Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala Leo Novemba 27,2024 ameshiriki zoezi la kupiga kura kwenye kituo cha Rest House kilichopo mtaa wa Shangani East Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.
Kanali Sawala amewahimiza wananchi wa Mtwara kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo la kupiga kura kwenye vituo vyao walivyojiandikishia ili waweze kuchagua kiongozi atakae leta maendeleo kwenye mtaa husika.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Aidha amewataka wananchi kupiga kura kwa utulivu na amani na baada ya kupiga kura watoke kwenye maeneo ya kupiga kura na kwenda kuendelea na majukumu mengine huku wakisubiri matokeo kwa mamlaka husika.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman,amesema mkoa huo uko salama kwenye vituo vyote 3734 vya kupiga kura