Mamshungulii
Senior Member
- May 3, 2023
- 175
- 88
MUAFAKA WA MAAMUZI JUU YA UKUSANYAJI WA MAPATO BADO NI UTATA MTUPU
Kufuatia kauli za Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya tarehe 17/5/2023 akiwa anaongea na Wafanyabiashara wa Kariakoo ipo haja ya kupatiwa muarobaini wa haya masuala kusudi kama taifa tusiendelee kupoteza mapato kwa baadhi ya watumishiwa umma kutokuwajibika ipasavyo,Waziri mkuu alisema, ‘‘Kwanza hakuna mtumishi wa serikali ambaye anapaswa kumdharau kiongozi wake wa juu,Raisi wetu wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania ,Makamu wa Raisi hata waziri ,popote anaposimama, hilo lililotamkwa na yeye ni agizo Leo TRA ,Rais amesema kodi za miaka 5 iliyopita huko …mziache …nyie mnadai barua kwa watu wa Kariakoo. Mtu wa Kariakoo ataipata wapi barua ya Rais?’’
Ukusanyaji wa Mapato na Matumizi ya Serikali za Mitaa Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ibara ya 145 (2) ya katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ,1977, inasema “bunge au baraza la wawakilishi, kadri itakavyokuwa, litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo vya Serikali za Mitaa, miundo na wajumbe wake, njia za mapato na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo”.
Ukusanyaji wa Mapato, Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 (The Local Government Finances Act, 1982) imeainisha vyanzo vya mapato kwenye Halmashauri za Wilaya Na Vijiji. Serikali za Mitaa zinapata mapato yake kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Vyanzo hivi ni pamoja na fedha zitokanazo na biashara, viwanda, huduma, ada ya leseni, ushuru, vibali, nk. Baadhi ya makusanyo ya mapato katika Serikali za Mitaa yanafanywa na taasisi za Serikali Kuu (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).
Matumizi ya Fedha Pamoja na kwamba fedha hizi zinakusanywa kutoka kwenye Serikali za Mitaa, matumizi yake yanaamuliwa na Serikali Kuu (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Makusanyo ya serikali za mitaa hubaki serikali za mitaa isipokuwa makusanyo ya kodi ya ardhi. Makusanyo ya kodi ya ardhi yanayokusanywa na serikali za mitaa hugawanywa na Serikali kuu. Katika mgao huo Serikali kuu hupata (70%) inayopelekwa hazina kuu na matumizi yake kuamuliwa na Serikali Kuu (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), wakati Serikali za Mitaa hupata 30%.
Waziri anayehusika na Serikali za Mitaa baada ya kushauriana na wadau wengine anaweza kuamua mgawanyo wa vyanzo vya mapato kwenye ngazi tofauti za halmashauri. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982. Serikali za Mitaa hazina uhuru wa kujiamulia matumizi ya makusanyo yanayopatikina katika maeneo yao, badala yake ni lazima wapate idhini ya waziri ambae anatoka Serikali Kuu (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).
Kwa upande mwingine nchi zingine kama Kenya Katiba yao (ibara ya 209 na 210) imeweka mgawanyo wa madaraka ya kukusanya mapato 14 na kodi kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Ibara ya 202 na 203 ya Katiba ya Kenya inatoa mwongozo wa namna ya kugawa mapato kati ya Serikali mbili yaani Serikali kuu na Serikali za Mitaa. Ibara ya 187 na 176 zinatoa mwanya na nafasi kwa serikali kuu kupeleka baadhi ya majukumu yake (Serikali kuu) kwenda Serikali za Mitaa. Ibara ya 204 inatoa fursa ya mgawanyo sawa wa mapato na rasilimali kwa maeneo yaliyoachwa nyuma kiuchumi.
Ardhi na Uhifadhi wa Mazingira Serikali za Mitaa zina nafasi kubwa sana katika usimamizi wa Ardhi na Uhifadhi wa Mazingira. Ingawa Sheria za nchi zimetoa fursa na majukumu ya Serikali za Mitaa katika usimamizi wa Ardhi na Uhifadhi wa Mazingira, lakini Katiba ya sasa haijasema chochote katika masuala haya muhimu kwa maisha ya binadamu. Katiba za nchi nyingine kama Kenya zimeweka bayana nafasi za Serikali kuu na Serikali za Mitaa katika usimamizi wa Ardhi na Uhifadhi wa Mazingira.Hii inaonyeshwa katika ibara ya 69 na 70.
NINI KIFANYIKE
• Serikali za Mitaa zisiingiliwe na Serikali Kuu (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) na ziwe na uhuru kamili wa kujiamulia mapato na matumizi yake ikiwemo wajibu wa kuchangia hazina ya Serikali Kuu (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).
• Sehemu kubwa ya mapato yatokanayo na makusanyo kwenye Serikali za Mitaa yatumike katika eneo husika.
• Ziwepo mamlaka/taasisi katika Serikali za Mitaa ambazo zitakuwa na jukumu la kukusanya mapato katika halmashauri.
• Serikali za Mitaa ziwe na vyanzo vyake vya mapato kwa ajili ya halmashauri husika na kuwa na uwezo wa kuandika bajeti ya halmashauri yake yenyewe na si kutegemea mwongozo wa bajeti kutoka serikali kuu (ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) na sehemu ya mapato yake kupelekwa hazina kama ilivyo kwa sasa.
• katiba mpya inapaswa iangalie namna ya kujifunza kutoka Katiba za nchi zingine mfano katiba ya Kenya hasa mambo yaliyomo katika ibara ya 202 (kugawana mapato kwa haki na usawa-equitable sharing of revenue), 203 (masuala muhimu ya kuzingatia katika mgawanyo wa mapato ya Taifa mfano maslahi ya Taifa), 209 (mamlaka ya kutoza Kodi ya Mapato itafanywa na Serikali kuu tu) na ibara ya 210 (mamlaka ya kutoza kodi au ushuru yatokane na Sheria kuu-Parent Act).
• Umuhimu wa kuwa na katiba yenye Serikali mbili huru yaani Serikali kuu (central Government) na Serikali za Mitaa (local government) zenye uhuru wa madaraka na maamuzi.
• Katiba mpya iangalie mfano wa nchi zingine kama Kenya Chile kwa kuweka bayana nafasi za serikali kuu na serikali za mitaa katika usimamizi wa ardhi na uhifadhi wa mazingira.

Upvote
3