Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 2,318
- 8,464
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara, imemfikisha Mahakamani, Hakimu Mkazi wa Mtwara, Mussa Esanju kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi cha Sh. 50,000 kutoka kwa Mtuhumiwa mmoja aliyefikishwa mbele yake.
Hakimu Mussa amefikishwa Mahakamani na kusomewa makosa mawili ambayo ni kushawishi kuomba fedha Tsh. 200,000 na kupokea Tsh. 50,000, amesomewa makosa hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mtwara, Lucas Jang’andu.
Kwa upande wake Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo amesema Mtuhumiwa alikamatwa Aprili 5, mwaka huu eneo la Mangamba Tanki la Maji majira ya saa mbili usiku, akiwa na fedha ambazo ziliandaliwa maalum na mamlaka hiyo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mlalamikaji.
Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka amekana na kuachiwa kwa dhamana na kesi hiyo itatajwa tena May 18, mwaka huu.