Muafaka ni utayari wa Taifa kuponya majeraha yake

Muafaka ni utayari wa Taifa kuponya majeraha yake

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Kuna nyakati bahari huwa sio nzuri sana na kuna nyakati bahari hutulia. Kama binadamu tunatakiwa kujua nyakati zote hizo. Captain mzuri anajua kucheza na mawimbi na kuongoza meli vizuri bila kuzama. Maisha yana changamoto zake mpaka mwisho wa uhai wetu natumaini tutakuwa tumejifunza kitu kuhusu maisha. Mtu ambaye anaishi na hajajifunza kitu kuhusu maisha ni kama mtu ambaye hajawahi kuishi kabisa duniani.

Wajibu wetu kama binadamu ni kutafuta maarifa na kuyarithisha maarifa kwa kizazi kingine. Maarifa ni muhimu kuliko kitu chochote kwasababu yanatufanya tuishi maisha yaliyobarikiwa. Kuwa na pesa bila maarifa ni tatizo kwa mtu makini atatufuta vyote kwasababu maarifa humfanya mtu kuishi maisha mazuri yasiyo na mikwaruzano. Maafa mengi binadamu anayokutana nayo ni sababu ya ujinga na kushindwa kutambua kilicho bora na chenye manufaa.

Jamii yoyote ikitaka kuendelea haina wajibu kutafuta maarifa kwasababu ujinga ni kifo. Matendo yanayotokana na ujinga huadhibu ili tuishi vizuri hatuna wajibu tutafute maarifa kama tutafutavyo pesa.

Hivi vitu viwili lazima viende pamoja maarifa na pesa ili upate heshima lazima uwe navyo vyote.

Kama tunavyoangaika kutafuta pesa tusisahau kutafuta maarifa yatakayo tusaidia tuishi vyema katika jamii zetu, katika familia na katika Taifa.

A well harmonius society ni ile ambayo watu wake wameelimika na wanatenda matendo yaliyo sahihi kutokana na elimu yao.

Wenye Hela wanatakiwa watafute Mental ambaye atakuwa mshauri katika storms za kila siku za maisha. Yule ambaye anaamini ata m guide katika right direction.

Katika maisha kila mtu amebarikiwa na kitu chake kuna waliobarikiwa hela kuna waliobarikiwa akili sio kila wakati wenye akili huwa na pesa. Kwahiyo binadamu hutegemeana nafikiri ni muhimu sisi kama binadamu kuheshimiana na kutumia kipaji cha kila mmoja wetu alichobarikiwa nacho.

Kuna wajenzi kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kivita, kuna madaktari, kuna mainjinia watu wote hawa wanatengeneza kitu kimoja ambacho kama tukitumia vipaji vyetu vizuri kitakuwa na faida kwa taifa.

Ni ushirikiano wetu tu ndio utatutoa kama taifa na kama mtu mmoja mmoja kama hatushirikiani tusahau kuhusu Tanzania kutoka kwenye umaskini.

Ili tutoke na tuendelea kama taifa ni lazima tushirikiane hili jambo ni muhimu pasipo mashirikiano hakuna harmony. Kwahiyo ni wajibu wetu kujenga jamii yenye mashirikiano na inayojitambua ni nini ina kijenga.

Kwasasa tunaishi kama watu ambao sio taifa moja ni wajibu wetu kujenga jamiii zetu na ni wajibu wetu kutaka kuona jamii zetu zikiendelea.

Ni lazima tukubaliane ya kwamba tabia tunazozijenga kwasasa katika taifa letu hazina manufaa kwetu na wale hazitufanyi tuwe wamoja tumegawanyika.

Hautuwezi na kamwe hatutaweza kujenga taifa hili katika ubinafsi ikiwa kila mtu anajiangalia mwenyewe na familia yake au kundi analotoka.

Mapenzi yetu kwa jamii yameondoka kumekuwepo na mapenzi ya ubinafsi nchi haiwezi kufanya kazi hivi.

Shule za serikali na za jamii zimeachwa kama hazina mwenyewe hivi tutawezaje kujenga jamii bila elimu bora? Au ndio tunakaribisha ujinga ambao ni hatari sana kwa ustawi wa taifa na jamii kwa ujumla.

Elimu yetu ni muhimu kujenga tabia za watu wetu kinyume cha hapo elimu yetu haitokuwa na manufaa kwetu kama haito m shape mtu kuwa raia mwema.

Haya mambo ni ya msingi yanahitaji kila raia kutafakari kwasababu yanahusu baadae yetu kama taifa. Baadae ya taifa hili tutaitengeneza sisi kwa fikra zetu na matendo yetu tunawajibu wa kuitayarisha.

Ni muhimu kutambua kila mmoja wetu anawajibu kwa taifa hili. Kulilinda na kuhaikikisha liko salama. Ila kwa tabia ambayo inaonekana kwa sasa ya ulafi wa madaraka ili kupata mali inasikitisha. Care of the citizen ni attribute ya a good leader na sio kuingia madarakani kujikusanyia na kisahau raia ni muhimu viongozi wakabadilika.

Naomba tutafakari kwa pamoja maajaliwa ya taifa letu na mwelekeo ambao tunapaswa kuelekea kwa sasa kama taifa. Tuchanganue changamoto tulizo nazo kwa sasa na majawabu yake ili tutibu majeraha yanayotukabili kama taifa.

Kwasababu pasipo kutibu majeraha yaliyopo taifa halitoweza kupona tunahitaji kuwa wamoja ili taifa hili lisonge mbele kila mtu ni muhimu sana kwa ukuaji wa taifa lolote.

Muafaka sio jambo la mtu mmoja au wawili au vyama viwili vya siasa bali ni utayari wa taifa kuponya majeraha yake na kuwa tayari kuanza upya. Kwa sasa hili halipo hata kwa sasa tunapoandika katiba mpya hatutotibu chochote.

Watu wataendelea kuwa mafisadi na walafi, wabinafsi na wachoyo mpaka tutakapo kubali kubadilika nafsi zetu na kutambua sisi ni wamoja na baadae yetu ni moja kama taifa.
 
Back
Top Bottom