Waungwana,
Kenya matatizo yao yalitotokea katika uchaguzi wa Dec, 2007 waliweza kuyamaliza kwa muafaka na kuunda serikali ya mseto. Zimbabwe matatizo kati ya vyama vya ZANU-PF na MDC yamemalizwa kwa muafaka na kukubaliana kuundwa serikali ya mseto. Je, huu muafaka wa CUF na CCM utafikiwa lini? JMK yuko serious kweli kuona muafaka huo unafikiwa au ni anafanya usanii wa kuchelewesha muafaka huo usifanyike mpaka hapo baada ya uchaguzi wa 2010?
Na CUF hawautaki mseto ndio maana wameondoka mezani na hawatorudi tena ,kwani walipopahitajia wamepapata ,si mnaona CCM ndio wanaokwenda mbio kutaka kuwarudisha kwenye meza ,hivi Jeuri ya CCM imekwenda wapi ,naomba mjiulize kwa nini kwa wakati huu tulio nao only CCM ndio wanaosikika kupiga makelele eti warudi mezani kuendeleza pale walipo ishia ,hivi walisahau kama mazungumzo yalikwisha kufungwa na waraka wa yaliokubaliwa kusomewa wananchi kwenye mikutano.
Ila hapa CCM Tanganyika wanataka kupindisha mambo yanayohusu Taifa (Zanzibar ni nchi au si Nchi) ,wanataka kutumia mambo ya muafaka kuwagawa tena Wazanzibari baada ya kuona wameungana kudai uhuru wa nchi yao kutoka kwa mkloni Tanganyika.
Zimbabwe kweli kulikuwa na tatizo na lilihitaji suluhisho kama lililopatikana. Halikadhalika Kenya. Lakini Zanzibar hakuna tatizo kama hilo. Si umeona kuwa kama wao wanaelewana (hoja ya Bango la Zanzibar ni Nchi au si Nchi). Wao wa CUF na CCM hawahitaji suluhisho kama la Zimbabwe, Kwanza hakuna matatizo kule isipokuwa matatizo ni ya kupangwa. Wewe ( na wenzako wengine wa Tanzania Bara)wala wasikushughulisheni hao.
Siasa za Zenj zimejaa vijembe na hasa wakati wa kampeni... lolote linawezwa kusemwa ili mradi kubeza upande wa ushindani na kufurahisha umati kama si kuuvuta. CUF na CCM wanajuana vizuri na inapofika wakati wa kurushiana vijembe mengi husemwa kiasi cha kuweza kumshangaza mtu asie kuwa na ufahamu wa vijembe hivyo...
Mhe Karume jr aliwahi kunukuliwa kwenye kampeni za mwaka 2005 akisema hata kama wazanzibar wote wakipigia kura CUF kura yake na ya mkewe tu zinatosha kuwaingiza ikulu. Pia akaenda mbali kidogo akasema ikiwa CUF watachukua nchi watatumia mapanga na silaha walizotumia Jan 24 1964 kwani wanazo wamezihifadhi.
Wasalaam
Unaposema zanzibar hakuna matatizo sijajua una maana gani! au unataka yatokee makubwa kuliko ya 2001?ndio ujue kuwa kuna matatizo? tafadhali tueleze tukuelewe Mkuu Ndivyo ilivyo.
Siasa za Zenj zimejaa vijembe na hasa wakati wa kampeni... lolote linawezwa kusemwa ili mradi kubeza upande wa ushindani na kufurahisha umati kama si kuuvuta. CUF na CCM wanajuana vizuri na inapofika wakati wa kurushiana vijembe mengi husemwa kiasi cha kuweza kumshangaza mtu asie kuwa na ufahamu wa vijembe hivyo...
naona Wazenj wapo usingizini wala hawaamki na wakiamka game ishageuzwa, lete maneno kibunango kwasasa ndio kwisha hebu niambie wale waliopindua wanatoka wapi ? na wapo wapi nyinyi mnapiga kelele tu kama kuna kura ya maoni basi two third ni watanzania wanaoishi zenj sasa mlie
Nimesema matatizo yaliyopo ni yale ya kupangwa (au kutengenezwa makusudi ili yaonekane yapo). Haya si aina ya matatizo ambayo unaweza kuyafananisha na matatizo halisi kama yale ya Kenya au Zimbabwe.