DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Mimi niliwahi kusoma ktk moja ya shule za huko mkoani Mtwara. Hivyo naijua kiasi hasa pale Mtwara mjini. Enzi zile bahari na ufukwe ulikua mchafu sana. Yaani ilikua unaenda pale kivukoni (kivuko cha msanga mkuu) au huku beach unakuta matakataka tu yamezagaa. Pamoja nabupepo wote wa baharini lakini ufukwe ulikua unatoa harufu mbaya.
Sasa mwaka jana mwishoni nikabahatika kutembelea Mtwara mjini, nikastaajabu sana na hali ya ufukwe ilivyo safi, kuanzia pale Mikindan. Ikanilazimu niende kule kwenye soko la samaki nikajiridhishe nikakuta hali ya mazingiza ni safi tena safi sana, hamna uchafu uliokua unazagaa zagaa kwenye fukwe za Mtwara. Moja kwa moja nikasema haya ni matokeo ya kazi ya RC hapa. Itakua hili suala amelivalia njuga na hakika amefanikiwa.
Kwa hili, nasema wana Mtwara watamkumbuka sana Byakanwa..!!