ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Matunda ya ziara ya Rais Samia Nchini Indonesia na Yale ya Rais wa Indonesia hapa Tanzania yamezaa matunda Kwa Wana Mtwara.
Ambapo kampuni ya kutoka Indonesia ya Essa Group of Industries imesaini MoU na Tanzania Kupitia TIC tayari kuanza uwekezaji wa Ujenzi wa kiwanda kikubwa Cha Mbolea Afrika chenye thamani ya $1.2 Bilioni( sawa na Shilingi Trilioni 3.2) ambacho Kitakuwa na uwezo wa Kuzalisha zaidi ya Tani Milioni 1 za mbolea ya Urea Kwa kutumia gesi ya Mtwara.👇👇
----
Ziara ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Nchini Indonesia yazaa matunda, Waziri Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ashuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi kiwanda kikubwa cha Mbolea Nchini
"Kuanzishwa kwa kiwanda hichi (kiwanda cha kuzalisha mbolea kitakachotumia gesi ambacho kinatarajiwa kujengwa mkoani Mtwara na wamiliki wake ni kampuni ya Essa group kutoka nchini Indonesia) ambacho tunatarajia kinaweza kikaanza rasmi kufanya production mwaka 2029 au kabla ya hapo, tunategemea sasa tutakuwa na uwezo wa uzalishaji wa mbolea ambazo zinaweza kusaidia kukidhi mahitaji ya ndani na kufikia ile azma yetu ya ajenda 10/30" -Joel
Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) Joel Laurent amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo, Jumatano Julai 31.2024 muda mfupi baada ya kushudiwa kwa utiaji saini wa uwekezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha mbolea mkoani Mtwara, hafla iliyofanyika Regency Hotel, jijini Dar es Salaam
Imeelezwa kuwa kukamilika kwa mradi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea kinachotarajiwa kujengwa mkoani Mtwara na kampuni ya Essa group kutoka nchini Indonesia kutapelekea kuzalisha tani za mbolea takribani milioni moja kwa mwaka, jambo ambalo litatengeneza ziada ya kuuza nje ya nchi kwa kuwa mahitaji ya nchi ni tani laki nane na elfu hamsini
Hayo yameelezwa na Abdallah Saad Kitete ambaye ni Mwakilishi mkazi wa kampuni ya Essa group alipozungumza na wanahabari leo, Jumatano Julai 31.2024, muda mfupi baada ya kushuhudiwa utiaji saini wa kiwanda hicho kitakachotumia gesi, hafla hiyo imefanyika Regency Hotel, jijini Dar es Salaam
Chanzo: Jambo online
My Take
Alifanya JK Kwa Ajili ya Wana mtwara kwa.kumleta Dangote na Sasa anafanya Rais Samia.
Ikumbukwe hiki Kitakuwa kiwanda Cha pili Cha Mbolea ambacho kina Ushawishi wa Moja kwa Moja wa Rais Samia, kingine ni intracom fertilizer company ltd Dodoma ambacho Rais Samia aliwashawishi Kampuni ya Burundi kujenga kiwanda Dodoma.
Hongera sana Rais Samia, juhudi zako huko kwenye ziara zinaonekana wazi.
View: https://www.instagram.com/reel/C-ID4MoO5gE/?igsh=MXMzeTVvcThqM3M3Ng==
Pia soma Rais Samia anatafsiri Tanzania ya viwanda kwa vitendo
Zaidi soma Mafanikio ya Rais Samia katika kujenga Tanzania ya Viwanda yaanza kuzaa matunda