shughuli kutokwenda kwa wakati. Leo ameagiza wakuu walipie gharama za usafiri kwa mara ya pili... tena kwa gharama kubwa...
 
Hela za uviko?
Basi hongera sana kwa wote waliofanikisha tukapata hili fungu kwani sasa tunaona faida yake,
Wacheni mama akae angalau mpaka 2035
 
Waache ufanyaji kazi wa hivi. Tayari makosa yalishafanyika kwenye usimamizi, kuwapa saa48 ni chanzo cha kuzima moto na kuharibu.

Kama fungu lipo, yeye mkuu wa mkoa na team yake waingia front aka nyapara style kwa mwezi mmoja kuhakikisha madarasa yamekamilika.

Ndani ya mwezi wahusishe wanasiasa wote kutoka vyama vyote, wamobilize manpower kutoka kwa wananchi wakujitolea hata sikunza weekend madarasa yajengwe.
Masaa 48 yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ni sehemu ya Siku 60...

Hivyo hizo 48hrs ndani yake kuna extention ya muda..

Huu ni ujenzi ambao unafuata taratibu zote muhimu.. Tuache kutoa kauli za kupinga kama haupo na haujaona kinachoendelea huku field..

Majengo mengi yamekamilika bado tairiz, jipsam na milango tu.. Je hivyo vilivyobaki vinahitaji Mwezi mmoja??
 
Tairiz, jipsam na milango ndivyo vitakamilika ndani ya saa 48?
 
Hahahah yaani athari za huu ujenzi tutaziona mbeleni, yaani tofali siku tatu tu tangu ifyatuliwe inajengewa. Zima Moto at work
 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza Halmashauri zote mkoani humo kukamilisha majengo 452 ya madarasa ndani ya saa 48. Madarasa hayo 452 yamejenga na fedha za Uviko-19 na yapo katika hatua ya umaliziaji.

Akizungumza Desemba 7, 2021 wakati wa kupokea vyumba vya madarsa 22 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya, Gaguti amesema kuwa Halmashauri zote zinatakiwa kufanyakazi usiku na mchana ili kukamilisha madarasa hayo ndani ya saa 48.

Amesema kuwa madarasa hayo yanajengwa kwa fedha za Uviko-19 ambapo kwa Manispaa ya Mtwara Mikindani ampokea madarasa 22 yenye thamani ya Sh440 milioni.

"Nataka hadi kufikia Desemba 10 mwaka huu madarasa 452 yenye thamani ya Sh11.67 bilioni yawe tayari nimekabidhiwa fanyani kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo" ameagiza Gaguti

"Tuendelee kujenga majengo yetu kwa kasi hii hii ni dhambi kwa watumishi kupewa fedha za ujenzi wa miradi na kushindwa kukamilisha kwa wakati tunakuwa hatutendi haki kwa wananchi na Serikali pia"

"Tunazo zaidi ya Sh11 bilioni kwenye miradi ya afya na elimu nataka ikamilike kwa wakati ili shughuli zingine za maendeleo ziweze kufanyika ingawa kwa leo nakagua madarasa" amesema

Chanzo: Mwananchi
Saa 48 mbona nyingi sana, Rais Samia alikwenda Misri mwezi wa 11 akaongea na wawekezaji mwezi wa 12 kiwanda cha vifaa vya umeme tayari!
 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza Halmashauri zote mkoani humo kukamilisha majengo 452 ya madarasa ndani ya saa 48. Madarasa hayo 452 yamejenga na fedha za Uviko-19 na yapo katika hatua ya umaliziaji.

Akizungumza Desemba 7, 2021 wakati wa kupokea vyumba vya madarsa 22 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya, Gaguti amesema kuwa Halmashauri zote zinatakiwa kufanyakazi usiku na mchana ili kukamilisha madarasa hayo ndani ya saa 48.

Amesema kuwa madarasa hayo yanajengwa kwa fedha za Uviko-19 ambapo kwa Manispaa ya Mtwara Mikindani ampokea madarasa 22 yenye thamani ya Sh440 milioni.

"Nataka hadi kufikia Desemba 10 mwaka huu madarasa 452 yenye thamani ya Sh11.67 bilioni yawe tayari nimekabidhiwa fanyani kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo" ameagiza Gaguti

"Tuendelee kujenga majengo yetu kwa kasi hii hii ni dhambi kwa watumishi kupewa fedha za ujenzi wa miradi na kushindwa kukamilisha kwa wakati tunakuwa hatutendi haki kwa wananchi na Serikali pia"

"Tunazo zaidi ya Sh11 bilioni kwenye miradi ya afya na elimu nataka ikamilike kwa wakati ili shughuli zingine za maendeleo ziweze kufanyika ingawa kwa leo nakagua madarasa" amesema

Chanzo: Mwananchi
Miradi ikamilike kwa wakati na viwango stahiki na si vinginevyo.
 
Ndio maana wanatokea mashemeji zake akina Delta hawa akina Omcron sasa wewe pesa za kupambania Corona unazijengea madarasa tena kwa kuyalipua...zingeboresha sekta ya afya na kuimarisha disasters management ya korona

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Waangalie hizo amri zao watoto wetu wasije wakaporomokewa na matofali.
 
Back
Top Bottom