Mtwara: Watu 151 wamekamatwa na kilo 82 za Bangi, lita 1915 za Gongo

Mtwara: Watu 151 wamekamatwa na kilo 82 za Bangi, lita 1915 za Gongo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, ACP Nicodemus Katembo amesema watu 4 kati yao walikutwa na Nyama ya Tandala kilo 21, Nyama ya Swala kilo 50 na Pembe za Ndovu vipande 4.

Pia, watuhumiwa walikutwa na mitambo 10 ya PombeHaramu, Televisheni 7, Jenereta 1, Kiyoyozi 1, Godoro 1, Mbao Asili 76, Majiko ya Gesi 2 na Pikipiki 2.

Kamanda Katembo amesema watuhumiwa wote wamefikishwa Mahakamani na taratibu nyingine za Kisheria zinaendelea dhidi yao.

==========================

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia watu 151 kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu huku wengine wakikutwa na bangi kg 82 na gramu 564 pamoja na dawa zinazodhaniwa kuwa za kulevya aina ya Heroine gramu 2.38.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema kuwa wa katika kipindi cha miezi miwili ya Septemba na Oktoba 2022 jeshi hilo limefanya msako na ukamataji wa makosa mbalimbali.

Alisema kuwa madawa yaliyokamatwa bangi kg 82 gramu 564 na watuhumiwa 47 pamoja na dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya aina ya heroine gramu 2.38 na watuhumiwa 5 ikiwemo na pombe ya moshi lita 1,915 na watuhumiwa 73.

“Vilevile Jeshi hilo limekamata watuhumiwa wanne wakiwa na nyara za serikalia ambazo ni nyama ya tandala kilo 21, nyama ya swala kilo 50 pamoja na meno ya tembo vipande vinne (8) vyenye uzito wa kilo saba (7) vilikamatwa,” amesema.

Amesema kuwa mitambo 10 ya kutengenezea pombe ya moshi na watuhumiwa tisa 9, mazao ya misitu (mbao) 76 nawatuhumiwa 2, pikipiki mbili 2 aina ya TVS.

Televisheni saba 7 zenye ukubwa tofauti jenereta mmoja, godoro moja, majiko mawili mawili ya gesi, viti vitano vya plastic pamoja na air condition moja ambapo watuhumiwa wote wameshafikiwa mahakamani.

MWANANCHI
 
Endeleeni kukamata gongo wakati hapo Airport watu wanatorosha mamia ya kilo za dhahabu kila siku.
 
Back
Top Bottom