Nimekuwa nikikerwa sana na tatizo la kuvuja kwa mitihani mashuleni, vyuoni n.k. Kwa muda mrefu nimekuwa nikifikiria njia mmbadala kukomesha tatizo hili. Nadhani kutumia mfumo ambao nitauitwa "Open Questions System" tunaweza kumaliza tatizo hili kabisa na kulifanya kuwa historia. Mfumo ninaoupendekeza utafanya kazi kama ifuatavyo;
1. Maswali yasiyopungua 200 yatatayarishwa kwa kila somo litakalofanyiwa mtihani na huwekwa bayana kwa watahiniwa wote mwanzoni mwa muhula.
2. Vitabu vya kutosha vyenye maswali ya mtihani vitachapishwa na kugawanywa mashuleni, vyuoni, bookstore, kwenye web n.k
Kwa mantiki hii maswali ya mitihani hayatakuwa siri tena hivyo nadhani hakutakuwa na haja ya kufanya njama/ hujuma ya kuiba mitihani.
Siku ya mtihani baraza la mitihani litawajibika kusambaza vitabu vipya vya mitihani kwa watahiniwa wote. Hii itasaidia kudhibiti ujanja wa kuandika majibu katika vitabu husika; Na asubuhi hiyohiyo wakati wanafunzi wamekaa kwenye madawati yao wakisubiri kuanza mitihani, baraza litakaa na kupitisha maswali ya mtihani na kuwasilisha namba ya maswali hayo kwa shule/ vyuo husika kwa njia ya simu, fax, e-mail etc.
Naomba mchango wenu wana JF kuhusiana na hili.